Aunt Ezekiel: Tununue bongo movie, movie za mbele hazituhusu

Watu wengi wanazipotezea bongo movie kwasababu sio wabunifu wanatengeneza kazi mbovu yaani jambazi anavua viatu kuingia kufanya tukio!
20aecc8e906dc6be43d324f47c9fb8f2.jpg
 
Tatizo hizo Bongo movie zenyewe hazina uhalisia wa mTanzania...wanaiga maisha ya nje! Sa si bora niwatch movie ya nje asilia kuliko Bongo movie inayokopi maisha ya nje!
 
JF bana, kila mtu anajifanya anacheki movie za mbele tu, Auntie Ezekiel asijali, sisi wazalendo tutaangalia sana, tena ngoja niongeze ratiba ya kuangalia.
Hakuna anayejifanya Bali tunaongea ukweli..soko la movie bongo limeanza juzi tu kama sikosei. 2003 au 2004 na movie ya girlfriend..
Sasa kwa mm ambaye nilianza fwatilia filamu tokea kitambo lazima utumie akili ya ziada kunitoa Kwenye filamu nilizozoea...
Wacha nikupe mifano.. Kwenye miaka ya 2005 hadi 2010 walikuja na mbinu wanazotumia bongo fleva now.. Yaani kutafuta kick kupitia magazeti ya shigongo... Kuna kick moja niliipenda Rich na jb.. Walijifanya kugombea movie.. Mara wakapigwa picha wanakunjana mbele za watu kisa kila mtu anasema movie ni yake.. Nikasema hii ikitoka Lazima nikaicheki.. Basi siku imetolewa nikajitorokea shule maana nilikuwa boarding nikazama kibanda umiza kitaani.. Doooo nilichoshuhudia nikajuta kwa nn nilitoroka kuja angalia huu upumbavu..
Tokea hiyo siku nikaacha fwatilia bongo movie kabisa hata waibue story gani.. Labda niwe ugenini na nikute wanaangalia ndio utanikuta naangalia nami..
Yaani movie zingine zina makosa ya wazi kabisa.. Kipaza kinaonekana.. Sauti mbovu.. Scenes zisizo na maana Kwenye mtiriko wa hadithi kupewa robo saa.. Yaani kuangalia bongo movie ni kero haswa kwa sisi tulioanza na filamu za nje...
 
Bongo movie wanataka mapenzi na kugombaniana mabwana na wanawake..hiyo ndiyo furaha yao kuhusu soko si lazima. Acha watu wafanye kile kitu kinachowapa raha na furaha Tele......wabaki na movie zao, mbona mziki unashabikiwa sana japo hakuna cha muhimu waimbacho wasanii wetu
 
Utafurahi Kwenye filamu ya bongo kuwe na scene ya nje ya tanzania.. Basi watatafuta chumba cha hoteli na kufunga mapazia kabisa... Yaani aliyeko nje Scene zake zitakuwa Kwenye hicho chumba pekee
 
Hakuna anayejifanya Bali tunaongea ukweli..soko la movie bongo limeanza juzi tu kama sikosei. 2003 au 2004 na movie ya girlfriend..

Sawa nimekusoma, ila hujanibadili msimamo, hivi unajua kuna watu wanaponda tu huku hata hizo movie za nje hawaangalii?

Yaani ili mradi na wao waonekane wameponda.
 
Na wao waache kukocopy na kupaste... No one likes fake.. We stick on the original..
Mnacopy story mpaka dressing code.. Na uzungu mwingi kwenye movie za Nyumbani mnaboa
 
Shida ya bongo wanaigiza vitu walivyoona kwenye muvie za wenzetu kama sio india basi us au nigeria ss si bora nipite shortcut nikaangalie moja kwa moja muvie ya us. Kingine si watunzi wala madirector wako kimaslahi zaid nadhani na sio passion same apply to wasanii wanatafuta kick zaid ya kipaji ss. Watafute shule za sanaa nje wakasomee kwanza otherwise wanasafar ndefu
 
Sawa nimekusoma, ila hujanibadili msimamo, hivi unajua kuna watu wanaponda tu huku hata hizo movie za nje hawaangalii?

