Autism inatibika?

BUSARA6

JF-Expert Member
Jan 8, 2007
357
50
Naomba kujua kama haya maradhi ya autism yanatibika? na kama yanatibika naomba kama kuna yeyote aijuaye dawa anifahamishe hata hizi dawa za asili pls.
 
Uchunguzi na utafikti mwingi uliofanywa unasema kuwa hiyo hali haitibiki. Autism siyo ugonjwa bali ni hali, hali ambayo inamfanya mwathirika awe na hiyo tabia unayoiona.
Kuna vyakula ambavyo vinasaidia watu au watoto wenye hiyo hali wapunguze huo utundu wao au waongeze utundu na kutokusikia kwao. Vyakula vinavyoizidisha hiyo hali ni kama maandazi, mikate, vitu vyenye wanga na pia sukari nyingi, mfano chocolate, visheti visheti na pipi pipi. Pia vyakula kama viazi, chips, pia vitu kama tambi, crisp nk siyo vizuri hivyo kama kuna uwezekano inabidi huyo mtoto asilishwa kabisa, au hata akilishwa ale kidogo tu.

Kitu kingine ni kelele kelele au kumfokea (hasa kwa nguvu) huyo mwathirika hii huwa inazidisha matatizo badala ya kupunguza. Pia kuongea haraka haraka kunawazuzua hao waathirika, hivyo njia nzuri ni kuongea polepole na pia kutosema maneno mengi. Mfano badala ya kusema "...we fulani nenda kalale sasa hivi kwani ni usiku...." Unatakiwa usema kwa upole hivi;"...Fulani kalale sasa..", na ikibidi urudie hivyo hivyo huku ukimwashiria kwa vitendo pia.

Hali hii huwa inasababisha mtu awe mgumu kwenye Lugha, kuchanganyika na watu, kuelewa au kusoma mtu/au vitendo, na sababu kubwa ni kuwa kuna sehemu ya ubongo wa mwathirika ambayo haijengeki vizuri kama watu wengine.

Kwa maelezo zaidi unaweza kunitumia PM
 
choveki,
Ahsante sana kwa maelezo yako na ufafanuzi wa kina.
 
Hamna tabu ndugu Lamba,
Ndivyo tunavyosaidiana kindugu hapa JamboForums. Na kama nilivyosema usisite kuuliza.
 
Nina watoto wawili wa kiume wenye hali hii.Mkubwa ana miaka 6 na mdogo ana miaka 4.Ingawa wote wana autism, huyu mdogo hali yake iko savere kiasi cha kwamba hata neno moja halitoki mdomoni.Na madoctor wameshatueleza ya kwamba to get used na hali ya mtoto wetu.Vyakula apendavyo ni chips,crips,mikate,choclate na biscut.Usipompa hivyo,atakaa kutwa nzima bila ya kula.
Nilijaribu kuwapeleka kwa wachina ili wakafanyiwe accupancure.Nilianza na huyu mtoto mkubwa na kwa kiasi fulani ilimsaidia na kuanza kutamka baadhi ya maneno ingawa hachanganyi sentence.Lakini huyu mdogo hajamsaidia hata kidogo.
Jambo la kushanganza hali hii huanza kujitokeza baada ya kufikia miaka miwili ndipo ninapojiuliza haya matatizo ni ya urithi au hizi vaccine wanazowadunga? Kwa sababu nimeshasikia mengi kuhusu mmr vaccine.
 
Ngugu Lamba,
Wengi wanasema siyo ya kurithi, ila inatokea tu, zipo familia zenye watoto watatu ambao wote wana autism, chanzo au sababu bado ni tata. Wengine wanasema inahusiana sana na chanjo nyingi za watoto, wengine wanasema hapana ila inatokea tu. Hapo bado wataalam napo hawajapata jibu kamili. Wengine wanasema ni hali fulani ambayo inaongezewa na chanjo za utotoni, hususan kuanzia miezi kumi na nane hadi miaka mitatu.

