Atupwa jela miaka 30 kwa kukutwa na meno ya tembo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193


MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Amani Rashid (30), kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada kupatikana na hatia ya kumiliki meno nane ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 120 kinyume cha sheria.

Mahakama hiyo pia imemwamuru mshtakiwa huyo kuilipa serikali kiasi cha Sh bilioni 1.2, ikiwa ni fidia ya kuua tembo hao. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Januari mosi, mwaka huu kijijini Nsenkwa wilayani Mlele.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa, alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Wankyo Simon kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo.

Tengwa alisema ametoa hukumu hiyo, ili iwe fundisho kwa mshitakiwa mwenyewe na wengine wanaojihusisha na ujangili wa meno ya tembo.

chanzo.Atupwa jela miaka 30 kwa kukutwa na meno ya tembo
 
Back
Top Bottom