Austerity measures in the West Vs JK's big govt

ishalua

Member
Dec 3, 2008
10
20
Wana JF,

Wakati serikali za wenzetu wa Magharibi zikichukua hatua ngumu za ki-state ili kurekebisha mgogoro uliopo na utakaokuja wa hali mbaya ya kiuchumi, sisi ni kama hatutumii mwanya huu kujifunza kutoka kwao. Serikali za Uyunani, Uspanyola, Uingereza, Ufaransa na kwingineko wameanza kupunguza matumizi ya government coffers ikiwa ni pamoja na kupunguza ukubwa wa serikali yenyewe na hata serikali zingine zikienda mbali kutaka kufanya marekebisho ya kupunguza utegemezi toka serikali kuu na kupelekea sehemu kubwa ifanyike na serikali za mitaa pamoja na 'watu kujitolea'. Makala hii hapa chini toka The Economist inanipa kujiuliza, je serikali yetu huwa inafikiria mbali namna ya kuchukua hatua ngumu za ki-state ili kurekebisha pamoja na kuboresha hali za watu wake za hapo baadae au ndio ile kupeana asante za uchaguzi, nk? Unless kama serikali inaweza kuwa na jitihada za makusudi kabisa ku-cast their nets wider kukusanya kodi pamoja na kuboresha sera zenye lengo la kuongeza shughuli za uzalishaji _kwa walio wengi_, hapa tulipo na tunakokwenda ni kama kutembea kwenye ukungu!

Soma mwenyewe kisha tafakari!

Reforming the state

Radical Britain
Britain has embarked on a great gamble. Sooner or later, many other rich-world countries will have to take it too

Reforming the state: Radical Britain | The Economist
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Wa kwetu yeye anaongeza ukubwa wa serikali akifikiri ndio ufanisi. Sijui alisomea wapi hiyo degree yake maana mambo mengine hata mwanafunzi wa chekechea anayajua na yeye hayajui. Mhhhhhh
 
Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Kama kuna jambo linawafanya viongozi wetu waonekane kama limbukeni ni hii tabia yao ya kutaka kuishi peponi huku wakitembeza bakuri kuomba msaada kutoka kwa wafadhili hata kwaajili mishahara kwaajili ya watumishi wake.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Sisi tuko ULIMWENGU WA TATUUUU ndani ya shimo chini chini kabisaaaa!!! Na asante kwa washikaji lazima tutoe kwa marafiki kikazi kwa gharama yawalipa kodi. Halafu bila aibu bado tunaenda na bakuli kwa wahisani tena kwa kuwadanganya figures ili hela za kuja kununulia chaguzi zijazo zipatikane haraka.

Kauli mbiu, 'mwisho wa uchaguzi mkuu mmoja ni mwanzo wa maandalizi wa uchaguzi mkuu mwingine'. Mmmhhh!!!
 
KunjyGroup

JF-Expert Member
Dec 7, 2009
352
170
'Asili mia therasini ya budget inaibiwa kila mwaka na wajanja wachache. Mwaka huu tunategemea asili mia therasini na tatu ya budget itaibiwa...' Huyo alikuwa jk wakat anazindua jengo la takukuru huko Mwanza. Think bout it. A president proudly admitin theft of public funds. Unategemea nin kwa mtawala kama huyu? Regea mameno ya Mramba juu ya ununuzi wa ndege ya rais.
Hamna kitu kama austerity measure kutoka sirikali ya sisiem
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
"Imitate what is good" is written. Tz leaders turn it to mean 'imitate what isn't good'.

When they set-out their strolls (Mwl Nyerere's early days and foward) they stubornly opted for quantity over quality. And funny but lucky enough they cannot see yonder the maze! They're perfectly blind and numb.