Mimi pia sijui chanzo ni nini ila nimefuatilia uchanguzi wa pande zote mbili, inaelekea kama pande zote zina sababu ambazo zinaonesha kama za msingi, na kwa sabanu hizo mimi binafsi nipo katikati 50/50 pande zote mbili. Ila nahisi chanjo inawezekana kabisa kuchangia kuleta hiyo hali, kwani wataalam wengine wanasema, ingawa siyo hali ya kurithi wapo watoto wengine ambao wakichomwa hizo chanjo tatu za pamoja basi zinaamsha hiyo hali, na kama wangechomwa chanjo hizo tatu moja moja hiyo hali isingeamshwa (mfano labda hata wewe ungechomwa zote kwa mpigo labda ungepata autism).

Mimi nitacho kushauri ni kuwa kama Mwenyeezi Mungu akikujalia ukapata mtoto/watoto wengine basi hakikisha hizo chanjo wanazopatiwa ni zile za moja moja (ingawa zinagharimu) na siyo hizo tatu kwa mpigo (au MMR kwa jina la kitaalam). Kwani inawezekana kabisa ikawa ni kitu cha kurithi toka kwa wazazi wote wawili kinachosababisha kuwa ikichanganyika na hizo MMR inaleta hiyo hali ya autism.

mtoto wako mkubwa kutoweza kuchanganya maneno ndivyo ilivyo kwa hao wenye autism, na ndiyo maana mwanzoni nikwambia unapoongea nae/nao jaribu kupunguza maneno uyasemayo ili aelewe na pia utumie zaidi vitendo na vielelezo. Unapoongea sentensi ndefu, au maneno mengi basi wanakuwa hawaelewi kabisa (wanasikia kama mayowe au mzozo mzozo bila mpangilio wowote, na baada ya hapo wanapandwa na hasira na kuanza labda kuvunja au kutupa vitu au hata kugalagal chini-wataalam wanasema sauti waisikiayo ni kama ile ya mkwaruzo wa sufuria na kijiko/chuma etc. ambayo huwa inaumiza meno au masikio kwetu sisi).

Pia vyakula ulivyovitaja nadhani vyote vinamwongezea hiyo hali huyo wa pili, (nadhani ndo maana haongei). Ina maana kama ukipunguza sana, au ukiweza kumwachisha kabisa vitu kama crisps, chocolate nk basi tofauti yake utaiona katika siku moja. Tatizo ambalo lipo ni kuwa ina maana kumbadilishia siyo rahisi kwani hiyo hali inasababisha wawe na obsession na hivyo vyakula. Unachotakiwa kufanya ni kununua spesho ambavyo nadhani kuna baadhi ya maduka wanauza,ambavyo havina hivyo vitu vinavyoongezea hiyo hali nitajaribu kutafuta jina la kitaalam ili nikupatie.

Naona niishie hapa, ila narudia usisite kuuliza kama kuna ambacho hujakielewa.
 
Nitajaribu kuwapunguzia hivyo vyakula vya wanga pamoja na chips ili nione matokeo yake.
lakini kwa nini matatizo haya yapo sana huku nchi za magharibi kushinda kule bongo? Sijapatapo kuona wala kusikia mtoto ana autism kule bongo.
Kuna kama familia tatu za wa tz nao pia wanalalamika kuhusu hii hali kwa watoto wao.Ndio maana wasiwasi wangu mkubwa uko kwenye hizi chanjo!!
 
Choveki nashukuru sana kwa maelezo yako-hata mimi kwakweli nina fikiri hizi chanjo zinasababisha sana Autism ila hawawezi kusema,namimi na swali ,apart from kuchelewa kuongea ,je ni test gani itanijulisha kama mtoto ana autism?nitashukuru nikipata maelezo zaidi ya autism-inamaana mtoto akiwa na autism ,haaweza kusoma kabisa katika maisha yake?hivi kuna vitamins zinaitwa OMEGA 3-OR FISH OIL je hizo haziwezi kuwa msaada mkubwa kwa watoto hao?
 
Karibu Ndugu Ledwin na wengineo
Nitajaribu kueleza kadri ninavyofahamu. Ni hivi test ya kuangalia au kupima mtoto ana autism siyo ngumu sana na pia siyo rahisi sana, inategemea unavyomfahamu mtoto wako na jinsi anavyochanganyika na wenzake na kucheza nao, pia ana ubinfsi kiasi gani na anavyoongea au asivyoongea. Mara nyingi hizo test hufanywa kuanzia miezi kwenye 18 hadi miaka mitatu, inategemea na anavyokuwa na vitu hulka anayoonesha. Mara nyingine inatokea kuwa watoto wengine wanachelewa kuongea au kutopenda kucheza wenzao na pia wabinafsi sana, ila pia haimaanishi kuwa wana autism, ila hizo ndiyo dalili za mwanzo. Mara nyingi daktari akihisi hivyo atakuuliza maswali kidogo halafu mtapelekwa kwa mtaalam ambaye atamfanyia mtoto hito test. Test yenyewe siyo kumpima kwa vipimo bali ni kama maswali na majibu utakayoyatoa yataonesha kama ana autism au hana. watoto wengine huhitaji test zaidi ya moja na wengine moja hutosha.Na ndiyo maana test nyingi zinakamilia wanapotimiza miaka mitatu, na wengine dalili kamili zinaonekana wakiwa na miaka karibu minne.

Tatizo kubwa la hi hali ni kuwa hakuna watoto au watu wawili wanaoweza kuwa na hali sawa kabisa, autism inatofautiana baina ya mtoto na mtoto. Pia wakati mwingine inaweza ikawa kinyume na kuwa mzito ki akili, hawa mara nyingi huitwa wana Aspergers. yaani, aspergers ni aina ya autism ambayo mwathirika akili zinachemka kupita kiasi kwenye kitu kimoja tu au viwili, tetesi ni kuwa Bill Gates wa microsft ni mwathirika. Kama ushasoma na mtu akili zikawa zinachemka labda za hesabu, chemistry au Jiografia nk kupita kiasi lakini akawa hawezi kuelewesha mtu na pia akawa hawezi kuongea vizuri au kuwa na rafiki, pia mkawa mnamuona sijui yukoje yukoje mara nyingi huyo anakuwa na autism ya aspergers-Tanzania watu hutumia maneno kama haya "...jamaa yule zinachemka sana lakini kidogo chizi chizi..." nk.

Omega 3 au fish oil inasaidia saana, ingawa inatofautiana baina ya mwathirika na mwathirika. Yaani faida yake inatofautiana baina ya mtoto na mtoto. Kitu kingine kwenye hizi Fish oil ni kwamba, utafiti wa karibuni umeonesha kuwa zinasaidia saana watoto wote, mimi nashauri mtu yeyote mwenye watoto wadogo ahakikishe anawapatia fish oil kila siku, kama anavyowapa chakula, kwani faida yake ni kubwa mno.

Watoto wenye autism wanatofautiana kwa umri wakati ambao wanaweza kuanza au kujaribu kuongea. Wengine wanaweza kuanza kuongea kidogo wakiwa na miaka kama minne na wengine hadi wanapofiksha hata kumi, yaani hakuna formula kamili. Mimi nashauri tu kukwepa vyakula vinavyo waongezea hiyo hali kwani hali hiyo inapopungua na uwezekano wa kuongea mapema unakuwa mkubwa zaidi. Wengine huwa wanaaweza kuandika mapema na wengine wanaweza wasiweze kuandika kabisa, yote inategemea hiyo autism ilivyowaathiri.
Naona niishie hapo, msisite kuuliza.
 
Dalili nyengine ya mtoto kuwa na autism ni hii ya kurejea rejea maneno.
 
Choveki
Ahsante sana kwa hii information. Hata mimi nina rafiki yangu ana watoto wawili mmoja 7yrs mwingine 2yrs ila wote wana tatizo la kuweza kuongea. Nafikiri hii itaweza kuwapa msaada wa kutatua hili tatizo.
Je ni katika umri gani mtoto anastahili kuanza/kujifunza kuongea (Ideal Age?).
 
Nashukuru sana kwa discussion hii. I have doctors that I know well and htey recommended a few websites.
Causes of autism na chanjo are unscientifically unproven, just unfounded claims. Here is the official explaination:

