Auawa na kutupwa kando ya barabara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auawa na kutupwa kando ya barabara

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, May 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  KIJANA mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Bakari amepoteza maisha kwa kuuawa kikatili na watu wasiojulikana na kumtupa pembezoni mwa barabara huko maeneo ya Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la mauaji lilitokea jana majira ya alfajiri, katika maeneo hayo ambapo maiti ya kijana huyo ilikutwa kando ya barabara katika majani ikiwa imefungwa kamba miguuuni na mikononi.

  Kijana huyo ilidaiwa kuwa ni mwajiriwa na mkazi mmoja maeneo hayo ambapo ni dereva wa familia aliyeajiwa katika familia moja maeneo hayo.

  Kijana huyo alivamiwa na wauaji hao na kumfunga kamba miguuuni na mikononi na kisha kumuua na wezi kuondoka na gari ndogo aliyokuwa akiendesha.

  Ilidaiwa kuwa kijana huyo ni dereva wa familia moja katika maeneo hayo na kila alfajiri hufika katika nyumba hiyo kuwapeleka wanafunzi shuleni na wakati akielekea huko ndipo njiani wezi hao walimvizia na kumpora gari hilo na kumuua na kumtupa kando ya barabara.

  Hata hivyo jeshi la polisi linafanya msako mkali kuwabaini watu waliohusika katika tukio hilo la mauaji.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kila siku matukio ya mauaji yanaongezeka kulikoni?
   
Loading...