Awamu Ya JK Kwenye Televisheni Ya Sweden; Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Awamu Ya JK Kwenye Televisheni Ya Sweden; Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jul 29, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  Katika miezi ya karibuni, nchi yetu Tanzania, katika hali isiyo ya kawaidia kwenye media ya nchi za Magharibi, mara kadhaa imezungumzwa katika sura chanya kwenye vyombo vya habari vya nchi ya Sweden ikiwamo televisheni yao ya taifa.


  Huko nyuma nimepata kukaa Sweden kwa miaka kumi na miwili; 1992-2004 sura ya Tanzania iliyokuwa ikionyeshwa kwenye media ni kuwa ni moja ya nchi masikini Afrika na inayotegemea misaada ikiwamo misaada kutoka nchi ya Sweden tangu miaka ya 1970. Ni kama mtoto anayenyonyeshwa kila anapolia njaa.


  Lakini, katika mfululizo wa vipindi vya Televisheni “ Det Nya Afrika"-ikiwa na maana ya ' Afrika Mpya' vilivyoonyeshwa mapema mwaka huu kwenye televisheni ya taifa ya Sweden, mwandishi Erica Bjorstrom alitembelea Tanzania mara kadhaa. Mwandishi huyu anaitaja Tanzania kuwa mfano mzuri wa nchi iliyoanza kusimama na kuinuka kiuchumi. Unaweza kuona moja ya vipindi hivi kwa lugha ya Kisweden ukitembelea; Tanzania: Välståndet växer - Rapport | SVT Play


  Kwa mujibu wa mwandishi huyu, uchumi wa Tanzania ni moja ya uchumi unaokua kwa kasi kubwa barani Afrika. Kwamba uchumi wa Tanzania unakua na hali za maisha ya watu zimeanza kuwa bora. Inasemwa , kutokana na kukua huko kwa uchumi na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na kodi,Tanzania imeanza hata kufikiria kutoa malipo ya pensheni kwa wasio katika mfumo rasmi wa ajira kwa mfano wakulima.


  Mwandishi huyu anatoa sababu mbili zinazopelekea Tanzania kuinuka kiuchumi; Mosi,Tanzania imetoka kwenye mfumo wa chama kimoja na kuingia kwenye vyama vingi, pili, kuwepo kwa mfumo wa soko huria na kuruhusu watu kuendesha shughuli za viwanda na biashara.


  Mwandishi huyo wa televisheni anatoa mfano wa moja ya viwanda vya kampuni ya Azam; ni kiwanda cha kusindindika matunda. Kwamba kinachangia kuinua uchumi wa nchi kwa kutoa ajira, kununua mazao ya wakulima na hata kuchangia uchumi wa Sweden kwa vile kampuni ya vifaa vya viwandani ya Sweden, ABB inauza vifaa na vipuri vya viwandani kwa kampuni hiyo ya Azam.


  Katika moja ya vipindi hivyo vya televishen mwandishi huyu Erica Bjostrom anaongea na gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu . Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anatoa picha ya Tanzania iliyojizatiti kuinua uchumi wake kwa kujenga uchumi unaotegemea sekta nyingi.


  Pia mwandishi huyo anamhoji Balozi wa Sweden nchini Tanzania , Bw. Lennarth Hjalmaker ambaye anakubali kuwa uchumi wa Tanzania unakua na kuwa Sweden, kama nchi, imeanza kujipanga kubadili aina ya misaada inayotoa kwa Tanzania. Sweden sasa inafikiria zaidi katika kuisaidia Tanzania katika maeneo ya biashara na viwanda.


  Hayo ni machache tu katika mengi mazuri ambayo Tanzania na hususan utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete umepambwa nayo na mmoja wa nchi wafadhili wakubwa wa Tanzania tangu tupate uhuru, Sweden. Ni sifa ambazo nilikutana nazo kutoka kwa baadhi ya raia wa Sweden tangu siku ya kwanza nilipotua Sweden yapata majuma sita yaliyopita.


  Ni mtazamo huo chanya wa kimaendeleo ya kiuchumi kwa Tanzania kutoka kwa watu wa kawaida wa Sweden ndio ulionifanya nipekue mtandaoni kuona ni nini hasa kilichoripotiwa na vyombo vya habari vya Sweden juu ya Tanzania.


  Tafsiri yangu;

  Vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kuathiri mitazamo ya watu . Kazi ile ya mwandishi Erica Bjostrom imechangia kuifanya Tanzania, machoni mwa watu wa Sweden kuwa ni nchi yenye kuleta matumaini ya kuwa mfano wa taifa la Kiafrika linalopiga hatua kutoka hali ya ukale na kuingia kwenye kuwa taifa la kisasa zaidi. Mara nyingi, hilo la mwisho ndilo lenye kuiletea nchi na watu wake heshima zaidi.

