AU si kwa Waafrika wote -Hoja. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AU si kwa Waafrika wote -Hoja.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Apr 17, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna sababu ya kuwashirikisha wapinzani katika jumuia ya Nchi za Afrika AU ,kama vile katika mashirikisho ya Ulaya ambapo vyama wapinzani hupata nafasi ya kuweka wajumbe .
  Kwa ufupi vyama vyote vyenye wabunge jupewa nafasi ya kutoa wabunge watatu kuwepo katika ushirika huo,
  Hivyo hapa Afrika kunahitajika kuwemo kwa wabunge kutoka vyama vya upinzani kwa nchi zilizomo katika umoja huo ,ile tabia ya kushirikisha wabunge wa chama kinachotawala peke yake ni ya ukandamizaji na hauwezi umoja huu ukaonekana kama ni wa Afrika nzima bali ni wa wachache tu ambao kumekuwepo na tabia ya kulindana au kutumia umoja huo kuukandamiza upinzani.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naendeleza hoja ya umuhimu wa kuwepo kwa wawakilishi kutoka vyama vya upinzani ambayo vinawabunge katika bunge la Nchi kuweza kuruhusiwa kuwakilisha katika Umoja wa nchi huru za Afrika.
  Kama hili halikufanyiwa marekebisho basi vyama hivi navyo vinaweza kuanzisha umoja wao nao ukawa na jina lile lile la Umoja wa Afrika wa Vyama vya Upinzani na vikaweza kutoa ushirikiano mzuri tu wakiwa na lengo la kuanzisha umoja wa nchi za Afrika ambao utawashirikisha wadau wote ,vyama vilivyomo kwenye madaraka na vyama vya upinzani ambayo vina mbunge ndani ya bunge la nchi yao.Hata katika hii Jumuia ya East Afrika ni lazima wawemo wabunge kutoka vyama vya Upinzani ili kushirikisha wananchi wote wanapokuwa hawa hawamo inamaana wametengwa.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kweli ki mantiki inabdi wabunge wa upinzani washirikishwe, la si hivyo utakuwa ni umoja wa vyama tawala vya Afrika.
  kwa sababu nchi nyingi za Afrika bado vyama tawala vinakaa kwa muda mrefu japo kuwa upinzani umekuwa na unashinda kuongoza nchi hizo
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sijui unamaanisha nini unaposema kushirikisha wapinzani katika umoja wa afrika maana hicho ni chombo kikubwa chenye organisations nyingi. Ninafahamu kwa mfano kwenye Bunge la Afrika, kati ya wabunge wanaoiwakilisha Tanzania, yumo mpinzani
   
Loading...