#COVID19 Austria yaweka hatua za kuifunga nchi kutokana na Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Austria imekuwa nchi ya kwanza katika Ulaya Magharibi kutangaza tena hatua za kusitishwa shughuli za nchi kupambana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Kansela wa Austria Alexander Schallenberg amesema hatua hiyo ya kufungwa shughuli za nchi itaanza kutekelezwa Jumatatu na agizo la kumtaka kila mtu kuchanjwa dhidi ya virusi hivyo itaanza Februari mosi.

Nchi jirani Ujerumani imeonya huenda ikafuata mkondo huo, hali inayosababisha mtikisiko katika masoko ya hisa yakihofia kuanguka uchumi.

Wimbi la nne la maambukizi limeitumbukija Ujerumani, ambayo ndio nchi kubwa kabisa kiuchumi Ulaya, katia hali ya dharura ya kitaifa. Waziri wa Afya Jehns Spahn amewahimiza watu kupunguza mikusanyiko, akionya kuwa chanjo pekee hazitapunguza idadi ya maambukizi.
 
Back
Top Bottom