Auawa katika ugomvi wa kuuziana pete

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Moshi. Samson Conrad (24), ameuawa akidaiwa kukatwa na sime shingoni na Kereto Lekoko katika ugomvi wa kudaiana pete.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,”amesema Kamanda Issah

Chanzo: Mwananchi
 
Kilimanjaro na hela
ni stori nzuri ya mapenzi kuliko story yoyote duniani
 
alitaka apate pete bila kutoa pesa ,acha achezee sime tu.
 
Wamasai wazuiwe kutembea na Sime maana wamekua na mambo ya kifala sana..kuna mmoja alikua kalewa anatishia watu hovyohovyo kwenye daladala halafu anatukana matusi ya hatari. Sime waruhusiwe wakiwa porini sio mijini
 
Mtoto-1024x768.jpg
JESHI la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kereto Likoko (Mmasai) kwa madai ya kumuua Mwanafunzi Samson Conrad aliyekuwa akiyesoma katika Chuo cha Faraja kwa kumkata na sime shingoni kwa madai ya kushindwa kumlipa fedha ya pete ambayo alikuwa akiuza.





Akizungumza jana Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.





“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,” amesema Kamanda Issah.
 
Back
Top Bottom