Auawa na kutupwa ****** | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auawa na kutupwa ******

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 4, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  *Wauaji mbaroni
  Na Waandishi Wetu, jijini

  UMATI wa watu jana ulishuhudia mwili wa Mohamed Ramadhani (30), aliyeuawa kinyama kisha kutupwa ****** kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na ugomvi wa simu na viatu.Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo limetokea jana saa moja jioni, Mbagala Kingugi, baada ya marehemu huyo, akiwa na wenzake, wakidaiana mali.

  Imedaiwa kuwa marehemu akiwa na wenzake walikuwa wakibishana kuhusiana kila mmoja kudai mali zake hali ambayo ilizua mzozo baina yao.

  Kutokana na hali hiyo, anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo ambaye alijulikana kwa jina moja la Fadhili alidaiwa kuamua kuondoka na simu ya marehemu hali iliyosababisha marehemu kumfuata nyumbani kwake.

  Imedaiwa kuwa hali hiyo ilisababisha ndugu wa marehemu kuamua kumfuatilia kwa marafiki zake mbalimbali lakini hata hivyo jitihada hizo ziligonga mwamba.

  Imedaiwa kuwa ndugu hao walihangaika maeneo mbalimbali wakimtafuta lakini walimkosa.

  Kaka wa marehemu, Mwinyijuma Mohamed, aliamua kurudi nyumbani na kuendelea na shughuli nyingine, lakini baadaye alipigiwa simu kuwa mdogo wake ameonekana ****** akiwa amekufa.

  Kaka wa marehemu alikwenda eneo la tukio na kumkuta mdogo wake akiwa na majeraha mbalimbali.

  Katika uchunguzi walibaini kuwapo kwa michirizi ya damu inayotoka katika nyumba anayoishi Fadhili.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi lake linawashikilia watuhumiwa watatu kuhusiana na mauaji hayo.

  Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Ajuaye Ally, Hemed Said na Said Hussein ambapo uchunguzi ukikamilika watafikishwa mbele ya sheria.
   
Loading...