Awamu ya 6: Tusije zembea ujenzi wa Bwawa la uzalishaji umeme Stieglers Gorge

Gesi ya Mtwara ni yetu kama ilivyo madini mengine. Tunagawana mapato na wale wenye uwezo wa kuiendeleza. Mkiingia kichwa kichwa faida yote watachukua wao.

Amandla...
Gesi ya Mtwara si yetu, huu ni ukweli. Gas ni Mali ya mwekezaji aliyechimba.
Sisi tunanunua kwao kwa Bei ya soko, alafu tunachopata ni Kodi kutoka kwao.
Mwekezaji akirudisha gharama za uwekezaji ndio inakua Mali yetu, swali ambalo hata ccm wenyewe hawana majibu ni je itachukua miaka mingapi mwekezaji kurudisha gharama zake
 
Wishful thinking. Makampuni ya Symbion yalikuja baada ya uzalishaji kupungua kutokana na ukame na kujaa matope kwenye mabwawa. Hali hii itajirudia Stiegler. Ndio maana EIA ilikataa na hamna mwekezaji wa maana kwenye huyu tembo mweupe.

Amandla...
Kuhusu mabwawa kupungua kina ilikua ni propaganda tu ya kuhalalisha symbion kutuuzia umeme.
Linatengenezwa tatizo ili watu wapate nafasi ya kuleta kampuni ituuzie umeme alafu wachukue 10%
Hilo ndio kinafanywa na serikali ya CCM
Kuhusu kuwa inaweza kutokea Tena kwenye stieglers gorge au laa hiyo hatujui.
Kwa nini hakuna mwekezaji wa maana huko, sababu ni kuwa hili bwana ni letu halimilikiwi na mtu yoyote.
Wawekezaji hawawezi kupenda hii project kwa kuwa ikatokea tukawa na umeme wa uhakika Ina maana hatutaweza Tena kununua umeme kutoka kwao.
 
mkuu Shida umeme ulipokuwa unaozalishwa na maji ulikuwa kidogo sana ndio ikapelekea kuuziwa umeme na Yale makampuni akina symbion, Dowans n.k
Hiyo ndio ikapelekea bei kuwa juu.
Waondoe makampuni yanayotuuzia umeme, alafu tuzalishe umeme wa maji kwa wingi hapo bei itakua ndogo.

Kwa sasa naomba nitunze tu huu uzi, kisha umeme wa maji utakapoanza kutumika nione kama tutanunua unit moja chini ya shilingi 100. Isije ikawa kama hizi ndege zetu, lakini nauli ni juu kuliko fastjet.
 
Wewe ndio hujapitia sayansi. Nothing is constant in the universe. Hata universe yenyewe inapanuka.

Amandla...
Mkuu tusilishwe vitu na tukakariri tu.
North Korea na China leo wamefika mahali ilipo by NOT believing an thing the West has thrown at them.
3 Gorges Dam la China is a good example.

Sisi tukiambiwa Rufiji itakauka, tunaamini mazima mazima.
 
Mkuu huo umeme wa maji ni rahisi umeonea wapi? Au unatumia umeme tofauti na huu tunaotumia sisi wengine? Maana hao wataalamu wanasema umeme wa maji unapaswa kuwa shilingi 36 per unit, ila kwa sasa ni karibu kabisa ya 350+VAT. Swali si umeme wa sasa maana tunatumia na gas humo humo. Je tuliwahi kununua chini ya shilingi 200 kwa unit huko nyuma kabla ya kuanza kutumia umeme wa mafuta mazito, since gas ilianza 2014 na kuendelea.
Mkuu
Hiyo shilling 400 bado ni rahis maana tunalipia na madeni ya iptl escrow na richmondi na ufisadi humohumo. Ila kimsingi kama tunalipa 400tsh wa gas tutalipa 2000 per unit.
 
Kwa sasa naomba nitunze tu huu uzi, kisha umeme wa maji utakapoanza kutumika nione kama tutanunua unit moja chini ya shilingi 100. Isije ikawa kama hizi ndege zetu, lakini nauli ni juu kuliko fastjet.
Umeme wa maji ni umeme rahisi, shida iliyopo ni viongozi tulionao.
Bwawa linaweza kuisha na umeme ukazalishwa lakini badala ya kushuka Bei ndio ikapanda.
Kwa nini inaweza kupanda? Sababu ndio sehemu rahisi ya kupata mabilioni kwa haraka.
 