"Scientists aren’t certain what causes autism, but it’s likely that both genetics and environment play a role. Researchers have identified a number of genes associated with the disorder. Studies of people with autism have found irregularities in several regions of the brain. Other studies suggest that people with autism have abnormal levels of serotonin or other neurotransmitters in the brain. These abnormalities suggest that autism could result from the disruption of normal brain development early in fetal development caused by defects in genes that control brain growth and that regulate how neurons communicate with each other. While these findings are intriguing, they are preliminary and require further study. The theory that parental practices are responsible for autism has now been disproved.
Recent studies strongly suggest that some people have a genetic predisposition to autism. In families with one autistic child, the risk of having a second child with the disorder is approximately 5 percent, or one in 20. This is greater than the risk for the general population. Researchers are looking for clues about which genes contribute to this increased susceptibility. In some cases, parents and other relatives of an autistic child show mild impairments in social and communicative skills or engage in repetitive behaviors. Evidence also suggests that some emotional disorders, such as manic depression, occur more frequently than average in the families of people with autism.
There is no cure for autism. Therapies and behavioral interventions are designed to remedy specific symptoms and can bring about substantial improvement. The ideal treatment plan coordinates therapies and interventions that target the core symptoms of autism: impaired social interaction, problems with verbal and nonverbal communication, and obsessive or repetitive routines and interests. Most professionals agree that the earlier the intervention, the better.

Educational/behavioral interventions: Therapists use highly structured and intensive skill-oriented training sessions to help children develop social and language skills. Family counseling for the parents and siblings of children with autism often helps families cope with the particular challenges of living with an autistic child.
Medications: Doctors often prescribe an antidepressant medication to handle symptoms of anxiety, depression, or obsessive-compulsive disorder. Anti-psychotic medications are used to treat severe behavioral problems. Seizures can be treated with one or more of the anticonvulsant drugs. Stimulant drugs, such as those used for children with attention deficit disorder (ADD), are sometimes used effectively to help decrease impulsivity and hyperactivity.
Other therapies: There are a number of controversial therapies or interventions available for autistic children, but few, if any, are supported by scientific studies. Parents should use caution before adopting any of these treatments."

I hope this helps.

Also ni vyema kujua kama mwenzetu uko Tanzania au nje ya nchi, maana hapa nchini ni ngumu sana kupata hizi medication. Lakini if you need more help I can PM you later, if you are in Bongo.
Actually some children improve with time:
"For many children, autism symptoms improve with treatment and with age. Some children with autism grow up to lead normal or near-normal lives. Children whose language skills regress early in life, usually before the age of 3, appear to be at risk of developing epilepsy or seizure-like brain activity. During adolescence, some children with autism may become depressed or experience behavioral problems. Parents of these children should be ready to adjust treatment for their child as needed"

God Bless!
 
Choveki
Ahsante sana kwa hii information. Hata mimi nina rafiki yangu ana watoto wawili mmoja 7yrs mwingine 2yrs ila wote wana tatizo la kuweza kuongea. Nafikiri hii itaweza kuwapa msaada wa kutatua hili tatizo.
Je ni katika umri gani mtoto anastahili kuanza/kujifunza kuongea (Ideal Age?).

Watoto huwa wanatofatiana. Kuna mtoto ninayemfahamu alikuwa haongei hadi alipokuwa na zaidi ya miaka mitatu na nusu, hata wazazi wake walishakuwa na wasiwasi, na alipoanza kuongea akawa kama cherehani, utadhani analipiza kisasi au kulipia ule muda aliokuwa hawezi kuongea, cha ajabu zaidi ni kuwa akili nazo zinamcheka sana na hana tatizo lolote.

Rafiki yako anaweza akashangaa kuona huyo mtoto wa miaka miwili akaanza kuongea na akawa hana tatizo lolote lile. Pia nadhani huyu wa miaka miwili ni mapema sana kuanza kumweka kwenye kundi la wenye autism. Pia kutokana na kuwa kaka yake ana autism na anamwigiza kwa kila kitu inakuwa vigumu kwake kuonesha hulka yake kwa umri wake. Hivyo huyo inabidi kusubiri hadi awe na miaka kama mitatu hadi minne ndo itaeleweka kuwa naye ana hiyo autism au hana.

Mwisho ni kuwa vyakula vya watoto wenye autism inabidi kuchagua visivyowekwa rangi rangi na pia viwe GLUTEN FREE, yaani visivyo na "GLUTEN". Hii Gluten inawaathiri sana na inawaongezea hiyo hali. Kwa wale watoto wapendao Crisps sana, basi nzuri ni zile za"READY SALTED" tu, nyingine zote si nzuri ni bora wasipewe au wasilishwe hizo. Kwa kifupi ni kuwa hata hizi binzari binzari, (hata Pilau), ketchup soda soda (mirinda,, hizi cola cola, fanta nk) si nzuri kabisa.