  Na taifa la kisasa ni lile lenye kuheshimu misingi ya utawala bora ikiwamo kuamini katika demokrasia ya mazungumzo na si ya virungu . Taifa la kisasa ni taifa lenye kuruhusu uwazi zaidi na si kuruhusu usiri hata kwenye masuala ya msingi yenye maslahi kwa umma. Mfano hapa ni uwepo wa mikataba ya siri. Ni mikataba yenye kuhusu rasilimali za wananchi kufanywa kuwa jambo la siri.


  Ndio, taifa la kisasa lazima liachane na ubaguzi wa kisiasa. Tanzania, tangu awamu ya kwanza imeendesha siasa za kibaguzi ikiwa na maana kuwabagua wale wote wenye fikra tofauti na kuwapiga mihuri ya wasaliti, wapinzani na majina mengineyo. Na tunayoyavuna leo ikiwamo ufisadi uliotamalaki unaolitafuna taifa ni matunda ya ubaguzi wa kisiasa ambao mbegu zake zimepandwa miaka 50 iliyopita.


  Tumekuwa ni watu wa hovyo hovyo. Watu tusiotanguliza maslahi ya taifa bali ya chama, na hakika si ya chama, bali maslahi binafsi na ya kimakundi. Ni watu wa hovyo hovyo tunaotanguliza udini na ukabila badala ya utaifa.

  Kwenye makala ya ’ Neno la Leo’ niliyoandika usiku wa kuamkia leo nimesimulia kisa cha Mfalme Ihsani kwenye nchi ya bahari ya giza.

  Ndio, popote panapotokea maendeleo makubwa na ya haraka, basi, hutokea pia mabadiliko yenye kuyakwaza na kuyavunja maendeleo hayo. Ni mambo yenye kusababishwa na ubinafsi, chuki, husuda, fitina, wivu na siku hizi kuna neno mizengwe pia. Yote hayo ndio haswa ’ Magamba’ tuliyo nayo Watanzania. Hayo si magamba ya chama cha siasa tu. Ni magamba ya kitaifa.Kuyavua hayo sharti ukokwe moto ili kuipasha moto kwanza miili yetu!


  Tufanye nini?


  Umefika wakati sasa kwa Chama na Serikali iliyopo madarakani ijenge ujasiri wa kukubali kuwa Tanzania ni muhimu zaidi kuliko Chama cha siasa au watu mmoja mmoja. Kiandae mazingira yasiyokuwa na mizengwe ya kuandaa Katiba itakayowatoa Watanzania walio wengi kwenye umasikini wa kudhalilisha unaotokana na ubaguzi wa kisiasa. Maana, nchi yetu ni nchi tajiri sana ila watu wake ndio masikini kutokana na maovu ya wachache tuliowapa dhamana ya kutuongoza.


  Ona Finland . Haka ni ka- nchi kadogo sana katika dunia hii. Lakini ni moja ya nchi tajiri sana na ambazo Tanzania kama nchi, viongozi wake hupita huko kutembeza bakuli la ’ Saidia Masikini!’.


  Ndugu zangu,

  Ka- nchi ka Finland kale uchumi wake ulianza kwa kutegemea miti ya mbao nyepesi. Hawana miti ya mpingo wala misonobali. Lakini kwa vile hawaendekezi ubaguzi wa kisiasa na kuwa wanatanguliza maslahi ya nchi yao, wameweza kujenga miundo mbinu imara ikiwamo ya hata akilini kwa maana ya elimu.

  Sisi Watanzania tuna miti ya mipingo, dhahabu, almasi, gesi asilia, uranium, makaa ya mawe, Tanzanite,mito, maziwa, bahari, mbuga za wanyama na mengine mengi. Lakini bado tunaona hata fahari kujitambulisha kuwa; ” Sisi ni nchi masikini bwana!”

  Na tuna viongozi wanaosimama hadharani na kutamka kuwa ni vizuri tukabaki na mfumo wa chama kimoja. Vyama vingi vitatuletea vita!”
  Na kiongozi mwingine katika kuendekeza ubaguzi wake wa kisiasa anatamka hadharani; ” Ukitaka biashara yako ikuendee vizuri njoo CCM!”

