Aunt Ezekiel na Shigingo mnaisumbua familia yangu


Vito Andolini

Vito Andolini

Member
Joined
Jun 11, 2013
Messages
66
Likes
9
Points
15
Vito Andolini

Vito Andolini

Member
Joined Jun 11, 2013
66 9 15
Kuna huyu sijui ndio msanii au nani anaeitwa Aunt Ezekiel kwa muda wa wiki nzima sasa ameleta tafrani kwenye familia yangu.

Kilichopo ni kwamba kupitia gazeti la udaku linaloitwa IJUMAA la terehe 31 May mwaka huu wawili hao (Ezekiel na gazeti la Ijumaa) wamechapisha kwamba Aunt Ezekiel ana nia ya kuwasaidia wasanii chipukizi ili wapate mafanikio,, na mwisho akamalizia kwa kuweka number ya simu ya mdogo wangu.

Kinachotokea sasa mdogo wangu amekua akisumbuliwa mfululizo na simu za watu wanaotaka msaada huo. simu zimekua zikimiminika hadi usiku wa manane.

Cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya wanaopiga simu sio waelewa/sio wastaarabu wamekua wakikataa kata kata tunapowaambia ukweli kwamba hiyo number sio ya huyo mtu wanaemtaka, wanasisitiza na kung'a ng'ania mpaka inakua kero.

Kutokana na umuhimu wa simu kwa shughuli za kila siku za mdogo wangu tunashindwa kuzima simu hiyo ili kuepuka usumbufu, hivyo tuliamua kwenda kuweka taarifa kituo cha Polisi Ng'ambo (hapa Zanzibar) huko tulipata ushauri kwamba tujaribu kuwasiliana na wachapishaji wa gazeti hilo.

Wachapishaji tuliwapata, walichotujibu ni kwamba tujaribu kuwasiliana na mhariri kwani hiyo number wao wamepewa na huyo Ezeckil mwenyewe tena kwa maandishi. Bahati mbaya sana mhariri huyo tumeshindwa kupata mawasiliano nae.

Kupitia baraza hii adhimu ya JF naomba wadau kwanza wapate ujumbe huu, kisha watusaidie mambo yafuatayo

Kwanza baraza itusaidie kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba namba hiyo ***617260 iliyoachwa na huyo Ezeckiel na kuchapishwa na gazeti la Ijumaa sio ya kwake hivyo wasipoteze muda na fedha zao na wasitusumbue,,

Pili kama kuna ushauri mwengine wa kisheria kutoka kwa wana baraza hii mtusaidie ili kukomesha tabia hii

Tatu naomba nisaidiwe namna ya kutuma post katika blog ya michuzi ili pia niweze kufikisha ujumbe huu.

Asanteni
 
CYBERTEQ

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
7,415
Likes
264
Points
0
CYBERTEQ

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
7,415 264 0
Nenda TCRA haraka iwezekanavyo ukiwa na nakala ya hilo Gazeti. Kisha fungua kesi ulishitaki gazeti pamoja na huyo Anti nani sjui, wakulipeni fidia kisha wawatake radhi kwenye hilohilo gazeti! FANYA HIVYO SASA.
 
P

PERFECT

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Messages
361
Likes
2
Points
0
P

PERFECT

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2011
361 2 0
Mkuu Vito Andolini Poleni sana,
Inatakiwa uanze ha huyu member TCRA, atakushauri pa kuanzia,
Hii mamlaka sasa inatakiwa ianze kufanya kazi, siyo kila siku longolongo tu,
gazeti issue ijayo linatakiwa wawaombe radhi, wameingilia uhuru wenu wa faragha,

Hii sijujua ka nini jukwaa sahihi, namuachia Invisible
 
Last edited by a moderator:
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
32,019
Likes
5,336
Points
280
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
32,019 5,336 280
Nenda TCRA haraka iwezekanavyo ukiwa na nakala ya hilo Gazeti. Kisha fungua kesi ulishitaki gazeti pamoja na huyo Anti nani sjui, wakulipeni fidia kisha wawatake radhi kwenye hilohilo gazeti! FANYA HIVYO SASA.
huu ndio ushauri wa maana....
 
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
4,216
Likes
1,952
Points
280
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
4,216 1,952 280
Kama hajakosea namba basi tabia hii ni ya kix?%$#@ kabisa
 
Vito Andolini

Vito Andolini

Member
Joined
Jun 11, 2013
Messages
66
Likes
9
Points
15
Vito Andolini

Vito Andolini

Member
Joined Jun 11, 2013
66 9 15
Nawashkuru wote kwa faraja zenu na ushauri wenu, bahati njema nimesikia kwamba kuna ofisi ys TCRA hapa Zanzibar labda tuende huko kupata msaada wao.
 
P

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
1,567
Likes
53
Points
145
P

pilau

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
1,567 53 145
Huyo anaitwa AUNT EZEKIEL GRAYSON "JUJUMAN" Mtoto wa Nyota wa soka wa zamani wa Taifa Stars Yanga na Simba marehemu Ezekiel Grayson 'JUJUMAN' R.I.P....
 
Loy MX

Loy MX

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2012
Messages
1,259
Likes
17
Points
135
Loy MX

Loy MX

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2012
1,259 17 135
Daah au ndo imekuwa mtindo mpya mtu anabuni namba na kuiweka hadharani kwenye udaku hilo ni tatizo...
 
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,680
Likes
34
Points
145
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,680 34 145
huyo aunt ndo yule wanasemaga dume jike?
 
Msarendo

Msarendo

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2011
Messages
9,507
Likes
3,773
Points
280
Msarendo

Msarendo

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2011
9,507 3,773 280
mwambie abadilishe namba ya Simu. Mia.
 

Forum statistics

Threads 1,273,086
Members 490,268
Posts 30,470,815