Awamu hii ya Utawala na undugunaizesheni katika teuzi

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amemteua Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal - FCT).

Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Zainab Goronya Muruke ambaye amemaliza muda wake.

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.

Wajumbe wa Baraza la Ushindani ni;
  1. Mustafa Siyani
  2. Donald L. Chidowu
  3. Susana Mkapa
  4. Bibi Bitamo Kasuku Phillip
  5. Yose Joseph Mlyambina
  6. Dkt. Theodora Mwenegoha
Uteuzi huu umeanza tarehe 18 Agosti, 2017

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Agosti, 2017

=====

Rais Magufuli afiwa na mjukuu wake, makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassan na rais mstaafu Kikwete wampa pole. Jun 8, 2016
2-D92A8223.JPG

Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwafariji wazazi wa Marehemu Jose Mlyambila na Suzan wakati wa ibada ya mazishi ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlambila huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo
 
Nepotism iliyopo kwenye huu utawala hata Sadam Husein alikuwa na afadhali. Magufuli sasa uwe na aibu. Unavyofanya sio kabisa. Haujengi nchi unajenga familia yako na kanda yako. Badilika
 
Chadema ni serikali? Hivi nyie watu hata akilni zebu mmevunja nazo mkataba? Kwamba mnadaiwa na hamuezi kutumia akili zenu hadi mlipe deni?
e
Chadema inataka kushika dola ikiwa chini ya mtu na mkwewe.
 
e
Chadema inataka kushika dola ikiwa chini ya mtu na mkwewe.
Hahaa hujaona mtoto kapewa ujembe FCC, mpwa ni mhazini mkuu wa serikali, na wengine wengi. Na unajua mpwa akipewa kitengo lazima na shemeji akumbukwe. Hii serikali yenu ya mtu na wapwa/mashemeji zake hamuioni mnaona ya chadema.
 
Back
Top Bottom