Awamu hii tuache kwenda kanisani, msikitini

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,091
1,202
Ndio! Acheni kwenda msikitini au makanisani kusali kwani waumini wengi mmejaa unafiki, majungu na mnaleta utani na swala!! Why? Wengi wanasali kila Ijumaa na Jumapili na hata jumamosi lakini matendo yao yanachefua na hawana dhamira ya kuacha dhambi.

Yanini kwenda msikitini au kanisani wakati baada tu ya sala unaenda kuiba, kuzini, kusengenya na ama kufitini?

Kuna haja gani ya kujimwambafai kanisani au msikitini kwa kutoa sadaka kubwa wakati unajijua utajiri wako sio wa halali? Hivi dhamira haiwasutii?
Ni bure kabisa kujishebedua kanisani au misikitini wakati unajiua unatembea na waume za watu. Ni upumbavu kuimba 'bwana asifiwe' kila kukicha wakati wewe ni tapeli mkubwa.

Kipindi hiki tuache kwenda kanisani na au misikitini kwa vile viongozi wa dini karibu wote wamegwaya kukemea ukandamizaji na kuchagua kuwa vibaraka wa serikali.

Tusiende kanisani na misikitini kuswali kwani baadhi ya viongozi wengi wa dini ni wanafiki wakubwa. Hawana ujasiri wa kuieleza Serikali maovu yake. Baadhi ya masheik, wachungaji ama maaskofu ni 'nunuliwabo'.
Hakika viongozi wa dini wamewaangusha sana Watanzania katika awamu hii ya uongozi kwa kuushabikia utawala wa Sasa na hivyo kuufanya uzidi kujimwambafai.

Viongozi wa dini wafahamu kuwa mtu kusema 'mniombee' kila kukicha haina maana kwamba ni kiongozi mzuri.
Tuache kwenda kanisani na misikitini kama dhamira zetu chafu. Ni kupoteza muda. Bora wanaotambika kwa mababu na au kujiita athiests!!! Kataa unafiki wa viongozi wa dini kwa kususia ibada zao!
 
Daima sisi binadamu in wakosefu na ndo maana ikawekwa toba. Omba msamaha kila siku kwa kuwa sisi ni wakusefu na ni viumbe tunaojifunza kila siku maishani mwetu kutokana na makosa.
Pia, kwa upande wetu sisi waislam ibada kama swala ni jambo la lazima it does not matter kuwa we ni tajiri, masikini, mzinifu au mshirikina..
Mwenyezimungu amekuumba ili umuabudu.
Tunaamini kama ww ni mzinzi, mchawi, mshirikina basi unapokwenda kila siku/kila mda ibadani kwa uwezo wa Allah utapandikizwa roho ya uchamungu hatimaye utaacha mambo yote yasiyompendeza mungu na utakuwa ktk njia nyoofu.

Ila ibada ni muhimu sana.. Binafsi naona bora yule mshikina anayekaa na kumkumbuka mola wake na akafanya ibada kuliko ww usiye mshirikina na hautaki kumjua muumba wako.
 
Back
Top Bottom