Atumia Tsh. Milioni 50 Kwaajili ya Harusi ya Mbwa Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atumia Tsh. Milioni 50 Kwaajili ya Harusi ya Mbwa Wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ametumia paundi 20,000 (Karibia Tsh. Milioni 50) kwaajili ya kuandaa harusi ya kifahari na gauni la harusi la kifahari kwaajili ya mbwa wake wa kike.
  Louise Harris mwenye umri wa miaka 32 alitumbua paundi 20,000 kwaajili ya harusi ya kifahari ya mbwa wake wa kike anayeitwa Lola ambaye aliozeshwa kwa mbwa anayeshikilia taji la mbwa mwenye sura mbaya kuliko wote Uingereza anayejulikana kwa jina la Mugly.

  Sherehe hiyo ya kifahari ilihudhuriwa na watu 80 ambapo gharama za kuukodisha ukumbi kwaajili ya harusi hiyo ya aina yake ilikuwa paundi 2,500.

  Mbwa Lola alivalishwa gauni la harusi lenye thamani ya paundi 1,000 ambalo lilitengenezwa maalumu kwaajili yake na duka la vito vya thamani la Swarovski.

  Mbwa Lola pia alivalishwa cheni shingoni na kikuku mguuni ambavyo vyote viligharimu paundi 750.

  Maua ya kupamba ukumbi wa harusi yaligharimu paundi 1,000 wakati wapambaji wa ukumbi walilipwa kitita cha paundi 3,000.

  Miongoni mwa gharama za harusi hiyo ni mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama kwenye harusi hiyo ambao walilipwa paundi 400, madansa na wacheza shoo waliolipwa paundi 500, gari la kukodisha aina ya Bentley kwaajili ya maharusi liligharimu paundi 500 wakati Dj alilipwa paundi 500.

  "Mbwa wangu ni fahari yangu na furaha yangu ni kuwafanyia kila kilicho kizuri", alisema bi Harris.

  Bi Harris alisema kuwa furaha yake imetimia kwa kuona Lola amefanikiwa kupata mwenza wake wa maisha ambaye amekuwa akicheza naye wakati wote.

  5591202.jpg
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hizi ni kufuru...
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaa wangekua na huruma hizo pesa wangesaidia maskini tu naumia sana na yule dogo wa kigoma anaekosa pesa laki 7 na 50 kwaaajili ya kufanyiwa oparesheni pale kcmc kwaajili ya kumtengenezea tundu la haja kubwa!
   
 4. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,545
  Likes Received: 1,591
  Trophy Points: 280
  kazi kwelikweli.
   
 5. r

  rubii JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2015
  Joined: Feb 22, 2015
  Messages: 11,320
  Likes Received: 9,931
  Trophy Points: 280
  Mi nimekuja mbio nikajua madam mwafurani
   
 6. Illovo

  Illovo JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2015
  Joined: Feb 21, 2015
  Messages: 2,305
  Likes Received: 417
  Trophy Points: 180
  hapo ni sawa tu, na halali yake kwa sbb iyo ni "devil ceremony" suppopted by lucifer as it recieve glory
   
Loading...