Aunt Ezekiel afunguka kuhusu nyumba ya kupanga

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,161
2,000
18809011_429242030767775_2002670699537235968_n-e1497887377104.jpg


Baada ya kuandamwa mitandaoni kuwa tangu amekuwa staa bado anaishi nyumba za kupanga maeneo ya Kijitonyama jijini Dar, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefungukia madai hayo kuwa wengi wanaongea bila kujua undani wa maisha yake.

Akizungumza na Star Mix, Aunt alisema ameamua kuishi maisha ya kupanga kwa sababu ya ukaribu na kazi zake na kama ni nyumba yake ipo maeneo ya Kigamboni.

“Nawashangaa sana wanaosema hivyo. Nimepanga katikati ya mji ili nifanye kazi zangu kwa wepesi na kama ni nyumba mbona ninayo Kigamboni?” Alihoji Aunt ambaye ni mzazi mwenza na Moze Iyobo.


Muungwana
 

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
4,596
2,000
Kuwa staa Bongo kumbe sio ishu kama kujenga nalo tatizo mbona walimu wa shule za misingi wana mijengo na wanaendesha magari manene
 

ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
12,081
2,000
wenye nazo wengi wanahusudu kupanga kuliko kuishi kwenye mijengo yao.....wahindi ni mfano mdogo tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom