Awamu nne, yupi bora? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Awamu nne, yupi bora?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Oct 24, 2009.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tanzania imeshatawaliwa na marais wanne tofauti, maarufu kwa jina la awamu nne. Akianza J.K. Nyerere, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Che Mkapa na J.K. Mrisho.

  Kwanza, kabla sijaendelea tuangalie muujiza mkubwa kabisa uliojitokeza kati ya awamu ya kwanza na ya nne. Angalia kwa makini majina hayo, J.K yanalingana. Na hii si bahati mbaya, bali iltabiriwa na Kinjeketile mwaka 1903 kabla ya kuanza vita vya maji maji. Lakini nini maana ya kushabihiana huko. Hili ni swali ninalowaachia wasomaji.

  Kwa bahati nzuri mimi nimepata sababu moja wanayoshabihiana, nayo ni kupata umaarufu sana kwa watu wa ndani na nje. Pili kushika madaraka wakiwa vijana. Uchumi je? Sitii pua yangu huu ni uwanja wenu.

  Ali Hassan Mwinyi na Mkapa. Hawa nao wana sifa moja inayoshabihiana, kuwa ni maraisi waliopata urais bila wananchi kuwadhania kuwa wangekuwemo katika jopo la wagombea Urais. Ya mwisho lakini si ndogo, wote huacha mouth touch.

  Lakini yote tisa kumi, yupi ni mbora kuliko wote kama rais wa nchi? Tupe data zako za kina na toa ushadi tosha. Ni hoja makini tu ndizo zitazohesabiwa.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wewe tunajua ni "die hard" wa kumfagilia Kikwete sasa unataka watu waseme nini? Na huyo Kinjekitile yupi unayemsema? Yule aliyewaaminisha watu kwamba eti risasi za Wajerumani zingegeuka kuwa maji na hatimaye Watanganyika waliuawa vibaya? Na ndio huyo Kinjekitile ambaye unadai kuwa alitabiri kuhusu Kikwete? Ama kweli JF imevamiwa!
   
 3. u

  under_age JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2009
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ungeanzia enzi za ukoloni. ningeprefer pale tulipokuwa tumetawaliwa na wakoloni.
   
 4. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Mkapa
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Oct 24, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  bado hayupo!
   
 6. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Haiwezekani! Tanzania ni nchi maarufu sana Afrika. Na umaarufu huo hautokani na jina la nchi kuwa zuri, bali utendaji wa marais wake pamoja na timu yake.

  Hivi sasa ni miaka zaidi ya 40 toka tupate uhuru, Tanzania bado ni kioo na mfano kwa Afrika licha ya umasikini wetu. Kwani umasikini ni bahari ya Afrika nzima.

  Kwahiyo sikubaliani nawe pale unaposema hayupo bado. Basi angalau ungesema ni yupi aliyekuwa afadhali, maana hata katika wajinga kuna kiongozi ambaye anaonekana kuwa mzuri kuliko wengine.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Oct 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sasa kama unakataa majibu basi toa majibu yako! Kwa taarifa yako Tanzania haijulikani sana nje kama unavyofikia mahali pa kuiita "kioo!" Kwa wale wachache wanaoifahamu wanaifahamu kwa mabaya kuliko mazuri! Ukiona mimi mwongo tia timu kwenye nchi yoyote Afrika na kuulizia habari za Tanzania toka kwa watu wa kawaida, upate habari zake! Viongozi wetu wanawadanganya wananchi kwamba eti "Tanzania inasifika," kwa lipi? Tuanze kwenye huduma za jamii: viongozi kama wanaona wanatoa huduma bora, kwa nini wao hawasomeshi watoto wao kwenye shule za kata? Kwa nini hawatibiwi kwenye hospitali za hapa nchini? Kuhamia Dodoma: mawaziri bado wanajikita Dar, hawataki kuhamia kwenye ukame (Dodoma). Uwekaji fedha benki: viongozi hawazithamini hata benki zao, wanakimbilia kuweka fedha nje! Kulingana na maelezo hayo hapo juu, kama viongozi wanapika chakula "kizuri" kwa nini wao wasianze kula? Na huu "ukioo" wa Tanzania unatokana na nini? Sio kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa ambako kunafanywa na watu weupe (kama kuna watu wenye rangi hiyo anyway!) ili waendelee kutunyonyoa vizuri? Ni sawa na mwanamke mwenye sura mbaya, mwanamme ili ampate atamsifia kwa sifa za kila namna halafu akimpata ataanza kumkejeli!
   
 8. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hoja zako ni nzito na za msingi. Lakini huwa najiuliza maswali yafuatayo:

  Mara baada ya Mzee Mandela kuachiwa moja kati ya nchi za mwanzo 5 alizotembelea duniani, Tanzania ni moja wapo. Marais wa Marekani ni vile vile Hawaishi kuweka mguu Tanzania. Waarabu nao huinyemelea sana Tanzania.