Gesi ya Mtwara si yetu, huu ni ukweli. Gas ni Mali ya mwekezaji aliyechimba.
Sisi tunanunua kwao kwa Bei ya soko, alafu tunachopata ni Kodi kutoka kwao.
Mwekezaji akirudisha gharama za uwekezaji ndio inakua Mali yetu, swali ambalo hata ccm wenyewe hawana majibu ni je itachukua miaka mingapi mwekezaji kurudisha gharama zake
Sidhani kama uko sahihi. Kwani ukimpangisha mtu nyumba inakuwa ya kwake? Mwekezaji ana haki ya kuitumia gesi kulingana na mkataba wake na mwenye mali. Kikomo cha Mkataba makini ni muda na sio mtu akirudisha gharama zake. Mwekezaji anakubali muda uliokuwepo kwenye mkataba kwa sababu anajua katika muda huo atakuwa amerudisha investment yake, faida au hasara atakayoipata ni juu yake. Kununua gesi ni kitu obvious. Hatuwezi kutegemea kupewa bure. Mbona hivi sasa tunanunua umeme ingawa ni wa kwetu?

Kama CCM hawajui mkataba utakoma lini basi hiyo ni dalili ya mkataba mbovu. Ni kama wewe ukimwambia mtu atengeneze nymba yako halafu akae mpaka arudishe gharama zake. Kama hautasimamia vizuri hizo gharama ili zijulikane kwa uwazi na uhakika hiyo nyumba hutaipata tena.

Amandla...
 
Mkuu huo umeme wa maji ni rahisi umeonea wapi? Au unatumia umeme tofauti na huu tunaotumia sisi wengine? Maana hao wataalamu wanasema umeme wa maji unapaswa kuwa shilingi 36 per unit, ila kwa sasa ni karibu kabisa ya 350+VAT. Swali si umeme wa sasa maana tunatumia na gas humo humo. Je tuliwahi kununua chini ya shilingi 200 kwa unit huko nyuma kabla ya kuanza kutumia umeme wa mafuta mazito, since gas ilianza 2014 na kuendelea.
Issue ni kuwa hatuzalishi umeme wa maji kwa wingi, hivyo bado tunanunua umeme kutoka kwenye makampuni yanayozalisha umeme, ndio maana Bei bado ipo juu.
Hata hili bwawa likiisha bado umeme unaweza usishuke Bei, itategemea na viongozi wetu wataamuaje.
Lakini ni kweli kabisa umeme wa maji ni umeme rahisi.
 
Sidhani kama uko sahihi. Kwani ukimpangisha mtu nyumba inakuwa ya kwake? Mwekezaji ana haki ya kuitumia gesi kulingana na mkataba wake na mwenye mali. Kikomo cha Mkataba makini ni muda na sio mtu akirudisha gharama zake. Mwekezaji anakubali muda uliokuwepo kwenye mkataba kwa sababu anajua katika muda huo atakuwa amerudisha investment yake, faida au hasara atakayoipata ni juu yake. Kununua gesi ni kitu obvious. Hatuwezi kutegemea kupewa bure. Mbona hivi sasa tunanunua umeme ingawa ni wa kwetu?

Kama CCM hawajui mkataba utakoma lini basi hiyo ni dalili ya mkataba mbovu. Ni kama wewe ukimwambia mtu atengeneze nymba yako halafu akae mpaka arudishe gharama zake. Kama hautasimamia vizuri hizo gharama ili zijulikane kwa uwazi na uhakika hiyo nyumba hutaipata tena.

Amandla...
Leo ndio unajua kuwa serikali ya CCM inaingiaga mikataba mibovu?
Mkuu mbona hili linanishangaza Sana?
Unasema sipo sahihi, Sasa unajua ni miaka mingapi itachukua kwa mwekezaji kurudisha gharama yake?
Swali lingine, madini ya kule kahama na geita ni yetu? Lakini si yapo nchini kwetu
Ilivyo kwenye madini ndio ilivyo kwenye gesi, mikataba tuliinga wenyewe na ndio maana hata mwendazake alipotaka kuwabana barrick alikula za uso tu
 
Mkuu huo umeme wa maji ni rahisi umeonea wapi? Au unatumia umeme tofauti na huu tunaotumia sisi wengine? Maana hao wataalamu wanasema umeme wa maji unapaswa kuwa shilingi 36 per unit, ila kwa sasa ni karibu kabisa ya 350+VAT. Swali si umeme wa sasa maana tunatumia na gas humo humo. Je tuliwahi kununua chini ya shilingi 200 kwa unit huko nyuma kabla ya kuanza kutumia umeme wa mafuta mazito, since gas ilianza 2014 na kuendelea.
Over a 50 year period umeme wa maji ni rahisi na nafuu kwa vigezo vyovyote.
Initial costs za ujenzi ni kubwa, lakini ukizigawa kwa mwaka katika period ya miaka 50 hadi 100, gharama inakuwa chini sana.
Kwa ulinganisho, gharama za mitambo ya gesi ambayo unaweza kulinganisha na gari, ndani ya miaka si zaidi ya 10, mitambo mipya lazima iwekwe kutokana na kuchakaa kwa matumizi.
 
Mkuu tusilishwe vitu na tukakariri tu.
North Korea na China leo wamefika mahali ilipo by NOT believing an thing the West has thrown at them.
3 Gorges Dam la China is a good example.

Sisi tukiambiwa Rufiji itakauka, tunaamini mazima mazima.
Mfano mzuri. North Korea mpaka leo wanashindwa kujilisha. China imefanikiwa baada ya kukaribisha wawekezaji kutoka nje.

Three Gorges Dams zilipingwa kwa sababu ya uharibifu wa mazingira ambayo kwao ilikuwa ni baadhi ya miji kuzamishwa.

Lengo kubwa la mradi huu ilikuwa ni ku control mafuriko ya kila mara pamoja na uzalishaji wa nishati. Na baada ya waliyojifunza kwenye mradi huo sasa hivi wachina wanawekeza zaidi kwenye nishati mbadala. Huu mradi wa kwetu lengo lake ni uzalishaji wa umeme tuu kwa kutegemea vyanzo ambavyo haviaminiki.

Amandla....
 
Kwanza nianze kwa kusema mimi si mpenzi mkubwa wa Rais wetu aliyepita, JPM.

Hata hivyo, pamoja na figisu nyingi za JPM katika mambo mbali mbali, mengine ambayo yalikuwa miradi ya upendeleo ulio wazi kimaeneo, katika mradi wa bwawa la umeme Stieglers alikuwa spot on.

Mradi wa ujenzi wa bwawa la kuweza kufua umeme la Nyerere Hydropower(Stieglers Gorge), ni kati ya miradi ya kimkakati yenye matokeo yanayoweza kuleta mapinduzi ya uchumi kwa miaka mingi ijayo.

(NB: Tunasikia kutoka kwa ka nzi, kuwa kuna wakubwa wamejipanga kuingiza figisu kwa makusudi mradi huu)

January Makamba haogopi kuharibu mambo ambayo yanaweza kumuandama maisha yake yote? Maneno na misimamo yake kuhusu mradi wa bwawa la umeme la Nyerere, yanasikitisha sana. Yanatufanya watu wengine tumuogope.
Tukumbuke hii Tanzania ni ya watanzania. Tuweke maslahi ya nchi yetu mbele. Haya mambo yenu ya kisiasa mpambane wenyewe
 
Leo ndio unajua kuwa serikali ya CCM inaingiaga mikataba mibovu?
Mkuu mbona hili linanishangaza Sana?
Unasema sipo sahihi, Sasa unajua ni miaka mingapi itachukua kwa mwekezaji kurudisha gharama yake?
Swali lingine, madini ya kule kahama na geita ni yetu? Lakini si yapo nchini kwetu
Ilivyo kwenye madini ndio ilivyo kwenye gesi, mikataba tuliinga wenyewe na ndio maana hata mwendazake alipotaka kuwabana barrick alikula za uso tu
Madini yote ni yetu. Mwekezaji tumemruhusu kuyauza kulingana na masharti tuliyokubaliana. Ndio maana kwenye takwimu wanasema Tanzania ina dhahabu kiasi fulani lakini Barrick ana migodi kiasi fulani. Barrick hajauziwa dhahabu bali amesema kibali cha kuchimba na kuuza kulingana na makubaliano yetu. Sasa tukiamua kumpa dhahabu yote hatuwezi kumlaumu mtu isipokuwa sisi.

