Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2017 kwa mara ya kwanza ilifikishwa mahakamani hapo Januari 16 na upande wa Jamhuri ulileta mashahidi wanne ambao walitoa ushahidi wao na hatimaye hukumu kusomwa leo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Chunya, Osmund Ngatunga alisema ushahidi wa daktari na mtoto ndio unamtia hatiani mshtakiwa huyo.
Alisema mahakama inamtia hatiani na kumpeleka jela maisha kutokana na vitendo hivyo kudhalilisha sana watoto licha ya kuwapo sheria kali.
Chanzo: Mwananchi