Avg antivirus 2011 – ni kimbilio lakini …

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,207
0
Mimi ni mpenzi wa kujaribu Programu za masuala ya Ulinzi na Usalama kama Antivirus , Internet Security , Firewall , Antispyware na nyingine nyingi tu kwa siku za karibuni nimekuwa mjaribuji wa AVG INTERNET SECURITY 2011 , Hili ni toleo jipya la AVG Antivirus 9 Ambayo kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita imekuwa inafanya vizuri zaidi kidogo na nilifikiri ingeweza kuleta upinzani mkubwa kwa Bidhaa kama Norton Internet Security na Kaspersky Internet Security 2011.

Toleo la sasa limeongezewa vitu kidogo na imekuwa taratibu sana katika kuinstall programu hiyo yote kwa ujumla pamoja na kuscan kuliko matoleo mengine yaliyopita ukitaka kujua hili ni vizuri uwe na komputa nzuri ambayo haina matatizo yoyote , iliyounganishwa kwenye mtandao na kuwa na uwezo mkubwa .

Wakati unainstall utaona kwamba inaruhusu moja kwa moja baadhi ya programu kufanya kazi moja kwa moja katika programu zako za kuangalia internet , zile za kusoma barua pepe kama OutLook na nyingine nyingi Programu zinazoweza kufanya kazi kwenye upande huu ni kama Microsoft Security Essentials, PC tools antivirus 2011 na Comodo


MABADILIKO MUHIMU

PC ANALYZER
Kwenye toleo hili utaona kuna vitu vipya na vingine ambavyo vimeboreshwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma moja ya bidhaa mpya kwenye toleo la 2011 ni PC ANALYZER hii ni programu ndogo kwa ajili ya kuangalia komputa yako kama ina matatizo kwenye registry na kukuambia wewe kwa ajili ya kurekebisha kutumia programu hiyo – haka kaprogramu kanauzwa tofauti ingawa kimeunganishwa na AVG 2011

LINK SCANNER
Hii ni programu iliyokuwa ndani ya AVG 2010 kwa ajili ya kuangalia Linki ( viunganishi ) vya kurasa zote na Tovuti za mtandao unazotembelea pamoja na majibu unayopata kwa njia ya seach engine na kukuambia kama salama au si salama usipofanya updates kwa wakati Link Scanner inaweza usikupe majibu ya uhakika kwa baadhi ya tovuti na kurasa kutokana lakini pia inainstall programu moja ya hali ya hewa toka kampuni ya yahoo pamoja na kubadilisha Home Page yako kwenda yahoo pia lakini yote hii unaweza kubadilisha au unaweza kusitisha kuinstall hizi toolbars wakati wa kuinstall mara ya kwanza .

Hayo ndio mambo unayoweza kuyapata kwenye AVG 2011 Unaweza kujaribu ili uweze kununa Full Version yake , unashauriwa kudownload bidhaa hizi kwenye tovuti za bidhaa husika mfano avg ni www.avg.com unaweza kutumia tovuti zingine lakini angalia linki ya download kama imeelekezwa kwenye tovuti ya bidhaa husika au kama kuna makubaliano yoyote kati ya watengenezaji wa bidhaa hizo .

Yona f maro
www.ictpub.blogspot.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom