dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,954
- 9,474
Serikali haina HELA za kulipa wakandarasi sisi wengine tumezikimbia hizo kazi Jiwe alikuwa anatumia ulaghai hakuwa na Hela hizi anazofanya January ni sarakasi tu unaamini kwamba Tanzania hakuna Crane ya Tani 26?Kwanza nianze kwa kusema mimi si mpenzi mkubwa wa Rais wetu aliyepita, JPM.
Hata hivyo, pamoja na figisu nyingi za JPM katika mambo mbali mbali, mengine ambayo yalikuwa miradi ya upendeleo ulio wazi kimaeneo, katika mradi wa bwawa la umeme Stieglers alikuwa spot on.
Mradi wa ujenzi wa bwawa la kuweza kufua umeme la Nyerere Hydropower(Stieglers Gorge), ni kati ya miradi ya kimkakati yenye matokeo yanayoweza kuleta mapinduzi ya uchumi kwa miaka mingi ijayo.
Katika hili, nampongeza JPM kama ambavyo nimempongeza mara kadhaa huko nyuma.
Maneno maneno tunayosikia toka kwa Waziri wa sasa wa Nishati, Januari Makamba, yanatutia wasiwasi juu ya azma kukamilisha ujenzi wa bwawa hilo kwa wakati.
Tunajua naye JPM aliupa kisogo mradi wa uendelezaji wa uchimbaji wa gesi kwa matumizi ya uzalishaji umeme.
Lakini Waziri Makamba awe careful katika kutekeleza miradi hii ili yote yakamilike kwa manufaa ya nchi, Tanzania.
Haya maneno maneo …………..mara oooh, maji hayajazwi kwenye bwawa leo wala kesho,………… mara mradi uko nyuma, …………….mara mkandarasi hawezi kazi,
hayo wananchi hatupendi kuyasikia.
Tunachotaka kusikia ni lini mradi unakamilika, na tupate umeme wa bei chee.
Tunajua figisu kati ya JPM na baba yake January, Yusufu Makamba, lakini ni vyema tukayaweka hayo nyuma yetu na tugange yajayo, afterall JPM sasa hayupo.
Tunataka mradi wa JNHPP (Julius Nyerere Hydropower Project) ukamilike kwa wakati.
(NB: Tunasikia kutoka kwa ka nzi, kuwa kuna wakubwa wamejipanga kuingiza figisu kwa makusudi mradi huu)