Authentic vs. Replica: Kwanini vilabu vya Tanzania vinatoa jezi aina moja tu?

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Baada ya jezi za Simba SC kutoka nimeamua kuja na uzi kwa wale wapenzi wa kuvaa jezi tujadili kwanini timu za Tanzania hazitoi jezi kwaajili ya matumizi ya kila siku kwa mashabiki.

Kabla ya kufika mbali tuongelee hizi aina mbili za jezi, Authentic na Replica.

Authentic na Replica ni jezi zinazofanana kwa kila kitu ila ni matoleo mawili tofauti yanayotofautiana katika matumizi na ubora.

Authentic ni aina ya jezi zinazotengenezwa kwa ubora na teknolojia ya hali ya juu kwaajili ta matumizi ya wachezaji wanapocheza uwanjani. Hutumia vitambaa imara na huwa haziachi nafasi kubwa zinapovaliwa ili kumuwezesha mchezaji kuwa huru na jezi yake isiweze kukamatwa na mpinzani pindi awapo uwanjani.

Replica hizi hutengenezwa maalumu kwaajili ya matumizi ya mashabiki, hutengenezwa kwa kitambaa imara ili kuweza kudumu pamoja na kuwa zinafuliwa mara kwa mara.

Tofauti ya hizi aina mbili ipo hapa:

1. Ukaaji mwilini.
Authentic huwa zinabana ili kumuwezesha mchezaji kuwa huru pindi awapo uwanjani na humsaidia jezi yake kutokamatwa na mchezaji wa timu pinzani.

Replica zina nafasi kubwa kwaajili ya shabiki kuwa huru pindi anaposhangilia timu yake uwanjani pia akivaa iweze kumpa nafasi katika mwili.

2. Aina za vitambaa
Authentic kitambaa chake ni chepesi na huwa na mashimo mengi madogo kuruhusu uingizaji hewa.

Replica hutengenezwa kwa kitambaa kizito ambacho hakina uingizaji hewa mwingi (yaani mashimo madogo kwenye kitambaa). Jezi hizi sio za kunyoosha na kitambaa chake hudumu kwa muda mrefu.

3. Nembo (Logo)
Authentic nembo zake hubandikwa kwa moto na huwa ni nyepesi.

Replica huwa na nembo sawa na za authentic ila zinashonewa katika kitambaa na huongeza uzito.

Sasa tukirudi katika mada yetu baada ya kujua hizi tofauti, timu zetu zinapaswa kuwa na aina hizi mbili za jezi kwasababu moja kuu:

Replica zina kitambaa imara kinachoweza kuhimili kufuliwa mara kwa mara, nembo zake zimeshonewa hivyo zitadumu mpaka kitambaa kitakapochakaa. Hivyo zinawafaa mashabiki kwakuwa jezi moja huweza kuvaliwa msimu mzima hivyo inahitajika jezi ambayo inamudu kufuliwa kila mara na kubaki katika ubora.

Aina hizi zote ziwe zinapatikana madukani na ibaki kuwa maamuzi ya mtumiaji ni aina ipi ya jezi anapendelea.

Mfano timu za nje huwa zinaachia aina hizi zote mbili ili kuendana na mapenzi ya mashabiki. Chukulia mfano jezi zinazouzwa hapa Tanzania za vilabu kama Manchester United, Real Madrid na timu nyingine zinazotengenezewa vifaa vyake na Adidas, ukinunua jezi yake hapa bongo inayofanana na Authentic baada ya kufua mara kadhaa tu utaona ile mistari (Adidas Stripes) ya Adidas inaanza kubanduka na rangi za logo kupauka ila ukichukua inayofanana na Replica itadumu zaidi, kitu pekee kitachakaa kwa haraka ni nembo ya mdhamini ambayo huwa imebandikwa kwa moto.

Ni hayo tu.

Man.%20Utd.jpg
 
Na vipi kuhusu jezi inatolewa na inafafa kama Night dress
Mimi naona simba tumepata faida Coz hiyo jezi yetu tunaweza kuvaa wakati wa kulala
Kwa hili naupongeza uongozi wetu imara wa simba na vunjabei mzee wa chimbo za kariakoo
 
Pia kwenye hilo swala la jezi kwa msimu huu mpya tumeongeza tarehe ya kuzaliwa ya Boss MO29 ila katika ya msimu tukitoa jezi nyingine kama kawaida yetu tutaongeza tarehe ya kuzaliwa ya Barbra na Vunjabei

Naomba kuwasilisha ndugu waandishi wa habari!

bwege kabisa wewe.
dah!,watu mnakero mpaka basi
 
Back
Top Bottom