Aunguzwa Vibaya Mkono na Mama wa Kambo Kwa Kudokoa Samaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aunguzwa Vibaya Mkono na Mama wa Kambo Kwa Kudokoa Samaki

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, May 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;"></td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Mtoto Matiko akionyesha mkono wake uliounguzwa moto na mama yake wa kambo</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Tuesday, May 18, 2010 3:26 AM
  Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba wa wilaya ya Tarime mkoani Mara ameunguzwa vibaya vidole vyote vya mkono wake na mama yake wa kambo baada ya kudokoa samaki aliporudi kutoka shule akiwa na njaa</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Polisi wilayani Tarime wamemtaja mtoto huyo kuwa ni Matiko Mwita anayesoma shule ya msingi ya Abainano.

  "Mama yake wa kambo alikasirika na kuunguza mkono wake wa kulia kwa moto wa mkaa sababu ikiwa ni kitendo cha mtoto huyo kula kipande cha samaki aliporudi toka shuleni", alisema kamanda msaidizi wa polisi wilaya ya Tarime, Constantine Masawe.

  "Nilikuja toka shule na kukuta samaki na ugali lakini mama yangu wa kambo aliponikuta nakula alinuuliza kwanini nakula chakula na ndipo alipoanza kuniunguza na moto mkononi", alisema mtoto Matiko.

  Matiko aliungua vibaya vidole vyote vitano vya mkono wake wa kulia kufuatia kitendo hicho cha mama yake wa kambo.

  Polisi wanamtafuta mwanamke huyo ambaye alikimbia pamoja na mumewe baada ya suala hilo kufikishwa polisi.

  Kamanda Masawe alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Pili Mwita mkazi wa kijiji cha Motana wilayani Tarime mkoani Mara.

  "Tunamtafuta pia mumewe kwasababu hakutoa taarifa yoyote polisi mpaka mwalimu wake alipomleta mtoto huyo kituo cha polisi".

  Mtoto Matiko baada ya kupatiwa matibabu amepelekwa kwenye kituo cha kulea watoto yatima kilichopo kwenye kijiji cha Gamasara nje kidogo ya Tarime.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Akina Mama wengine ni Makatili sana jamani
  </td></tr></tbody></table>
   
Loading...