Auawa na kundi la watu kwa kuchoma Quran

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mtu mmoja ameuawa na kundi la watu kwa madai ya kuchoma kurasa za Koran katikati mwa Pakistan, Khanewal, polisi wanasema, katika tukio la hivi karibuni la vurugu zinazohusiana na kukufuru ama kukashifu dini nchini humo.

Polisi wanasema zaidi ya watu 80 wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo siku ya Jumamosi katika Wilaya ya Khanewal katika Mkoa wa Punjab.

Ripoti zinasema kuwa mtu huyo alikuwa chini ya ulinzi wa polisi kabla ya umati wa watu kumteka na kumuua kwa kipigo. Mwili wake ulikabidhiwa kwa familia yake na mazishi yaliyofanyika siku ya Jumapili.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan amesema suala hilo: "Litashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria" na kuomba ripoti juu ya maafisa wa Polisi wanaotuhumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kumwokoa mtu huyo.

Munawar Gujjar, mkuu wa kituo cha polisi mjini Tulamba, ambako tukio hilo lilitokea, aliliambia Shirika la Habari la AP kwamba mwathiriwa huyo: "alikuwa na matatizo ya akili kwa miaka 15 iliyopita".

Source: BBC

f01f05a4-af50-4e51-89ef-a29e5858463b.jpg
 
Jamaa kweli alikua mfia dini' Yaan Pakistani kabisa na anajua ni Taifa lenye sehemu kubwa ya waislam na bado kafanya hilo jambo na kweli ashukuriwe Mungu.
Munawar Gujjar, mkuu wa kituo cha polisi mjini Tulamba, ambako tukio hilo lilitokea, aliliambia Shirika la Habari la AP kwamba mwathiriwa huyo: "alikuwa na matatizo ya akili kwa miaka 15 iliyopita".

Ukisoma paragraph ya mwisho utagundua kuwa wenye dini yao wana mihemko sana.
 
Na hata hao askar nao ni wenzao wa walioua.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Munawar Gujjar, mkuu wa kituo cha polisi mjini Tulamba, ambako tukio hilo lilitokea, aliliambia Shirika la Habari la AP kwamba mwathiriwa huyo: "alikuwa na matatizo ya akili kwa miaka 15 iliyopita".

Ukisoma paragraph ya mwisho utagundua kuwa wenye dini yao wana mihemko sana.
Siyo mihemko ila wajinga wakubwa, dalili ya kitu feki ni kulindwa kwa nguvu zote.
 
Dah, watu wanathamini kitabu kushinda hata Mungu mwenyewe aliyewaumba, hata subira tu kwamba labda huyo mtu alikuwa na matatizo ya akili hamna.!
Samia Suluhu akiteua muislamu JF huchafuka kwa malalamiko. Na kwakuwa ni jambo linalowafirahisha huwa wasimamizi wapo kimya.
Huwa huo uvumilivu mnakuwa mmeusahau wapi?

Unadhani waislamu wangekuwa na upuuzi huo wa dharau kwa vitabu vyenu hii nchi ingekuwa na hii amani uionayo?
Kumbuka tu mlivyoshindwa kujibu hoja mkaita mihadhara ya kashfa, uvumilivu mlimuazima jirani!?
 
Munawar Gujjar, mkuu wa kituo cha polisi mjini Tulamba, ambako tukio hilo lilitokea, aliliambia Shirika la Habari la AP kwamba mwathiriwa huyo: "alikuwa na matatizo ya akili kwa miaka 15 iliyopita".

Ukisoma paragraph ya mwisho utagundua kuwa wenye dini yao wana mihemko sana.
Kwakuwa alikuwa na matatizo ya akili basi pole yake. Angekuwa na akili timamu angekuwa kafa kifo cha kujitakia. Hata ukienda sehemu ukakuta watu wanaabudu ng'ombe, we jifanye huoni maana ukimpga teke wanakuua.
Kuna sehemu flani waliwahi kutengeneza sanamu la mwanamama flani wakawa wanalizungusha nyumba kwa nyumba, tena hapa hapa tz, sasa ungelipiga teke nahisi wangekuua.
 
Back
Top Bottom