Auawa akiwatoroka polisi waliokuwa wakimkagua

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKAZI mmoja wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na wananchi baada ya kuwakimbia polisi waliokuwa wamekwenda nyumbani kwake kumpekua.

Upekuzi huo ulikuwa unafanywa baada ya kuwapo kwa tetesi kwamba anamiliki silaha anayoitumia kufanikisha vitendo vya uhalifu.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Barlow alisema kwamba tukio hilo litokea eneo la Ushirika majira ya saa 11 jioni.

Akizungumzia tukio hilo kamanda huyo wa polisi alisema kwamba wananchi walitoa taarifa polisi kuwa kuna mkazi mmoja wa maeneo ya Ushirika mjini humo ana silaha nyumbani kwake aina ya SMG.

Alisema kwamba baada ya polisi kuzifanyia kazi taarifa hizo walienda nyumbani kwa mtuhumiwa aitwaye Athumani Shabani kwa ajili ya upekuzi.

Alieleza wakati polisi wanafanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa alifanikiwa kuwatoroka na kukimbia ambapo alikimbizwa na wananchi waliomkamata na kisha kumpa kipigo hadi kutoa uhai wake .

Kamanda Barlow alisema kwamba upekuzi huo wa polisi ulifanikisha kukuta bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1976720709 pamoja na risasi 28.
 
Maana ndo kama hao wamehukumiwa 60 yrs in jail, Lakini kesho yake anakamatwa kwenye ujambazi
Tena ana bahati wananchi wangepata fursa kidogo tuu wangemtoa uhai nyambafuu
 
Back
Top Bottom