  Waafrika nao ni vile vile, Ethiopia, Nigeria, Somali, Kenya, Uganda, Burundi na Ruanda wanakimbilia Tanzania. Hivi tunanini kizuri?
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Oct 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pole sasa kwa kutokusoma alama za nyakati: Mkapa aliyeukaribisha unyonyaji kwa jina la uwekezaji anasifika mno nje pamoja na ufisadi wake wote kupitia EPA, Meremeta, Ndege ya Rais, Deep Green Finance, Richmond, Twin Towers, Rada, Mwananchi Gold, Tangold, etc, etc! Reason behind? Kwa sababu anasuit interest zao! Hakuna mtu anayeheshimika kama mnyonyaji (mwekezaji) nchi hii! Ukitaka kuwa unpopular waseme vibaya wanyonyaji! Kikwete na yeye hajarealize kwamba anaendeleza makosa yaleyale ya Mkapa! Kuhusu Mandela: Jiulize kwa nini wa-South Afrika wengi wamelikamata soko la kuuzia bidhaa zao kusini mwa Afrika! Of course nakumbuka juhudi za TZ za ukombozi wa Afrika, lakini juhudi hizo kwa sasa hazithaminiwi hata kidogo! Niliwahi kuongea na baadhi ya Wa-RSA kuhusu hilo wanakuuliza "so what?" Kumbuka juzi juzi kulikuwa na xenophobia (chuki dhidi ya wageni) ya kutisha na mpaka sasa inaendelea! GW Bush: alikaa siku nne Tanzania! Reason? Jiulize mgodi wa Barick ni wa nani, ukipata jibu utajua kwa nini alikaa muda mrefu na kutuahidi vijisenti kibao! Pia huyu bwana alitaka kufungua military base ukanda wa Afrika Mashariki, japokuwa jambo hili halijawa wazi! Ukiona mtu wa rangi nyeupe (kama kuna watu wa aina hiyo anyway) wanakuita "rising star" kama walivyofanya kwa BWM ujue lipo jambo ndani yake, kwa manufaa yao! Kuhusu economic and refugees toka Rwanda, Ethiopia, Somalia, etc walio wengi wanaifanya Tz kama sehemu ya kupitia tu kwenda majuu! Kwa wale wanaobaki ndio tuseme wanatuona watz wazuri au watz wamelala usingizi? Oh, Tanzanians, pls wake up and put on your underpants!
   
 10. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nabii hapati kukosa heshima, isipokuwa kwa wale wa nyumbani kwake.
   
 11. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 873
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 80
  ulofa!!!!!
   
 12. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mie ninaomba kila mmoja amefanya mazuri 99%
  Hiyo 1% ni ubinadamu kwa maana wao sio malaika.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Oct 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wamefanya nini kwa 99%? Na kwa nini nchi iko kwenye umaskini wa kutupwa, huku baadhi yao wakidai hawajui kwa nini TZ ni maskini?
   
 14. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Chaguaenin wenyewe
  1. Aliyeleta mshikamano na kuua ukabila na kuleta ujamaa
  2. Aliyeuza mbuga za wanyama kwa waarabu na kuruhusu uchumi holela
  3. Aliyeuza machimbo ya madini na ardhi kwa bei chee
  4. Umeme wa IPTL unawaka lini jamani Uuuwwiiiiiiiiiiiiii!! Uuuwwiiii
   
 15. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Pamoja na makosa yote ya mkapa, mimi naona afadhari mkapa, maana hata uchumi ulipanda kidogo
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Oct 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tupende tusipende, nchi hii kuna "wananchi na wenye nchi!" By comparison: "Wananchi" wamejengewa shule za kata, "wenye nchi" wanapeleka watoto wao kwenye academies, international schools, english medium schools, overseas schools and colleges! "Wananchi" wanapiga foleni na kulala chini Muhimbili, Mwananyamala (hospitali ambazo hata hivyo hazina dawa), etc, "wenye nchi" wanatibiwa nje ya nchi! Kinachoumiza roho ni kwamba "mwenye nchi" ndiye anayelipiwa gharama hizo zote na "mwananchi!" Tupende, tusipende, tunajenga nchi mbili ndani ya nchi moja!
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Oct 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wewe upo nchi hii au ulihama? Uchumi wa kwenye makarabrasha ulipokua halafu ijawaje? Ukahamia kwenye Meremeta, Rada, Richmond, Ndege mbovu ya Rais, Mikataba Miovu ya madini, Deep Green Finance, TanGold, Kiwira Coal Mine, Mwananchi Gold, etc, etc! (-5) + (+5) = 0!
   
 18. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Chaguo langu la kwanza ni nyerere kwa sababu zifuatazo:
  1 Elimu yetu ilikuwa bora,
  2 Madawa yalikuwa yanapatikana mahospitalini,
  3 Kulikuwa na mshikamano wa taifa
  4. Aliweza kufuta kutojua kusoma na kuandika
  5 Wakati anapata uongozi palikuwa kuna wasomi wacheche sana alipigania watu wasome angalau wapatikane wasomi wa kuendesha ofisi na mambo mengine
  6 kulikuwa na maendeleo ya viwanda: kusindika vyakuka, nguo nk

  ukiangalia yote hayo kwa kipindi chake cha urais alikumbana na matatizo mengi kuliko mafanikio, fikiria vita vya idd amini vilimaliza pesa kiasi gani?
  pia alitufundisha kujitegemea.

  hebu angalia sasa hivi hivi tulivyogeuziwa vibao kila kitu ni kuomba msaada, angalia raisi wetu wa sasa anavyokata mbuga kuomba misaada, kila sehemu watu wanaomba misaada. hebu fikiria hiyo misaada itatupeleka wapi? wakati anayetoa nae bado anatafuta. angalia china wanavyoendela.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Modest, hapa ulimaanisha nini?
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Zawadi;

  Sidhani kama umekuwa fair kulinganisha zama tofauti bila kuweka vigezo sawia!! Pia naamini kiongozi bora ni yule achukuaye maamuzi na kusimama nayo hata kama yanaweza yasimpe sifa kwani ndio uongozi wenyewe, sticking to the strategy until proven fruitless... so far in Tanzania we have had only one president who could do that, Huyo ni Nyerere, period!!!

  • Mkapa alijaribu lakini alizungukwa na awapendao na hata baada ya kujua alimezea [its not good]
  • Mwinyi --- sina la kusema
  • JK --- sikumbuki lini amesimama upande mmoja wa shilingi, kila siku anaplay safe kama mzani [he is libra anyway]
   
Loading...