Amandla....
 
Mkuu tusilishwe vitu na tukakariri tu.
North Korea na China leo wamefika mahali ilipo by NOT believing an thing the West has thrown at them.
3 Gorges Dam la China is a good example.

Sisi tukiambiwa Rufiji itakauka, tunaamini mazima mazima.
Rufiji itakauka je wakati siku zote humwaga maji kwenye dam linaloitwa Indian Ocean. Kwani rufiji linapotitirisha maji yake kwenda baharini hua yanarudi kutoka baharini kuja milima ya kilombero tena?
Hii phenomenon ya mto kukauka sababu baadhi ya maji yanatiririka bwawani yanatoka wapi?

Halafu vyanzo vya mito ni milimani kuna chemistry ya Mungu huko miambani chazo ya mito siyo mvua naamini.
 
Over a 50 year period umeme wa maji ni rahisi na nafuu kwa vigezo vyovyote.
Initial costs za ujenzi ni kubwa, lakini ukizigawa kwa mwaka katika period ya miaka 50 hadi 100, gharama inakuwa chini sana.
Kwa ulinganisho, gharama za mitambo ya gesi ambayo unaweza kulinganisha na gari, ndani ya miaka si zaidi ya 10, mitambo mipya lazima iwekwe kutokana na kuchakaa kwa matumizi.
Hapo ndipo unakosea. Unaamini kuwa tutaweza kuzalisha umeme kwa miaka 50 mfululizo bila matatizo. Tujifunze kutoka Kidatu na Mtera. Unaposema gharama za uendeshaji ni ndogo unakuwa hujaweka gharama za kuondoa tope mara kwa mara ambalo kwa mazingira ya mto Rufiji litakuwa linajaa haraka sana.

Haujaweka gharama za uharibifu wa Rufiji Delta na hasara watakayopata watu ambao wanaitegemea kwa uhai wao. Samaki, prawns, mikoka n.k. yote itaathirika. EIA ya mradi ilisema hivyo ndio maana marais kuanzia Mwalimu mpaka Kikwete hawakuutaka huu mradi. Hili ni jiwe tunajifunga shingoni wakati tunaenda kuogelea.

Amandla...
 
Rufiji itakauka je wakati siku zote humwaga maji kwenye dam linaloitwa Indian Ocean. Kwani rufiji linapotitirisha maji yake kwenda baharini hua yanarudi kutoka baharini kuja milima ya kilombero tena?
Hii phenomenon ya mto kukauka sababu baadhi ya maji yanatiririka bwawani yanatoka wapi?

Halafu vyanzo vya mito ni milimani kuna chemistry ya Mungu huko miambani chazo ya mito siyo mvua naamini.
Basi tuweke imani yetu kwa Mungu ambae hataruhusu maji yakauke kama vile anavyofanya Mtera na Kidatu ambako kina cha maji hakipungui hata siku moja.

Amandla...
 
Madini yote ni yetu. Mwekezaji tumemruhusu kuyauza kulingana na masharti tuliyokubaliana. Ndio maana kwenye takwimu wanasema Tanzania ina dhahabu kiasi fulani lakini Barrick ana migodi kiasi fulani. Barrick hajauziwa dhahabu bali amesema kibali cha kuchimba na kuuza kulingana na makubaliano yetu. Sasa tukiamua kumpa dhahabu yote hatuwezi kumlaumu mtu isipokuwa sisi.

Amandla....
Ni kweli, tatizo na gas tulishawapa yote.
Philosophically gas ni yetu iko Tz lakini kiuhalisia tulishaigawa siyo yetu tena. Hivyo mitambo ya gas itakulazimu kununua gas huo ndo uhalisia.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom