Aviation news: Fly 540's low airfares rattle Tanzanian competition | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aviation news: Fly 540's low airfares rattle Tanzanian competition

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BASIASI, Jan 14, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,108
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Kampuni ya ndege ya 540 ifanyayo safari zake DAR NBO soon wiki ijayo itaanza safari zake kwenda DAR MWANZA,,HABARI ZILIZOTUFIKIA ZINASEMA KAMPUNI HIYO IMEPENGA KILA MTANZANIA MWENYE UWEZO MDOGO KUWEZA KUSAFIRI NA NDEGE HIYO KWA BEI YA CHINI KABISA HUKU IKITUMIA NDEGE ZAKE
  F28 ZENYE KASI NZURI

  TUNAWATAKIA KILA LA KHERI WADAU WA ANGA
  TURUDISHIEN NA COMMUNITY JAMANI 80,000 UNAFIKA MWANZA,SIJUI WALIKUWA WANATUMIA MKOJO KWENYE MAFUTA AMA LAH..MWENYE SIRI YA COMMUNITY AIR ATUJULISHE JAMANI..TUNAWEZAMCHANGIA
   
 2. T

  Tofty JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama habari hii ni ya ukweli basi itakuwa imewakomboa wananchi....it's about time to end Precision Air's monopoly!!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  540 hawana F28, nijuacho ni kwmb wana
  -Dash-8,
  -Beechcraft-19, na
  -Caravan C208.
  Fokker 28 ni kama ile ndege ya jet ya TGFL, yenye registration 5H-CCM. Kama wanayo, basi ni bahati. nadhan tuko pamoja.
  Hata hivyo nawatakia 540 kila la heri. Ni hatua ya ushindani, na mwenye nafuu atakuwa mlaji.
   
 4. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama una tetesi ya bei zao pia tupashe!
  Community Air Line hadi Mza ilikua about 12O,000/- kama sijasahau.
  Wakati nlipo kua huko Tz nili-Flight nayo mara kadhaa.
   
 5. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,108
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  mkuu iko pale chini airport una mtu akusaidie kuhakiki
  ni ktk zile ndege 2 walizonunua east african comp
  wanaanza tar 19 mwezi huu na leio wafenya innagural flt asbh
  angalia taarifa ya habari kaama uko uhindini dar
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kampuni ya safari za ndege ya Precision leo imezindua nauli maalumu kwa wasafiri wa ndege wa kampuni hiyo kwenda na kutoka Visiwani Zanzibar.

  Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Biashara - Phil Mwakitawa alisema; "Kwa muda wa miezi mitano ijayo abiria wetu kwenda na kutoka Zanzibar watalipa kiasi cha Shilingi za Tanzania 35,000 kwa safari moja na Shilingi za Kitanzania 60,000 kwa safari ya kwenda na kurudi."

  Pamoja na hayo, kampuni ya ndege ya Precision Air ilianzisha safari za ndege za mapema alfajiri mnamo mwezi Novemba mwaka jana ili kutoa nafuu hasa kwa wafanyabiashara kwa kuondoa usumbufu kwa abiria wake wanaosafiri katika njia hiyo.


  Safari ya ndege ya mapema alfajiri kwenda Zanzibar inaondoka Jijini Dar es Salaam saa saba na nusu usiku wakati safari ile ya kutoka Zanzibar kwenda Jijini Dar es Salaam inaondoka Zanzibar saa nane na nusu usiku.


  Kuongezwa kwa safari hiyo ya mapema alfajiri inafanya safari za ndege kwenda Zanzibar kufikia nne na zile za kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam kufikia saba.


  "Kwa kuanzishwa kwa safari hii ya mapema alfajiri, kwa sasa ni rahisi kwa abiria kwenda Zanzibar kwa ndege mapema kabla ya shughuli za kibiashara hazijaanza, kuhudhuria miadi pamoja na wale wanaotaka kuwasili Jijini Dar es Salaam mapema", alisema Mwakitawa.


  Kampuni ya ndege ya Precision imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kutumia vifaa vyake vipya na vya kisasa katika soko la biashara ya ndege.


  Mnamo mwaka 2006 Kampuni ya Ndege ya Precision na kampuni ya kutengeneza ndege ya ATR walisaini mkataba wa Dola milioni 129 kwa ajili ya ununuzi wa ndege saba mpya katika mpango wake wa kuboresha ndege zake. Ndege ya mwisho kutoka ATR iliwasili Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana.


  Mkataba huu wa kibiashara wa ndege hizi saba (2 ATR 42-500 na 5 ATR 72-500) uliiwezesha Precision Air kutunukiwa kwa zawadi mbili za kimataifa.


  Mwezi Aprili 2009, Jarida la Air Finance liliuzawadia mkataba huu kuwa Mkataba wa kibiashara bora zaidi kwa Afrika katika mwaka 2008. Mkopo wa ndege za ATR ulikuwa umeishazawadiwa Desemba mwaka juzi na Gazeti la Usafirishaji Jane's Finance, kama "Mkopo mkubwa wa mwaka Afrika wa ndege 2008."


  Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho mwezi Septemba imefanya kampuni hii ya ndege kuwa na jumla ya ndege kumi, saba kati ya hizo ni mpya kabisa. Kampuni ya Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.


  Kampuni hii ya ndege ina mtandao mkubwa wa safari za anga ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara.


  Kampuni ya Precisionair pia hufanya safari zake za anga katika miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya na Entebbe nchini Uganda.
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwa wale wanaopenda safari kazi kwenu
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kwanza izindue air hostess wenye adabu
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  hili ni muhimu zaidi, hata wafanyakazi wake ni matapeli, wanauza tikiti kwa magendo. Ni hovyo hovyo hovyo......................
   
 10. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  thats tz
   
 11. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Sijui ATCL imebaki na ndege ngapi jamani?
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi bado lipo?
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  By Wolfgang H. Thome, eTN | Feb 10, 2011

  (eTN) - The recent introduction of flights between Dar es Salaam, Tanzania's Indian Ocean port city, and Mwanza, the Tanzanian Lake Victoria municipality, has hit the market with a ban, as the fares charged by Fly540 are reportedly as much as 50 percent lower than the ones demanded by its competition.

  While Precision Air, which incidentally is preparing for an IPO on the Tanzanian financial market, is downplaying the competitive threat, Air Tanzania, struggling as it is against its financial expiry, seems more concerned about the latest entrant on the domestic market in Tanzania. Left with reportedly only one operational aircraft, the erstwhile national airline has seen its fortunes plummet, its markets taken over by Precision – and now Fly 540 overtaking it, too, and been subject to a range of allegations over financial dealings, exposed by WikiLeaks documents in recent weeks.

  Considering the cut-throat competition on the Kenyan domestic market, where of late Kenya Airways has gone on a major marketing offensive for their routes between Nairobi to Mombasa and to Kisumu, which has already led to the takeover of EASAX by Fly540, it will be interesting to see how competition will play out on the Tanzanian market
   
 14. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hao 504 nimekuwa nikiona advert zao sana lakini hawana ratiba za safari niliwahi kwenda ofisi zao mtaa wa samora jirani na Stears and Debonnairs sikuelezwa lolote la maana labda wajipange wafanye marketing watu wajue ratiba zao sio iwe biashara ya kubahatisha!
   
 15. Loner

  Loner JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Its about time PRECISION, has some challenges in the field. Off late they have been forgetting them selves since they know that there is no other alternative in flying around Tanzania. So there service just sucked and when they feel like the just cancel the flight..

   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  bora 540 .....kuliko PRECISION ...ambayo ilitumia hila zote kuhakikisha AIR TANZANIA inakufa....! I pray AIR TANZANIA TO COME BACK WITH 540 PATNERSHIP
   
 17. F

  Future Bishop Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wandugu heshima mbele, Naomba kwa anayejua ratiba na nauli za hawa 540 anisaidie.

  Nataka kujua return ticket ya Arusha/KIA to Dar Es Salaam ni shilingi ngapi na ni siku zipi wanasafiri, pia return ticket ya KIA to Mwanza kama route hii wanayo ni shilingi ngapi na ni siku zipi. Precision Air naona bei zao ni kubwa sana lazima uwe na zaidi ya laki tatu kwa trip moja.

  Natanguliza shukrani.
   
 18. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Siwafahamu hawa 540, lakini hiyo nauli wanayotoza kwenda MZA na kurudi DSM, sijui kama inaendana na huduma, usalama, n.k. Bure gharama jamani!!! Sikubaliani na Mahesabu kuhusu PRECISSIONAIR kuiua ATC, kusema la ukweli ni ufisadi ndo umeiua ATC (a.k.a Any Time Cancellation)!!!
   
 19. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Fly 540 are charging Tzs 199,000 for Dar - Mza - Dar ticket.
  As they were loosing customers Precision Air are now doing Tzs 149,000 on the same route. Wakati Unguja sasa wanalipa Tzs 60,000.
  That is to say Precision have been making super profits by charging Tzs 340,000 for Dar Mza Dar ticket.

  Kama kuna wadau kwenye aviation industry wajaribu ku-shade some light on how much can ATR - 50 passg seater make kwa trip ya Dar Mza Dar.
   
 20. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #20
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  YOU mean precision charges 149,000 on return ticket? that would be wonderful news.
   
Loading...