Awamu hii Spika wa Bunge ni kama Mlinzi wa Rais au Sekretari wa Rais

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,486
8,704
Kuna mihimili mitatu ingawa mmoja ni mkubwa yes ila haindoi dhana ya Check and Balance. Nashindwa kuelewa kama Bunge kwa sasa linaweza isimamia serikali make miradi ya Serikali na Spika yupo anaibaliki hata kama itakuja kutokea Ufisadi au utata wowote ule.

Kenya huwezi kukuta Spika anaandamana na Uhuru Kenyata ingawa wote ni Chama Kimoja.

Uganda huwezi mkuta Spika wa Bunge la Uganda akiwa na Mseveni ingawa wote ni kutoka Chama Kimoja.

Hata hapo tu Rwanda kwa Mbabe Kagame huwezi kukuta Spika anaandamana na Raisi Kagame lila sehemu.

Kwa sasa alipo Raisi basi Ndugai yupo nyuma yake.

Vipindi vilivyo pita.

Tulikuwaga tunawaona Maspika kwenye Shughuri maalumu pekee kama sherehe za kitaifa.

Sikuwahi kwenye Maisha yangu Kumuona Kikwete kwenye Ziara zake akiandamana either na Samwe Sita au Anna Makinda.

Sikuwahi kumuona Mkapa akiandamana na Msekwa.

Awamu hii kama mtu ni mgeni anaweza zania Ndugai naye ni Mlinzi wa Raisi au ni Secretary wa raisi kumbe ni Spika wa Bunge.
 
Leta Picha Msekwa akiwa na Mkapa kwenye Zinduzi na Kikwete akiwa na Makinda na Sita kwenye zinduzi
Huu ni upuuzi....Ni lipi la maana lililoonekana wakati Msekwa..Sitta..makinda hawaandamani na Raisi???
Asipoandamana na Rais hamshindwi kuleta umbeya huku ya kuwa Spika haelewani na Rais
 
Unataka spika hadi amtukane Rais Ndio useme ni muhimili mwingine?

Tuache kukosoa bila sababu
Natamani sana ungetulia halafu ukaja na kitu kwa faida ya nchi. Unajua maana ya muhimili? Unajua maana ya kiongozi wa Bunge? Huyu anatakiwa kuonekana kwenye Sherehe ya kesho na atoe maneno kuntu na sio kunanga watu fulani.
 
Ndugai ni mtaalam wa mambo ya kiafrika amemteka kiongozi wetu ndio maana kila kitu ni ndugai so, ktk hili japo sio mashindano wala vita ila mshindi ni ndugai
 
Hahaaaa aisee kumbe? Nilikuwa sijui
Ndugai ni mtaalam wa mambo ya kiafrika amemteka kiongozi wetu ndio maana kila kitu ni ndugai so, ktk hili japo sio mashindano wala vita ila mshindi ni ndugai
 
Ukiona hao wengine hawaandamani pamoja jua kuna tatizo mahali. Mbona ikulu au bungeni hawafuatani. Na hiyo ndio maana ya mihimili.
 
Back
Top Bottom