  Ni fikra kama hizi za ukale ndizo zitakazomfanya mwandishi Erica Bjostrom na wengine wa dunia hii kurudi tena Tanzania na kuripoti habari ya nchi ya Tanzania iliyoonyesha dalili za kusimama na kukimbia, kuwa sasa inaangamia tena kwa machafuko ya kisiasa na watu kuuana. Na sababu kubwa itakuwa ni ubaguzi wa kisiasa wenye kujenga misingi ya hila katika chaguzi.


  Naam, wahenga walinena; ngoma ikivuma sana hupasuka. Ndio maana ya kusema; Pavumapo palile, si kazi kudamirika!


  Maggid


  Sweden,

  Ijumaa, Julai 29, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huyo mwandishi akija sasa akiona hicho kiwnada cha Azam kinavyoa thirika na mgao wa umeme sijui atasemaje.

  Kuna washikaji wanakosa ujira wao roba za mbao zinaweza kongezekaa kwa kasi sababu hawa wanaofanya kai za 2000 kwa siku wasipoata ujira halali wao tayari kufanya chochote wasiose mlo.

  Pamoja na hizo sifa yaliyofanyika ni machache sana tofauti ya yale ambayo hayajafanyika. Kama wewe umeridhika na hoja za huyo mwandishi basi nawe una tazama mambo kwa jicho moja.........

  Mbona wasweeden hawaji kuwekza sana TZ? . Mfano k wenye sekta ya misitu? Umejaribu kumuuliza huyo msweeden kwa nn makampuni ya kisweeden waliyonunua Tanzania. hayafanikiwi. Mfano TANSCAN.......
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Sasa mbona thread title yako unampamba JK?
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu sometimes your good halafu kipindi cha uchaguzi umesahau kabisaa kuwa wewe ndo ulikuwa mbaguzi na mnazi mkubwa wa ccm!
  but nashukuru kwa hili kuimiza utaifa mbele! mwambia JK sasa nadhani atakuelewa tuu, si unajua wanamsemo wao wa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine badala ya MWISHO WA UCHAGUZI NI KUFANYA KAZI KUTIMIZA AHADI!
   
 5. m

  maggid Verified User

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Camaraderie,
  Hiyo ni tafsiri yako, una haki nayo hata kama sikubaliani nayo. Lakini hapa nitaongeza juu ya tafsiri ya alichosema kiongozi yule, kuwa; Ukitaka biashara zako zikunyokee, njoo CCM". Ana maana kuwa " Ukitaka kukwepa kodi pia, njoo CCM, tutakulinda!" Na maana yake, mfanyabiashara yule akiwa upande mwingine wa kisiasa, basi, atatumiwa sungusungu wa kodi. Naam, atabambikiwa kodi hadi biashara yake ife! Na hiyo ndio tafsiri ya ubaguzi wa kisiasa ninaouzungumzia.
  Maggid
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Jamaa hawana huruma hawa. Yaani kweli wanataka tuamini kuwa mambo yetu yako poa?? Mimi naona mwandishi anatafuta namna ya nchi yake kupunguza misaada kwetu kwa vile kaona hela zao zinatumiwa ovyo. Haiingii akilini nchi inayosifiwa bajeti yake ndiyo inazidi kutegemea wahisani zaidi kuliko huko nyuma.
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Hawa watu hawawezi kutusifia bila ya kuwepo uwezekano wa maslahi kwao. Pengine wameona kuna mianya mingi sana kimaslahi kwao kwenye awamu ya JK kuliko awamu zingine. Hata mtu akimsifia mkeo kwa urembo wake jua liko jambo.
   
 8. K

  Karata JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mkuu mbona unamwita Mwanakijiji wakati hii thread ni ya Maggid na mpaka anapomaliza kutoa hoja anaandika jina lake Maggid.

  Camaraderie,
  Hiyo ni tafsiri yako, una haki nayo hata kama sikubaliani nayo. Lakini hapa nitaongeza juu ya tafsiri ya alichosema kiongozi yule, kuwa; Ukitaka biashara zako zikunyokee, njoo CCM". Ana maana kuwa " Ukitaka kukwepa kodi pia, njoo CCM, tutakulinda!" Na maana yake, mfanyabiashara yule akiwa upande mwingine wa kisiasa, basi, atatumiwa sungusungu wa kodi. Naam, atabambikiwa kodi hadi biashara yake ife! Na hiyo ndio tafsiri ya ubaguzi wa kisiasa ninaouzungumzia.
  Maggid
   
 9. m

  maggid Verified User

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Karata,
  Hata mie nimeshangaa, lakini nikaamua kubaki kimya kuendelea na mengine. Ahsante sana!
   
Loading...