I sometimes resign to conclude my thoughts in this little self-constructive demo, in relationship to the current-past leaders. It goes:
" ....since wananchi periodically sends representatives to us (rulers) thru Bunge/Councilors .....by the same simplicity and measure we (rulers) obliged to give the 'chosen few' (individually) maendeleo so to represent us (rulers) back to wananchi. And in any case, if they querry us (leaders) why we served only the very fewest such favors and not all the citizens ...this is our thumb reply "what agreement or binding is there between we (rulers) and you (citizens)?. Further (to appease) behold how developed your representatives are now comparing to when you sent them up"

It's thus officialy cosmestcily state. ... where superficiality is virtue.
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,703
0
Wana JF,

Wakati serikali za wenzetu wa Magharibi zikichukua hatua ngumu za ki-state ili kurekebisha mgogoro uliopo na utakaokuja wa hali mbaya ya kiuchumi, sisi ni kama hatutumii mwanya huu kujifunza kutoka kwao. Serikali za Uyunani, Uspanyola, Uingereza, Ufaransa na kwingineko wameanza kupunguza matumizi ya government coffers ikiwa ni pamoja na kupunguza ukubwa wa serikali yenyewe na hata serikali zingine zikienda mbali kutaka kufanya marekebisho ya kupunguza utegemezi toka serikali kuu na kupelekea sehemu kubwa ifanyike na serikali za mitaa pamoja na 'watu kujitolea'. Makala hii hapa chini toka The Economist inanipa kujiuliza, je serikali yetu huwa inafikiria mbali namna ya kuchukua hatua ngumu za ki-state ili kurekebisha pamoja na kuboresha hali za watu wake za hapo baadae au ndio ile kupeana asante za uchaguzi, nk? Unless kama serikali inaweza kuwa na jitihada za makusudi kabisa ku-cast their nets wider kukusanya kodi pamoja na kuboresha sera zenye lengo la kuongeza shughuli za uzalishaji _kwa walio wengi_, hapa tulipo na tunakokwenda ni kama kutembea kwenye ukungu!

Soma mwenyewe kisha tafakari!

Reforming the state

Radical Britain
Britain has embarked on a great gamble. Sooner or later, many other rich-world countries will have to take it too

Reforming the state: Radical Britain | The Economist

Heri yako wewe unaye ona mbali hivyo.Wao sidhani kama wanaona hata mbali zaidi ya urefu wa pua zao.Kwajinsi hali ya uchumi ilivyo mbaya Ulaya na Marekani, kama wangekuwa wanaona mbali wangeanza kujiuliza kwamba kama hali ya magwiji hayo hali ni mbaya hivyo,sisi hali yetu hatimaye itakuwaje?Lakini sioni kama wanaliwaza hilo, badala yake wanaponda miraha tu,kazi kweli kweli. The truth is kama hawatachukua any austerity measures,tutaishia makaburini.We won't survive.
 
ishalua

Member
Dec 3, 2008
10
20
Nakubaliana na kwamba uongozi wetu huwa hautafakari kabisa juu ya ukubwa wa serikali na athari zake katika matumizi ya pesa za walipa kodi (ambao ni wachache mno!). Sasa hili suala la kupanua wigo wa kodi angalau basi mfuko wa serikali uzidi kuongezeka kila mwaka na idadi ya watanzania kuongezeka katika kuzalisha mali kwa faida tutaanza lini? Au kama tumeshaanza, tutaanza kuona lini utekelezaji wake?
 
Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,325
0
Sisi tuko ULIMWENGU WA TATUUUU ndani ya shimo chini chini kabisaaaa!!! Na asante kwa washikaji lazima tutoe kwa marafiki kikazi kwa gharama yawalipa kodi. Halafu bila aibu bado tunaenda na bakuli kwa wahisani tena kwa kuwadanganya figures ili hela za kuja kununulia chaguzi zijazo zipatikane haraka.

Kauli mbiu, 'mwisho wa uchaguzi mkuu mmoja ni mwanzo wa maandalizi wa uchaguzi mkuu mwingine'. Mmmhhh!!!

Mkuu,
hapo nilipokoleza umekosea sana, kwa taarifa tuu, ukweli ni kwamba sasa hivi Tanzania ipo ulimwengu wa NNE, imepitiliza ulimwengu wa 3 na imedidimia hadi kwenye huo ulimwengu mpya wa 4!
Sijui kama raisi wa NEC (JK) ameshawataarifu wadanganyika kwenye hili suala!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom