MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,218
Hivi benki za hapa nchi kwetu zinanunua ATM mtumba au vipi? kwa sababu wanatuibia sisi wananchi kwa kutoweka pesa kwenye mashine husika ndani ya muda mwafaka pindi zinapoisha au kupungua kana kwamba hawajui kuwa mashine yao ya eneo fulani iko kwenye hali gani. Pia masuala ya ubovu wa ATM yanachukua muda mrefu kushughulikiwa mpaka kero na sual la mtandao (network) kusumbua au kutopatikana pindi unapotaka kupata huduma ya ATM . Utakuta unaweka kadi inasoma na kufanya zile hatua husika za kutoa pesa yako ila mwisho unaishia kukuta kuwa pesa hakuna, jamaa hawa CRDB,BACLAYS, NMB, na wengineo wenye tabia hizi mjirekibishe kwani mnaboa sana , wakati sisi wateja ndo dhamana ya uhai na kushamiri/ kustawai kwa biashara yenu.