Awamu hii Mawaziri Wengi hasa Vijana wamehamishia Ofisi zao Tweeter. Wanaondolea Stress Huko

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Sijafahamu lakini nadhani kutakuwa na jambo. Kiuhalisia hakuna waziri anayesikika kwa sasa mpaka unaweza jiuliza waziri wa mambo ya ndani ni nani? unaweza jiuliza maswali hayo kwa wizara mbali mbali.
Wale vijana waliokuwa wakijitabanaisha kuwa ni wazalendo na wengine wakitaka kujitengenezea njia ya siku moja kuwa mabwana wakubwa wa nchi hii kwa awamu hii naona wengi ni kama wamelazimika kukalia mikia yao na kuinamisha pembe zao kama wanazo bado. wengine zilishakatwa kabisa.

Ukitaka kumsikia January Makamba nenda tweeter huko utamsoma leo ameamka na msongo gani wa mawazo au ana lipi jipya. Ofisini kiofisi hana ambalo anaweza kuibuka nalo likamfanya asikike. sijui kupanda miti na bustani kumeishia wapi?

Ukija kwa Mwigulu Nchemba hata skafu amepunguza kuvaa kwa sasa. Huyu ni waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa kweli kwa sasa hana majukumu kabisa zaidi ya kutembelea vituo vya polisi kukagua majengo yalivyochakaa na kwenda kuangalia matukio ambayo yalishafanyiwa kazi na wakuu wa wilaya au mikoa. Nadhani hata asipokuwepo hamna shida. naye stress zake utaziona ukienda tweeter. Unaweza mwona alivyo mnyonge akidumisha chama cha mapinduzi huku ngumi akiwa ameishusha chini. Nakumbuka ile salamu yetu ya
"kidumu chama cha mapinduzi"
"kidumu! mtu ananyosha ngumi juu....
sasa imekuwa
"kigumu chama cha mapinduz!
"kigumu!" nenda kamsome tweeter

Jamaa yangu wa karibu sana Kigwangalla.. huyu ana stress.. huamini? nenda kamsome tweeter utamwona anavyowayawaya... kwa tweets zake mbalimbali. nikadokezwa inawezekana alikuwa na mategemeo makubwa sana lakini yamefifishwa . Najiuliza hata kigwangalla naye alitegemea nini jamani? kama ambavyo najiuliza kabisa january makamba naye alikuwa anaamini anaweza siku moja kuja kuwa rais wa nchi hii?

Mawaziri wengi wameishia kutoa stress zao tweeter na facebook huko utaona wanacho post utagundua wapo katika hali gani. kwa sasa habari ya mjini ni bwana makonda. huyu ame cut across wizara zooooooote na yeye amekuwa ni waziri mkuu maana ana uwezo wa kuingia wizara yoyote na akafanya lolote. Akiamua kusema sasa tupange kupanda miti basi waziri mhusika inabidi uunge mkono na akiamua kusema sasa ulinzi shirikishi wewe waziri wa ulinzi unatakiwa uitikie chorus ya wimbo aliotunga yeye na ukarekodiwa home studio. studio ya baba yake. Ole wako usiimbe kiitikio chake. unatolewa kwenye kwaya.
 
sijafaham lakini nadhani kutakuwa na jambo. kuhalisia hakuna waziri anayesikika kwa sasa mpaka unaweza jiuliza waziri wa mambo ya ndani ni nani? unaweza jiuliza maswali hayo kwa wizara mbali mbali.
wale vijana waliokuwa wakijitabanaisha kuwa ni wazalendo na wengine wakitaka kujitengenezea njia ya siku moja kuwa mabwana wakubwa wa nchi hii kwa awamu hii naona wengi ni kama wamelazimika kukalia mikia yao na kuinamisha pembe zao kama wanazo bado. wengine zilishakatwa kabisa.

ukitaka kumsikia january makamba nenda tweeter huko utamsoma leo ameamka na msongo gani wa mawazo au ana lipi jipya. ofisini kiofisi hana ambalo anaweza kuibuka nalo likamfanya asikike. sijui kupanda miti na bustani kumeishia wapi?

ukija kwa mwigulu nchemba... hata skafu amepunguza kuvaa kwa sasa. huyu ni waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa kweli kwa sasa hana majukumu kabisa. zaidi ya kutembelea vituo vya polisi kukagua majengo yalivyochakaa na kwenda kuangalia matukio ambayo yalishafanyiwa kazi na wakuu wa wilaya au mikoa. nadhan hata asipokuwepo hamna shida. naye stress zake utaziona ukienda tweeter. unaweza mwona alivyo mnyonge akidumisha chama cha mapinduzi huku ngumi akiwa ameishusha chini. nakumbuka ile salamu yetu ya
"kidumu chama cha mapinduzi"
"kidumu! mtu ananyosha ngumi juu....
sasa imekuwa
"kigumu chama cha mapinduz!
"kigumu!" nenda kamsome tweeter

jamaa yangu wa karibu sana kigwangalla.. huyu ana stress.. huamini? nenda kamsome tweeter utamwona anavyowayawaya... kwa tweets zake mbalimbali. nikadokezwa inawezekana alikuwa na mategemeo makubwa sana lakini yamefifishwa . najiuliza hata kigwangalla naye alitegemea nini jamani? kama ambavyo najiuliza kabisa january makamba naye alikuwa anaamini anaweza siku moja kuja kuwa rais wa nchi hii?

mawaziri wengi wameishia kutoa stress zao tweeter na facebook huko utaona wanacho post utagundua wapo katika hali gani. kwa sasa habari ya mjini ni bwana makonda. huyu ame cut across wizara zooooooote na yeye amekuwa ni waziri mkuu maana ana uwezo wa kuingia wizara yoyote na akafanya lolote. akiamua kusema sasa tupange kupanda miti basi waziri mhusika inabidi uunge mkono na akiamua kusema sasa ulinzi shirikishi wewe waziri wa ulinzi unatakiwa uitikie chorus ya wimbo aliotunga yeye na ukarekodiwa home studio. studio ya baba yake. ole wako usiimbe kiitikio chake. unatolewa kwenye kwaya.
Labda wamemuelewa bosi wao ni mtu wa aina gani
 
Unajua kuitwa mpumbavu mtu ambaye ulikuwa unajiamini kwamba wewe ndo next... after President and PM lazima ukunje mkia....ingekuwa sio ugali wanaoupigia hesabu wengi wangeshazira hivyo viti walivyopewa wakalie na mkulu.
 
Ukweli mchungu wakina Makamba, Mwigulu na baadhi ya mawaziri hawana hali kabisa za kufanya kazi kama ilivyo enzi za kikwete.

Na wanachoogopa kujiuzulu ni wataonekana wasaliti ni kwa sababu bado wanakihitaji sana Chama cha Mapinduzi.
 
Back
Top Bottom