Atupwa lupango kwa kudai Mwinyi, Mkapa wameuza nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atupwa lupango kwa kudai Mwinyi, Mkapa wameuza nchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukundo, Jul 28, 2009.

 1. L

  Lukundo Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raia wa Irak kizimbani kwa kuwakashifu Mwinyi, Mkapa


  [​IMG]
  Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

  Raia wa Irak, Anney Anney (59), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam kujibu shtaka la kutoa maneno ya uchochezi yenye hisia za kusababisha uvunjifu wa amani. Anadaiwa kutoa maeno hayo wakati akiwakashifu viongozi wastaafu wa Tanzania.

  Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka na Mrakibu wa Polisi, Naima Mwanga, mbele ya Hakimu Samwel Maweda.

  Mrakibu Mwanga alidai kuwa Julai 23, mwaka huu katika eneo la Ikulu jijini Dar es Salaam, na kuanza kumshutumu Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akisema aliuza Azimio la Arusha.

  Aliendelea kudai kuwa kana kwamba haitoshi, mshtakiwa huyo alimshutumu Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisema aliuza mashirika ya umma na ardhi ya wananchi wa Tanzania kwa waarabu na wazungu bila kujali utu na utaifa.

  Mwendesha mashataka huyo aliongeza kudai kuwa mshtakiwa huyo baada ya kuwakashifu viongozi hao, alihitimisha kwa kutoa maneno ambayo pia yanaweza kusababisha vurugu na uchochezi nchini pale alisema: “Udumu ujamaa na kujitegemeana, zidumu fikra za Mwalimu Nyerere."

  Vilevile Mwanga alidai mshtakiwa huyo katika matamshi yake alidai Rais Jakaya Kikwete amekuwa analinda ardhi ya Watanzania, utaifa na uzalendo.

  Mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 10, mwaka huu.
   
  Last edited by a moderator: Jul 28, 2009
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Haya wana ukumbi mashitaka haya yanasimama?
   
 3. L

  Lukundo Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je inawezekana huyu akawa ameandaliwa zengwe, au akwa chizi fulani anayetafuta populality, au ndo watu wale wanaoona wanyonge wanadhulumiwa haki na kuamua kujitoa muhanga, lakini baadaye wanakutana na tawala dhalimu zinazosema tupo huru, lakini kimantiki tukiwa watumwa katika nchi zetu wenyewe.
   
 4. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ...ni kichekesho au?
   
 5. C

  Chakarota Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona huyu angefaa hata kua bungeni kwa upande mmoja, lakini pia nahisi ameshtakiwa kwa kuwakashif aliowapongeza kwani hawastahiki. Wote tangu waliopita mpaka wa sasa wapo kwa maslah yao tu.
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi nashindwa kuelewa hebu nisaidie hapo.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ni kweli basi huu utakuwa mwanzo wa uongo ambao utapelekea kuwatisha na kuwakamata WaTz walioamua kuwatolea uvivu viongozi vihio ,wanaobabaisha kwenye majukwaa na uongozi wao ni wa kutiliwa mashaka.
   
 8. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna kitu hakipo sawa hapa, je hii ndo ile kesi ya yule aliyekamatwa ikulu kwa kuiba ua? Au ni kesi nyingine tofauti.
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  mhhh... mbona naona haijakaa sawa hii?

  Raia wa iraq akiwa maeneo ya ikuli kuwakashifu maraisi wa zamani!!!!!

  je ni resident wa hapa au? what made him to do that na alikuwa katika situation gani?

  Nadhani mwandishi alipaswa kuongezea infos.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Labda Muiraq wa kule Arusha.
   
 11. K

  Kalimanzira Senior Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi zenye demokrasis ya kweli, sioni ubaya wa mtu huyu! Alitimiza haki yake ya kidemokrasia kutoa mawazo yake ambayo kila kukicha wanasiasa na wanazuoni kwa nyakati mbalimbali wamekuwa wakiyatumia. ...."ZIDUMU FIKRA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA"
   
 12. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  My my my, hii sasa ni udhalilishaji ya taaluma ya uendesha mashtaka. This makes me question the education of the persons who prepared and the one who read the charges. Nyerere atakuwa aligeuka huko kaburini. Mamlaka za juu zijisafishe na hii ambayo naweza kuiita kashfa ya mwaka. Tunajua siasa ya ujamaa na kujitegemea wameshaitupilia mbali lakini hii ya ku-criminalize kutamka siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kwenda mbali mno. Talking of framed charges this is a vivid example.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa mtaji huu wengi wetu hapa JF pia tunapaswa kuswekwa lupango. Aliyoyasema mtuhumiwa yamo katika mioyo ya Watanzania wengi, me included.
   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mimi hata sioni kosa lake!!!
   
 15. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Raia wa Iraq?

  Jamaa ni mzalendo hata kuliko nyani ngabu wa JF Ville Forest Reserve!:D

  Jamani hao waandishi mbona hawakutufafanulia
  Miandishi Ndivo Ilivyo(sic)
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Junius...! Kosa lake ndilo ilo aliloshtakiwa nalo. Kwa kusema hayo aliyo yasema ndio kosa lake...!

  Unajuwa bro haya makosa mengine badala ya mtu kukasirika au kusikitika unaweza kuishia kucheka tu mbele ya hakimu. Wakakosa kuthibitisha kosa wakaishia kukufunga kwa kudharau mahakama.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Upuuzi mtupu. Vyombo vya serikali yetu havijui mambo ya kushughulikia
   
 18. D

  Domisianus Senior Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari, sasa amefunguliwa mashitaka ya kukashifu au kusema ukweli?
  Mbona alisema lidumu azimio la Arusha na ujamaa wa kujitegeme, nalo ni kosa?
  nadhani mwendesha mashitaka wa serikali ndo anunda hilo zengwe la kuwazindua watanzania jinsi hao viongozi walivyokuwa, hakuna mantiki yoyote ya kumshitaki huyo Mraik,je Kumsifia Nyerere na Kikwete nalo ni shitaka la uchochozi?
  Shall we make it kwa mtindo huu wa kuangalia mambo ya kipuuzi na kushindwa kuangalia vitu vya maana?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Huyo mtu ni Muiraqw!... I think.
   
 20. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ...........wanazisahau kesi za E.P.A
  wanasahau kutuambia hatma ya wale ''tuner fish''
  wanachelewesha kesi za kina mramba!
  WANALIONA HILI?!
   
Loading...