Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,283
- 33,889
Nimekaa natafakari na kujiuliza kama kwenye awamu hii hakuna uonzo serikalini. Ni kweli kwamba hakuna ufisadi ama ufujaji wa fedha za umma unaofanywa na waliomo serikalini?
Zile mbwembwe za wabunge hasa wa upinzani kama enzi za kina Slaa zimepotelea wapi kwenye uongozi huu wa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh: John Pombe Magufuli?
Yale magazeti yaliyojibebea heshima na sifa kwa kusema mambo ya hovyo yaliyokuwa yanayofanyika serikalini kwenye awamu zilizopita yameishia wapi. Au waandishi wa habari walikokuwa wanaandika habari za ufisadi zama zile wameshastaafu kazi?
Imekuwaje Taasisi zisizo za Kiserikali hazina tena ule uwezo wa kuitisha waandishi wa habari na kusema maovu mbali mbali yanayofanywa na serikali kwa wananchi maskini na wanyonge wa nchi hii kama ilivyokuwa zama za Jakaya?
Zile nyaraka ndeefu za viongozi wa dini hasa wa makanisa kama zile za Enzi Jakaya Kikwete akiwa Rais mbona siku hizi zimekuwa chache mno. Au viongozi wa Kanisa wanaona kila kitu kinakwenda kama kilivyotarajiwa?
Kule kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya Juu ile migomo na maandamano siku hizi siyo muhimu sana kama enzi za Kikwete. Au masomo yamekuwa magumu kiasi kwamba wanaosoma kwenye hivyo vyuo hawana muda wa kuandamana au kugoma kama wenzao waliowatangulia kwenye vyuo hivyo?
Awamu hii kila kitu ni safi??