Atuhumiwa kuua mke na kumzika, juu ya shimo apanda mpunga

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mkazi wa Tandahimba mkoani Mtwara, Shaibu Kauselela anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua mkewe na kitu Kizito kinachodhaniwa kuwa na ncha kali na baadaye kumzika kwenye shamba na kupanda mpunga ili kupoteza ushahidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa limetokea Februari 28, mwaka huu, katika kijiji cha Lipalwe mkoani humo.

Alisema kuwa mwanamume huyo alifanya unyama wa mauaji hayo ya mkewe Amina Mtausi (40) kwa kutumia kitu kinachodaiwa kuwa na ncha kali.

Alieleza baada ya kutekeleza mauaji hayo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuufukia katika shimo shambani kwao kisha kuchukua mpunga na kuupanda juu ya shimo hilo.

Pia, baada ya kutekeleza azma yake alitoweka kusiko kujulikana kutokana na kuhofia kukamatwa na vyombo vya sheria na chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.

ACP Katembo alisema tukio hilo limegundulika juzi baada ya mdogo wa mtuhumiwa huyo, Omari Saidi, alipokuwa akienda kisimani kuchota maji katika shamba hilo na kubaini harufu isiyo ya kawaida.

Alisema alipofuatilia kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikitoa harufu na aliona baadhi ya viungo vya marehemu huku sehemu ya mwili ukiwa umefukiwa ndani ya shimo.

ACP Katembo alisema, Saidi alitoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo kwa kina zaidi.

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara lilifika katika eneo hilo la tukio wakiambatana na madaktari kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu wa mwili huo na hatimaye baada ya vipimo ulibainika kuwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kisogoni na kutokwa na damu iliyosababisha kupoteza maisha.

Alisema Jeshi la Polisi bado linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo ili afikishwe katika mahakama kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili za mauaji.


Source: Nipashe
 
Aisee watu iko na roho ngumu, kupiga hadi kuua tena mkeo.

Nafikiri akili ya mtu inakua haiko sawa.
 
Ndugu zetu wakristo mnakwama wapi au ndio hyo kufa na kuzikana inawaponza mkichokana si kila mtu na hamsini zake tu.
 
Mara nyingi muuaji hata ajifiche vipi mambo huwa hadharani tu. Inaweza kuwa miaka kadhaa lakini itajulikana tu
 
Back
Top Bottom