Auwawa baada ya kuzaniwa "digi digi"

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
MKAZI wa Kijiji cha Bahaba wilayani Kondoa mkoani Dodoma, Degera Tamba (23), amefariki dunia baada ya kuchomwa mshale tumboni na watu wasiojulikana baada ya kumuhisi kuwa ni digidigi.

Hayo yalielezwa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

Kamanda Stephen alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 3 usiku kijijini hapo baada ya Tamba kuchomwa mshale tumboni na watu wasiofahamika wakati akitoka kilabuni.

Alifafanua kuwa mtu huyo alichomwa na mshale huo tumboni baada ya watu hao wasiofahamika wakiwa wanawinda kumfananisha mtu huyo ni digidigi.

Alisema Polisi mkoani hapa inaendelea kuwasaka watu hao ambao wamehusika na tukio hilo.

Katika tukio jingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Moses Maghati (48), amekufa baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kamanda Stephen alisema tukio hilo lilitokea juzi saa moja na nusu asubuhi katika Kijiji cha Makulu katika Manispaa ya Dodoma baada ya gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T552 AFE lililokuwa likiendeshwa na dereva Joel Koliya (27) kumgonga Maghati wakati akiwa anaendesha baiskeli.

Alisema dereva huyo alishindwa kumudu mwendo ndipo akajitahidi kumkwepa ndipo alimgonga mtu huyo na kumsababishia kifo. Mtuhumiwa Koliya anashilikiwa na polisi na uchunguzi unaendelea.
 
sasa huyu mwenzetu alikuwa ananuka kama digidigi au alikuwa anakaa shimoni?
 
Back
Top Bottom