Aung'ata na Kuunyofoa Ulimi wa Mwanaume Aliyekuwa Akimbaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aung'ata na Kuunyofoa Ulimi wa Mwanaume Aliyekuwa Akimbaka

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,610
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Monday, August 31, 2009 3:12 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amepoteza kipande cha ulimi wake baada ya mwanamke aliyekuwa akimbaka na kumlazimisha wanyonyane ndimi kuung'ata ulimi wake na kukinyofoa kabisa kipande kikubwa cha ulimi wake. Ronald Douglas McGowan, 32 mkazi wa California, Marekani alipoteza kipande cha ulimi wake baada ya mwanamke aliyekuwa akimbaka na kumlazimisha wanyonyane ndimi, kuung'ata kwa nguvu ulimi wake na kukinyofoa kipande kikubwa cha ulimi huo.

  Katika tukio hilo lililotokea juni 5 mwaka huu, McGowan alimvamia mwanamke huyo nyumbani kwake na kumtisha kwa kutumia silaha huku akijaribu kumbaka na kumlazimisha wanyonyane ndimi.

  Katika hali ya kujilinda mwanamke huyo aliung'ata ulimi wa McGowan na kukinyofoa kipande kikubwa cha ulimi wake na kisha kukitema chini.

  McGowan alikamatwa na polisi baada ya kwenda hospitali kupatiwa matibabu akiwa amekibeba kipande cha ulimi wake mkononi.

  Hata hivyo ilishindikana kukiunga tena kipande hicho cha ulimi na hivyo McGowan ataishi maisha yake yaliyobakia akiwa na ulimi kibubutu.

  McGowan alikuwa akitafutwa na polisi siku nyingi kutokana na matukio matatu tofauti ya ubakaji yaliyotokea katika kipindi cha kati ya mwaka 2007 na 2009.

  McGowan alipandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya ubakaji na kufanya shambulio la kudhuru mwili kwa kutumia silaha.

  Kesi yake inaendelea.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2952734&&Cat=2
   
Loading...