Awamu ya 4 ya kikwete ndio ilikuwa sehemu rahisi kubadili katiba, kwa sasa hakuna Rais atayekubali kirahisi

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,000
2,000
Ki ukweli mimi si mwanasheria, na sina taaluma yoyote ya uanasheria zaidi ya kusoma intro ya sheria wakati nasoma masters, ila ili suala la katiba na elimu yangu yote nimekuja kujua umuhimu wa kuwa na katiba imara katika awamu hii ya tano.

Nilikuwaga nasikia watu mbalimbali wakilalamikia katiba, nilikuwa siwaelewi, nilishawahi kusikia hotuba ya nyerere akisema kwa katiba yetu akija mtu wa namna flani anaweza kuitumia vibaya,ila kiukweli kabisa sikumwelewa.
Nimekuja kugundua maraisi wengi waliopita nchini kwetu waliitumia vizuri katiba yetu mbaya iliyopo kiasi cha kutoonekana kama ina mapungufu hasa kwa sisi tusiojua sheria.

Nimekuja kujua jinsi katiba yetu inavyompa madaraka makubwa Raisi wa nchi kiasi kwamba nobody can do anything, tunabaki kuongea tumejificha kwenye keyboard au vijiwe vya stori. Kiufupi anaanza president then the constitution then vinafuata vingine.

Wakati wa awamu ya nne ilikuwa rahisi kubadili katiba hata kikwete alikuwa hana tatizo sana na hilo, wala hakuwahi kuitumia katiba vibaya na tuliona fresh tu.

Ila kwasasa hivi kila MTANZANIA ANAJUA NGUVU Ya kiti cha URAISI, na hata akija Raisi mwingine hata kama ni mimi sitapenda kupunguziwa nguvu ambazo tunaona raisi anazo kwa sasa, nitapiga kelele nikiwa nje ila nikiingia sitakubali kubadili katiba. Nasema hakuna Raisi ambaye atakuja kushinda uraisi akakubali kubadili katiba hata Akiwa mbowe, Lipumba, Majaliwa .

Tuliipoteza nafasi hiyo wakati wa Jakaya, haitatokea tena
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
32,074
2,000
Tutulie tu tutafute maendeleo, hata ukitaka unaipataje.
Katiba inazuia maendeleo au huelewi usemacho? Ni kweli katiba ilikuwa ipatikane enzi za Kikwete ila ile ilikuwa ni kwa njia za amani, lakini sio lazima katiba ipatikane kwa njia ya amani, hilo ulitambue.
 
ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,000
2,000
Katiba inazuia maendeleo au huelewi usemacho? Ni kweli katiba ilikuwa ipatikane enzi za Kikwete ila ile ilikuwa ni kwa njia za amani, lakini sio lazima katiba ipatikane kwa njia ya amani, hilo ulitambue.
Sasa kwanini tupigane kisa katiba, c tutii amri tu
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
3,891
2,000
Kila mmoja kwa imani yake tufanye sala,dua na walozi wafanye yao bwana yule abariki mchakato say maboresho katiba ya Warioba. Ipo hatari Zbar anataraji kuifanya mkoa rasmi lile swali la mgao, usawa huwa halipendi sana!La zbar nipo na mkuu, tubaki ndugu moja wa damu.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
32,074
2,000
Sasa kwanini tupigane kisa katiba, c tutii amri tu
Lengo letu sio kupigana bali ni kupata katiba mpya tena kwa njia ya amani, lakini kama kuipata kwa amani haiwezekani basi itabidi itumike plan B. Ni dhahiri utawala uliopo hauna ridhaa yetu na unaingia madarakani kwa udhaifu wa katiba iliyopo. Hatuko tayari kuburuzwa bali tunahitaji viongozi wenye uhalali wa umma.
 
ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,000
2,000
Lengo letu sio kupigana bali ni kupata katiba mpya tena kwa njia ya amani, lakini kama kuipata kwa amani haiwezekani basi itabidi itumike plan B. Ni dhahiri utawala uliopo hauna ridhaa yetu na unaingia madarakani kwa udhaifu wa katiba iliyopo. Hatuko tayari kuburuzwa bali tunahitaji viongozi wenye uhalali wa umma.
Nawaonea huruma Zanzibar, wamesahaulika na wanamuogopa jiwe hakuna wa kuunguruma, nasikia itafanywa mkoa, cjui ni kweli.
 
alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
2,973
2,000
Hakuna katiba mpya itakuja,lakini kutakuwa na mabadiliko ya katiba hii tunayoitumia,mabadiliko gani hayo? Kipengele kikuu cha mabadiliko hayo ni kuondoa ukomo wa mihula ya urais.rais ataongoza nchi kwa mihula minne au zaidi kama hali ya afya itamruhusu kufanya hivyo.
 
Tehe tehe kama wachina walivyofanya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom