Atupwa jela miaka 7 kwa kumkata mkewe sehemu za siri ili apate mali

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkazi wa Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe kwa imani za kishirikina ili apate mali.

Hakimu Joctan Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imeridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Hakimu Rushwela alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho kwa wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina.

Awali wakili wa Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa jadi, walitenda kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika eneo la Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.

Wakati wa tukio hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata Sh5milioni.

Alidai baada ya kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza ukatili huo.

Alidai baada ya kunywa pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri mkewe na kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka.

Alidai kwa mujibu wa mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.
 
Kwenye sehemu ya siri ya mwanamke kuna shimo, mashavu, kaharage na msitu wa nywele, sasa kilichokatwa hasa ni nini?
 
Back
Top Bottom