Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature currently requires accessing the site using the built-in Safari browser.
Choveki
Ahsante sana kwa hii information. Hata mimi nina rafiki yangu ana watoto wawili mmoja 7yrs mwingine 2yrs ila wote wana tatizo la kuweza kuongea. Nafikiri hii itaweza kuwapa msaada wa kutatua hili tatizo.
Je ni katika umri gani mtoto anastahili kuanza/kujifunza kuongea (Ideal Age?).
Choveki naomba msaada wa mawazo Mimi pia nna mtoto mwenye shida hiyo japo haipo serious kupitiliza kwan mtoto anaongea japo kidogo ila kuunganisha sentensi ndio shida ana umri wa miaka 7, lakin kujieleza n shida...anaweza kusema Fulani kanipiga lakini ukimuuliza amekupigia nini ni mtihani kukupa maelezo...tabia anayoipenda sana ni kuruka ruka huku na kule anaweza akaruka hata masaa matatu mfululizo na ukimkataza yupo radhi akutoroke akarukie sehem ambayo haupo...je nikimdhibiti kuruka ni vibaya ??Ngugu Lamba,
Wengi wanasema siyo ya kurithi, ila inatokea tu, zipo familia zenye watoto watatu ambao wote wana autism, chanzo au sababu bado ni tata. Wengine wanasema inahusiana sana na chanjo nyingi za watoto, wengine wanasema hapana ila inatokea tu. Hapo bado wataalam napo hawajapata jibu kamili. Wengine wanasema ni hali fulani ambayo inaongezewa na chanjo za utotoni, hususan kuanzia miezi kumi na nane hadi miaka mitatu.
Mimi pia sijui chanzo ni nini ila nimefuatilia uchanguzi wa pande zote mbili, inaelekea kama pande zote zina sababu ambazo zinaonesha kama za msingi, na kwa sabanu hizo mimi binafsi nipo katikati 50/50 pande zote mbili. Ila nahisi chanjo inawezekana kabisa kuchangia kuleta hiyo hali, kwani wataalam wengine wanasema, ingawa siyo hali ya kurithi wapo watoto wengine ambao wakichomwa hizo chanjo tatu za pamoja basi zinaamsha hiyo hali, na kama wangechomwa chanjo hizo tatu moja moja hiyo hali isingeamshwa (mfano labda hata wewe ungechomwa zote kwa mpigo labda ungepata autism).
Mimi nitacho kushauri ni kuwa kama Mwenyeezi Mungu akikujalia ukapata mtoto/watoto wengine basi hakikisha hizo chanjo wanazopatiwa ni zile za moja moja (ingawa zinagharimu) na siyo hizo tatu kwa mpigo (au MMR kwa jina la kitaalam). Kwani inawezekana kabisa ikawa ni kitu cha kurithi toka kwa wazazi wote wawili kinachosababisha kuwa ikichanganyika na hizo MMR inaleta hiyo hali ya autism.
mtoto wako mkubwa kutoweza kuchanganya maneno ndivyo ilivyo kwa hao wenye autism, na ndiyo maana mwanzoni nikwambia unapoongea nae/nao jaribu kupunguza maneno uyasemayo ili aelewe na pia utumie zaidi vitendo na vielelezo. Unapoongea sentensi ndefu, au maneno mengi basi wanakuwa hawaelewi kabisa (wanasikia kama mayowe au mzozo mzozo bila mpangilio wowote, na baada ya hapo wanapandwa na hasira na kuanza labda kuvunja au kutupa vitu au hata kugalagal chini-wataalam wanasema sauti waisikiayo ni kama ile ya mkwaruzo wa sufuria na kijiko/chuma etc. ambayo huwa inaumiza meno au masikio kwetu sisi).
Pia vyakula ulivyovitaja nadhani vyote vinamwongezea hiyo hali huyo wa pili, (nadhani ndo maana haongei). Ina maana kama ukipunguza sana, au ukiweza kumwachisha kabisa vitu kama crisps, chocolate nk basi tofauti yake utaiona katika siku moja. Tatizo ambalo lipo ni kuwa ina maana kumbadilishia siyo rahisi kwani hiyo hali inasababisha wawe na obsession na hivyo vyakula. Unachotakiwa kufanya ni kununua spesho ambavyo nadhani kuna baadhi ya maduka wanauza,ambavyo havina hivyo vitu vinavyoongezea hiyo hali nitajaribu kutafuta jina la kitaalam ili nikupatie.
Naona niishie hapa, ila narudia usisite kuuliza kama kuna ambacho hujakielewa.