Vito Andolini
Member
- Jun 11, 2013
- 66
- 28
Kuna huyu sijui ndio msanii au nani anaeitwa Aunt Ezekiel kwa muda wa wiki nzima sasa ameleta tafrani kwenye familia yangu.
Kilichopo ni kwamba kupitia gazeti la udaku linaloitwa IJUMAA la terehe 31 May mwaka huu wawili hao (Ezekiel na gazeti la Ijumaa) wamechapisha kwamba Aunt Ezekiel ana nia ya kuwasaidia wasanii chipukizi ili wapate mafanikio,, na mwisho akamalizia kwa kuweka number ya simu ya mdogo wangu.
Kinachotokea sasa mdogo wangu amekua akisumbuliwa mfululizo na simu za watu wanaotaka msaada huo. simu zimekua zikimiminika hadi usiku wa manane.
Cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya wanaopiga simu sio waelewa/sio wastaarabu wamekua wakikataa kata kata tunapowaambia ukweli kwamba hiyo number sio ya huyo mtu wanaemtaka, wanasisitiza na kung'a ng'ania mpaka inakua kero.
Kutokana na umuhimu wa simu kwa shughuli za kila siku za mdogo wangu tunashindwa kuzima simu hiyo ili kuepuka usumbufu, hivyo tuliamua kwenda kuweka taarifa kituo cha Polisi Ng'ambo (hapa Zanzibar) huko tulipata ushauri kwamba tujaribu kuwasiliana na wachapishaji wa gazeti hilo.
Wachapishaji tuliwapata, walichotujibu ni kwamba tujaribu kuwasiliana na mhariri kwani hiyo number wao wamepewa na huyo Ezeckil mwenyewe tena kwa maandishi. Bahati mbaya sana mhariri huyo tumeshindwa kupata mawasiliano nae.
Kupitia baraza hii adhimu ya JF naomba wadau kwanza wapate ujumbe huu, kisha watusaidie mambo yafuatayo
Kwanza baraza itusaidie kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba namba hiyo ***617260 iliyoachwa na huyo Ezeckiel na kuchapishwa na gazeti la Ijumaa sio ya kwake hivyo wasipoteze muda na fedha zao na wasitusumbue,,
Pili kama kuna ushauri mwengine wa kisheria kutoka kwa wana baraza hii mtusaidie ili kukomesha tabia hii
Tatu naomba nisaidiwe namna ya kutuma post katika blog ya michuzi ili pia niweze kufikisha ujumbe huu.
Asanteni