Auwa mumewe baada ya kumfumania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auwa mumewe baada ya kumfumania

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gudboy, Dec 24, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  MWANAMKE Mwanaidi Majid anasakwa na jeshi la polisi kwa kitendo chake cha kumuua mume wake kwa kumchoma na kisu baada ya kumfumania.

  Mwanaume huyo aliyeuawa alifahamika kwa jina la Jophrey ama kwa jina maarufu 'Chochorii Chochoraa' aliuawa baada ya mzazi mwenzake kumchoma na kisu kwa kile kilichodaiwa kuwa alimfumania akiwa na mwanamke mwingine.

  Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana kwenye majira ya saa 4 asubuhi, huko katika Mtaa wa Mukendo wilayani Musoma mkoani Mara.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Liberatus Barow, amesema kuwa marehemu huyo ambaye ni mcheza ‘shoo’ maarufu mjini humo aliuawa na mzazi mwenzake huyo baada ya kumkuta akiwa na msichana mwingine kwenye bahati nasibu.

  Amesema mtuhumiwa Mwanaid, alipomkuta mzazi mwenzake huyo akiwa na msichana huyo ndipo alipomvaa mwanamume huyo na kuanza kupigana naye ambapo baada ya muda mfupi alichomoa kisu kisha kumchoma nacho tumboni.

  Kamanda Barow amesema, jeshi lake linaendelea kumsaka mwanamke huyo ambaye alitoweka baada ya tukio.

  source: nifahamishe.com
  Na Mwandishi Wetu. Musoma
   
 2. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Poetic Justice,i mean Fair dealt
   
 3. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  I mean huo ni mtazamo wangu tu!
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  "Mzazi mwenzake" kwa maana ya kwamba walikuwa hata hawajaoana? Hivi kuachana na mtu kuna ugumu gani mpaka umuue ?
   
 5. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naomba nikuulize kwa mfano,tafadhali........

  Mimi nina mguu mmoja,hivyo napata shida sana kwenye kutembea,kwa kunionea huruma au mapenzi,wewe unaniazima mimi mguu wako mmoja (just imagine) alafu wewe unabaki na mmoja na hivyo wewe huwezi kutoka unanisubiri mimi nikurusidhie mguu wako.
  Katika subira yako mimi nirudi anakuja mtu anakuambia mimi huko niliko nafanya kazi ya kuwabeba watu mtoni kwa kuwavusha na kupata hela na naweza yote hayo kwa sababu nina miguu miwili(mmoja wa kwako)

  Sasa,wewe utaamua nini kwenye hilo???
   
Loading...