Yaani ili mradi na wao waonekane wameponda.
Sasa hao ndio tunawaita wanafki.. Yaani kitu hukifahamu na unakizungumzia...
Ila huwa najiuliza mbona waliweza kututeka na maigizo yao ya kipindi kile.. Miaka ya tisini mwishoni..
Na kuna igizo moja waliigizia bagamoyo.. Uigizaji na uongizaji ulikuwa mzuri sana ingawa sikulifwatilia igizo lenyewe ila nilipenda lilivyopangiliwa.. Ila nilikuja fwatilia baadae nikagundua halikuongozwa na wabongo bali wageni...
Nimelisahau jina kidogo ila jamaa alikuwa kiwembe balaa ana afro... Hata sauti ilikuwa poa sana
 
Bongo movie wanataka mapenzi na kugombaniana mabwana na wanawake..hiyo ndiyo furaha yao kuhusu soko si lazima. Acha watu wafanye kile kitu kinachowapa raha na furaha Tele......wabaki na movie zao, mbona mziki unashabikiwa sana japo hakuna cha muhimu waimbacho wasanii wetu
Hawa watu ni maarufu kwa maisha yao nje ya sanaa.... Ila ukifwatilia upande wa sanaa utajiuliza why wanamwita super star
 
Sasa nyie wana-comment wa JF mbona mnaponda vya kwetu.
Tunabomoa au tunajenga.
Ila kwenye series hamunitoi ng'oo hasa drama za kikorea ndo drama zangu.
Ushaitazama swallow the sun wewe au ume-watch The Man called God.
Wakorea noma namely siyo wa sport sport.
BM sitazami tena.
 
Sijakuelewa.. Sisi tunaponda ila kumbe nawe umelowea korea..
Huwa nikikaa na kuangalia movie za miaka ya 70 kama godfather... Rocky au sholay.. Huwa najiuliza hivi kweli miaka zaidi ya 40 hatujafikia hata robo ya walipokuwa miaka ya 70
 
Watu wengi wanazipotezea bongo movie kwasababu sio wabunifu wanatengeneza kazi mbovu yaani jambazi anavua viatu kuingia kufanya tukio!
20aecc8e906dc6be43d324f47c9fb8f2.jpg
Eti jambazi pekupeku! Hii ya mwaka.. Utafikiri hadithi ya bulicheka na Yule mwenzake Sijui Nani vile! Nimemsahau
 
Sasa hao ndio tunawaita wanafki.. Yaani kitu hukifahamu na unakizungumzia...
Ila huwa najiuliza mbona waliweza kututeka na maigizo yao ya kipindi kile.. Miaka ya tisini mwishoni..
Na kuna igizo moja waliigizia bagamoyo.. Uigizaji na uongizaji ulikuwa mzuri sana ingawa sikulifwatilia igizo lenyewe ila nilipenda lilivyopangiliwa.. Ila nilikuja fwatilia baadae nikagundua halikuongozwa na wabongo bali wageni...
Nimelisahau jina kidogo ila jamaa alikuwa kiwembe balaa ana afro... Hata sauti ilikuwa poa sana

Unamzungumzia Chuma, nalikumbuka lile igizo.

Issue kubwa kwenye hii industry ni kwamba wengi wanaoingia kwenye hiyo fani shule iliwashinda, ma-director walio kwenye hiyo fani pia shule siyo kiviile, kiasi kwamba ubunifu ni mdogo sana hivyo wanaishia kufanya copying, tena hata kile wanacho copy wanapunguza standard. Unakuta eti movie owner ndiye director, ndiye main editor, ndiye mtungaji, ndiye location manager etc etc na mtu huyo ndo Auntie Ezekiel au Madam Sepetu, kwa nini isiwe famba?

Marehemu Kanumba kama angeendelea kuwepo leo hii tungekuwa na industry ya movie iliyo katika viwango vya juu sana, jamaa alikuwa creative sana, hivyo hata wapinzani wake kina Ray (Vincent Kigosi) ilibidi wa-raise game yao kukimbizana na soko, vinginevyo angeuza Kanumba tu. Toka alivyoondoka hakuna tena ule ushindani na ubunifu kwenye hii tasnia.

Kanumba alikuwa pia anaweza kutrain watu wakaingia kwenye movie hata kama hawana vipaji wakafanya vizuri, watu kama hawa kina Auntie, Wema, Patcho, Jeniffer, Uwoya etc etc ni watu ambao jamaa aliwa-introduce na wakawa wanafanya vizuri.

Kwa sasa tunasubiria kama anakuja mwingine tena kuokoa hili jahazi, ubunifu.
 
Back
Top Bottom