Luther House posta ndani ya kanisa la KKKT Azania Front wana ofisi zao (ofisi za mana). Hapo unaweza pata vitabu pamoja na cd za mafundisho ya mwl. Christopher Mwakasege.
Asante kaka/dada
Luther House posta ndani ya kanisa la KKKT Azania Front wana ofisi zao (ofisi za mana). Hapo unaweza pata vitabu pamoja na cd za mafundisho ya mwl. Christopher Mwakasege.
Natoaa wito kwa Wanazuoni, Wasomi na Wanaharakati ndani na nje ya Tanzania kwa kutambua mchango wa Mwl, hakika anastahili Ph.D ya heshima.
Upo wapi we we!!
Km in dar pale Luther house,makao makuu ya kkkt kuna ofisi yake utapata vitabu na CD/dvd.
Mkutano wake wa mwaka jana morogoro ilikuwa kipindi cha mvua ile siku ya 1 tu Jamaa akaomba samahani kwa wakazi wa moro wanaohitaji mvua maana Mungu anahitaji watu waje ktk mkutano hivyo alipiga maombi ya kufunga mvua na ndivyo ilivokuwa kwa siku zote za mkutano hakukuwa na mvua wala manyunyu. Siku anamaliza mkutano akashukuru na kutangaza "kesho tukimaliza kukusanya virago vyetu tutaruhusu mvua iendelee" lahaula! kama kawa kesho yake mida ya alasiri mvua ikarejea. I was shocked.
Yes uko sahihi mkuu
Same to dar, last year,mkutano WA mwezi WA 3,kulikuwa kuna mvua sana , akaomba na mvua ika stop!
Mpaka tulipomaliza mkutano.
Hawa ndo watumishi walioketi kwenye kiti cha enzi na Yesu!
Wana mamlaka,na wakisema jambo linakuwa!
Daaa minaunga mkono coz kunakitabu flani ameandika cha mzaliwa wakwanza kama lango"
Hikitabu kimenifumbua sana macho sanaa..mimi kama mzaliwa wakwanza.
Dada with all due respect.. . . . .huu ukame wa mwaka huu ya hauoni, tishio la njaa we hulioni au uko mbali na kilimo??!!!
Au mpaka awe ana hoja yake ndio anazuia na kuruhusu mvua???!!
Na ambao si wazaliwa wa kwanza kinawasaidieaje hicho kitabu?
Hahaaa mzima!!
Kwani yeye huwa anazuia mpaka njaa itokee nop!
Yeye huwa anazuia kwa siku anazokua na mkutano na ni siku 7 , then baada ya hapo mvua inaendelea kana kawaida.
BTW angalia huko kulikotokea maafa kwa ajili ya mvua!!
Mvua imezidi imeharibu mazao!
mm nadhani Ambilikile Masapile (babu wa loliondo) ndiye anayestahili Phd katika category ya degree without school. Wengi watanishangaa lakn i stand to be correct!
Elimu na status ya Mwakasege kwenye uchumi wa kimataifa kwa hapa Tanzania hana mbadala na kama haumjui Mwakasege wala usimseme waulize wanaomfahamu watakwambia.Msipende vya kupewapewa kama anataka phd aingie class apige kitabu, izo degree za kupewa sio nzuri wala hazibadilishi heshima ya mtu. Angalia kina Kikwete wamepewa ngapi na bado anaonekana wa kawaida tu na baadhi ya watu wakigoma kumwita profesa. Yesu alifundisha sana lakini hakuomba degree na bado heshima yake ni kubwa, Mwl. Nyerere hadi anaongoza taifa hili kwa uadilifu mkubwa hadi leo anaheshimika na kila mtu bado aliitwa Mwalimu. Mi nadhani Mchungaji Mwakasege inafaa sana kuliko Profesa Mwakasege unless atakaposoma na kuwa prof. ndipo title yake itabadilika coz tutakuwa hatuna jinsi kama tuwaitavyo kina Prof. Lipumba, Prof. Mwandosya na ni maprofesa kweli