Atumia Staili za Mike Tyson Kunyofoa Sikio la Mpenzi Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atumia Staili za Mike Tyson Kunyofoa Sikio la Mpenzi Wake

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mbonea, Sep 25, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Stephanie alivyo sasa na sikio lake lililonyofolewa kulia
  Friday, September 25, 2009 8:01 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani mwenye wivu wa ajabu baada ya mpenzi wake kuamua kuvunja uhusiano wao, kwanza alimshushia kipigo cha nguvu na kisha kutumia staili ya Mike Tyson kwa kumng'ata sikio lake na kunyofoa kipande cha sikio lake


  Mike J. mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi nchini Ujerumani alitumia staili ya wajina wake Mike Tyson kumng'ata sikio mpenzi wake aliyeamua kuvunja uhusiano wao.

  Mike mwenye umri wa miaka 29 alipata hasira za ajabu baada ya mpenzi wake aliyetajwa kwa jina moja la Stephanie mwenye umri wa miaka 19, mwanafunzi wa sekondari nchini humo kumtamkia wazi kuwa hataki kuendelea na uhusiano wao wa kimapenzi wa miaka miwili.

  "Mike ana wivu wa ajabu, muda mfupi baada ya kutamka maneno mazuri ya kimapenzi hubadilika ghafla na kuanza kunipiga, baada ya kubusiana naye huanza kuonyesha hasira zake", alisema Stephanie anayetoka mji wa Jessen.

  "Baada ya kushauriana na rafiki zangu niliamua kuvunja uhusiano wetu" aliendelea kusema Stephanie.

  Stephanie alisema kwamba baada ya kumtamkia wazi Mike kuwa hataki kuendelea na uhusiano wao wa kimapenzi, Mike hakuridhia na alimfuata siku hiyo hiyo nyumbani kwake mida ya usiku.

  "Aliponigongea mlango nilidhani anakuja tuongee naye kuhusiana na uhusiano wetu lakini alipoingia ndani moja kwa moja alinirukia na kunipiga na kisha kuning'ata sikio na kunyofoa kipande cha sikio langu na kisha kukitema chini, kila sehemu ilijaa damu" alisema Stephanie.

  Stephanie alidokeza kwamba alifanikiwa kukipata kipande cha sikio lake kilichonyofolewa lakini madaktari walishindwa kukiunga tena.

  Mike alifikishwa mahakamani na alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja pamoja na kulipa faini ya euro 1600.

  Mike alipinga hukumu hiyo na alidai atakata rufaa.

  Tukio hili limekumbushia tukio la bingwa wa zamani wa ndondi Mike Tyson kumng'ata sikio Evander Holyfield wakati wa pambano lao lililofanyika juni 28 mwaka 1997.  Source: Germany Newspapers
   
 2. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kivumbi hiko
   
Loading...