Nimechelewa kukujibu kwani nipo safarini na upatikanaji wa internet ni tatizo kidogo.
 
Ngugu Lamba,
Wengi wanasema siyo ya kurithi, ila inatokea tu, zipo familia zenye watoto watatu ambao wote wana autism, chanzo au sababu bado ni tata. Wengine wanasema inahusiana sana na chanjo nyingi za watoto, wengine wanasema hapana ila inatokea tu. Hapo bado wataalam napo hawajapata jibu kamili. Wengine wanasema ni hali fulani ambayo inaongezewa na chanjo za utotoni, hususan kuanzia miezi kumi na nane hadi miaka mitatu.

Mimi pia sijui chanzo ni nini ila nimefuatilia uchanguzi wa pande zote mbili, inaelekea kama pande zote zina sababu ambazo zinaonesha kama za msingi, na kwa sabanu hizo mimi binafsi nipo katikati 50/50 pande zote mbili. Ila nahisi chanjo inawezekana kabisa kuchangia kuleta hiyo hali, kwani wataalam wengine wanasema, ingawa siyo hali ya kurithi wapo watoto wengine ambao wakichomwa hizo chanjo tatu za pamoja basi zinaamsha hiyo hali, na kama wangechomwa chanjo hizo tatu moja moja hiyo hali isingeamshwa (mfano labda hata wewe ungechomwa zote kwa mpigo labda ungepata autism).

Mimi nitacho kushauri ni kuwa kama Mwenyeezi Mungu akikujalia ukapata mtoto/watoto wengine basi hakikisha hizo chanjo wanazopatiwa ni zile za moja moja (ingawa zinagharimu) na siyo hizo tatu kwa mpigo (au MMR kwa jina la kitaalam). Kwani inawezekana kabisa ikawa ni kitu cha kurithi toka kwa wazazi wote wawili kinachosababisha kuwa ikichanganyika na hizo MMR inaleta hiyo hali ya autism.

mtoto wako mkubwa kutoweza kuchanganya maneno ndivyo ilivyo kwa hao wenye autism, na ndiyo maana mwanzoni nikwambia unapoongea nae/nao jaribu kupunguza maneno uyasemayo ili aelewe na pia utumie zaidi vitendo na vielelezo. Unapoongea sentensi ndefu, au maneno mengi basi wanakuwa hawaelewi kabisa (wanasikia kama mayowe au mzozo mzozo bila mpangilio wowote, na baada ya hapo wanapandwa na hasira na kuanza labda kuvunja au kutupa vitu au hata kugalagal chini-wataalam wanasema sauti waisikiayo ni kama ile ya mkwaruzo wa sufuria na kijiko/chuma etc. ambayo huwa inaumiza meno au masikio kwetu sisi).

Pia vyakula ulivyovitaja nadhani vyote vinamwongezea hiyo hali huyo wa pili, (nadhani ndo maana haongei). Ina maana kama ukipunguza sana, au ukiweza kumwachisha kabisa vitu kama crisps, chocolate nk basi tofauti yake utaiona katika siku moja. Tatizo ambalo lipo ni kuwa ina maana kumbadilishia siyo rahisi kwani hiyo hali inasababisha wawe na obsession na hivyo vyakula. Unachotakiwa kufanya ni kununua spesho ambavyo nadhani kuna baadhi ya maduka wanauza,ambavyo havina hivyo vitu vinavyoongezea hiyo hali nitajaribu kutafuta jina la kitaalam ili nikupatie.

Naona niishie hapa, ila narudia usisite kuuliza kama kuna ambacho hujakielewa.
Choveki naomba msaada wa mawazo Mimi pia nna mtoto mwenye shida hiyo japo haipo serious kupitiliza kwan mtoto anaongea japo kidogo ila kuunganisha sentensi ndio shida ana umri wa miaka 7, lakin kujieleza n shida...anaweza kusema Fulani kanipiga lakini ukimuuliza amekupigia nini ni mtihani kukupa maelezo...tabia anayoipenda sana ni kuruka ruka huku na kule anaweza akaruka hata masaa matatu mfululizo na ukimkataza yupo radhi akutoroke akarukie sehem ambayo haupo...je nikimdhibiti kuruka ni vibaya ??
 
Back
Top Bottom