Atunge Sera, Atekeleze kisha Ajihoji

kila siku nashangaa wengi wetu hapa tunadhani kutoa maoni ya namna ya kusolve matatizo Tanzania ndiyo suluhisho la matatizo yetu. Tunajidanganya.

Suluhisho namba moja ni sisi kutwa madaraka na kutekeleza mawazo yetu. Toa maoni namna ya kujipanga ili kutwaa Ubunge siyo namna mbunge wako awezavyo kutatua matatizo jimboni mwenu.

Mawazo kwamba tutoe maoni yana mwelekeo wa kuendelea kuwaenzi viongozi walishindwa kazi walioko madarakani. Mawazo hayo yana nia ya kudumisha utawala wa viongozi walioshindwa na wanao jivisha vilemba zaidi ya vitatu ili kulinda himaya zao za uovu.

Viongozi waliopo wameshindwa wao na utaratibu wao.
Samaki ameoza lake ni jalala friji au ndani ya chungu si mahali pake.

Vilemba 7 vya madaraka ni Udikteta.
 
Hili ni tatizo tena kubwa kabisa haiwezekana mtu huyo mmoja atunge sera, azitekeleze yeye mwenyewe na pia ajihoji mwenyewe ktk kuzitekeleza hizo sera huo ni uroho

mbaya zaidi ktk kila kofia anafungu lake la pesa kwanini asijenge gorofa Uingereza? tena atalipa kodi Uingereza, atanufaisha Uingereza na Uingereza nao wajisifu tunatoa misaada Tanzania?
 
Hakuna ajengae UK kwa mishahara 3.
UK wanajenga kwa Pesa ya Ufisadi.

Dawa ni kuwapandia huko huko juu,ukisubiri washuke utaoza.
 
Back
Top Bottom