kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,293
- 12,593
Tanzania tangu ipate uhuru wake ilijihusisha na siasa za Afrika zaidi kiasi cha kukosa nafasi ya kuhusika na maendeleo yake kikamilifu, tulifanya hivyo kwa kuongozwa na fikra za utu, uafrika na umoja. Tanzania ilikuwa na jeshi kubwa kwaajili ya kujilinda wenyewe kutokana na maadui iliyokuwa inajitengenezea kutokana na kuunga mkono juhudi za nchi nyingine zilizotaka kujikomboa dhidi ya wakoloni wao wenye nguvu kama Wareno na Makaburu na kuwasaidia wengine kijeshi.
Tuliamua kuisadia Afrika bila ya kutarajia ujira wowote kiasi cha kupitwa kiuchumi na zile nchi tulizozisaidia kujikomboa. Duniani kote nchi zenye majeshi makubwa na yenye nguvu kama sisi huwa wanayatumia majeshi yao katika kupora mali za nchi nyingine ambazo zitatumika kuliendesha na kulijenga jeshi na nchi, lakini kwetu sisi majeshi yetu yanategemea kuendeshwa kwa kodi za wananchi wenyewe, hayakodishwi wala kutumika kupora mali za wengine. Hii inasababisha gharama za kuyaendesha majeshi yetu iwe kubwa sana.
Hata Marekani au Rwanda huwa wana nguvu kijeshi lakini majeshi yao ni sehemu ya uchumi wao, hivyo yanajiendesha yenyewe na kuendesha uchumi tofauti na sisi. Ni vizuri sasa Afrika ikatusamehe na sisi kidogo kwa muda wakati huu tunarekebisha uchumi wetu chini ya kamanda mpya Rais JPM. Tuachane na ule ukiranja wa Afrika tulioufanya tangu tupate uhuru wetu ambao umetujengea heshima na sifa lakini kutubakiza masikini wa kutupwa.
Hebu watuache kidogo tupumue ili turekebishe uchumi wetu. Tusione aibu kulipa kodi kikamilifu maana hata wazungu wanafanya hivyohivyo kwenye kujenga uchumi wao. Kinachotakiwa hapa ni serikali kutenga ardhi kuuuubwa sana na kuwapa wawekezaji wakubwa watakaolima na kufuga kwa njia za kisasa na kutoa ajira nyingi kwa wananchi watakaoyahudumia mashamba, mazao na viwanda vya kuchakata mazao ya shambani, mifugo na uvuvi mkubwa.
Hii itapanua wigo wa kodi badala ya kila mtu kulima nusu eka ya mananasi, nusu eka mihogo, nusu eka mbaazi. Majeshi yetu yasiwe ya kwenda kupora mali za wengine lakini yawe ya uzalishaji mali mkubwa wakati yanafanyakazi ya kuilinda nchi.
Majeshi yetu yawe mstari wa mbele kuwa na mashamba makubwa ya kujilisha yenyewe na taifa, viwanda, hospitali kubwa, n.k kuliko ilivyo sasa hata jeshi la magereza lenye wafungwa linapewa chakula na uniform kwa kutumia kodi za wananchi.