Aua mke kwa kisu, naye ajiua papo hapo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,690
2,000
Aua mke kwa kisu, naye ajiua papo hapo

Imeandikwa na Nashon Kennedy, Mwanza; Tarehe: 11th December 2010 @ 23:15

IKIWA ni wiki moja tu imepita baada ya Tanzania kuadhimisha siku 16 za harakati za kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake, bado vitendo vya ukatili kupigwa na kuuawa vimeendelea kusikika.

Hali hiyo imemfanya Chupasi Kabanikilo(40), mkazi wa Kijiji cha Ibondo wilayani Sengerema aliyemuua mkewe, Sikitu Lukanda(36) ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho kumchoma kisu tumboni hadi kufa na kisha yeye mwenyewe kujiua papo hapo katika ugomvi unaodaiwa kuwa chanzo chake ni wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro lilitokea Desemba 7 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika Kijiji cha Ibondo katika Kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema.

Sirro alisema kuwa tukio hilo lilitokea baada ya Kabanikilo kuwatuma watoto wake wawili dukani ili wakamnunulie mafuta ya kula.

Lakini taarifa zinasema mara baada ya kuwatuma watoto wale dukani, aliingia ndani alimokuwa mkewe na kujifungia kwa ndani na kisha kuanza kumshambulia na kumuua mkewe na kisha naye kuamua kujichoma kisu tumboni na shingoni na kufariki dunia.

Kwa mujibu wa Kamanda Sirro watoto waliporudi nyumbani walishindwa kuingia ndani kwa vile mlango ulikuwa umefungwa huku wakisia sauti ya baba yao akikoroma hali iliyowashtua na kuamua kwenda kutoa taarifa kwa majirani.

Majirani walilazimika kubomoa mlango ili waweze kuingia ndani na baada ya mlango kubomolewa, waliwakuta wanandoa hao tayari wamekwishafariki dunia ambapo Kamanda Sirro alisema chanzo cha awali cha mauaji hayo kinaonesha kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Aliongeza kwamba Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi huo na kusisitiza kuwa ni tukio la kikatili lililofanywa katika jamii ambalo halina budi kufuatiliwa kwa ukaribu zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom