Avumaye baharini papa

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,670
Kumbe wengine wapo. Wabongo wamekuwa wakiwasakama majaji wa BSS kwa sana. Ni kwa vile kile kipindi kinatazamwana na watu wengi na kiko muda muafaka. Kuna huyu jamaa anajiita SSssssebo Chibuluma. ni mganda huyu. yuko EA radio. anaendesha kipindi cha friday night live. ni mbabe. analeta ubabe wa Idi amini ndani ya bongo. si mara ya kwanza kuwakejeli wasanii wetu wa bongo. jana nilijisikia vibaya alipokuwa akihojiana na mtozi (mtozi ni producer) anaitwa steve white. kwa kweli alimharass vibaya hadi kufikia hatua ya kumfukuza. bahati nzuri au mbaya nilikuwa nasikilizia kupitia redio yangu ndogo. wakija wasanii wa kenya au uganda huwa anaongea nao vizuri sana. vipi kwa wasanii wa bongo? akiachiwa huyu atajenga himaya. tunaomba wadau walio karibu na chombo hiki wamweleze huyu jamaa kuwa hatutaki mambo ya ki idi amini hapa!!
 
Eeh, wadau nimesoma gazetini na kuona jana kuwa kipindi cha FNL kina mtazamo mpya chini ya Salama. Big up EATV
 
Eeh, wadau nimesoma gazetini na kuona jana kuwa kipindi cha FNL kina mtazamo mpya chini ya Salama. Big up EATV

Mkuu fafanua vizuri tukuelewe,mtizamo mpya kivipi? ina maana Ssebo amemwachia Salama icho kipindi?.Naona Salama anaboa tu,jana anangoa mitambdo ya kupokelea SMS anadai "sijui simu ya nani inapiga kelele",baadae ndio anakuja kushtukia SMS haziingi.
 
unajua kila kipya kina utaratibu wake. Salama na dj wake ndo wanaongoza FNL kwa sasa. Hata muonekano wa pale studio umechenji. Bora kuwa harassed na sebo au kuwa na salama ambae unahisi anaboa?
 
Mkuu, Sebo yuko sawa.Tatizo binadamu ukimweleza ukweli anachukia.
Kuhusu kufukuzwa msanii, umejaribu kufuatili kwanini alimfukuza,labda alianza kuongea pumba na matusi,make wasanii wetu pia ni bangi tupu.
Kuhusu salama, mimi nikimwona kwenye TV au redio nazima au nabadilisha channel.
 
Mkuu ni msanii gani huyo alifyefukuzwa ? na alifukuzwa na Sebo au na Salama...Mkuu Salama ni mtangazaji mzuri sana,labda unamatatizo nae binafsi au upendezwi nae tu.
 
Mkuu, Sebo yuko sawa.Tatizo binadamu ukimweleza ukweli anachukia.
Kuhusu kufukuzwa msanii, umejaribu kufuatili kwanini alimfukuza,labda alianza kuongea pumba na matusi,make wasanii wetu pia ni bangi tupu.
Kuhusu salama, mimi nikimwona kwenye TV au redio nazima au nabadilisha channel.

kuhusu sebo nilimsikia akimmwagia maswali ya rashasha huyo producer- steve white. Kila mara dogo alipokuwa anataka kutoa maelezo, sebo alimkatisha na mwisho wa siku kumtimua. Dakika za mwisho za uhai wake FNL, wasanii wengi hasa wachanga walipofika hapo studio walijawa hofu ya kuumbuliwa dhahiri kabisa
 
Ina maana Sebo amefukuzwa kazi kisa kamtimua steve white?

sijasema kama sebo kafukuzwa na wala sidhani ni kwa kesi ya huyo producer peke yake. kuna mlolongo mrefu wa matukio yake ya kiubabaishaji. hata kipindi cha asubuhi cha EA radio namsikia yule dada peke yake.
 
Ssebo ameacha kazi peke yake. Amere-sign wala hajafukuzwa. Mtu kuulizwa maswali ni sawa na kama hajibu vizuri unamwambia. Mbona mnaona vipindi kama hard-talk or Lary King live bomba sana? We wadhani zimeanza vipi?
 
Salama ni msanii, hata hivyo anazisha mbwembwe kidogo. Akipunguza mbwembwe kwa sana hakika anaweza vipindi vya burudani.
 
Back
Top Bottom