Attn:Avatar ya Maxence itumike na kila Mwana Jamii Forum Siku atakayopanda Kizimbani

SHANTI

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
296
365
Ndugu wana JF,

Ningependa kutoa wito kwa kila mwenye akaunti humu JF,instagram,twitter na facebook na WhatsApp kubadali profile picture au Avatar yake kila siku ambayo mwanzilishi wetu wa jamii forum Bw. Maxence Melo atakapokuwa anapandishwa kizimbani ikiwa ni ishara ya kuonesha kwamba tupo naye kwenye majonzi mazito.
Ikumbukwe pia kutokana na udogo wa chumba mahakama ,na pia baadhi ya member kwa namna moja au nyingine hawatoweza kuhudhuria kesi hii basi sio vibaya kubadili profile picha yako ili watu waliokuzoea wajiulize umemuweka nani? Jinsi wanavyojiuliza ndivyo ujumbe utasambaa kwa watu wengi na kuwafanya wasiomjua wamjue kuanzia siku hiyo walipoiona picha yake kwako.
Angalizo unapotumia picha yake kwenye kurasa za facebook, instagram na twitter usisahau hashtag yetu ile.
Karibuni kwa kila mwenye mchango wa kuboresha wazo hili
 
hata mimi niliwaza hivyo nikakosa njia ya kuyawakilisha....Ndivyo tutakavyofanya..
 
Kuweka picha yake kwenye Avatar zetu itasaidia nini?

Mbona wewe hujaweka?

Hatutaki kumwona kwenye Avatar tunataka kumwona na kufahamu kuwa yupo huru kama mtanzania, analala kwake na kuishi na familia yake.
 
Nasikia kuna wana JF / wanachadema wamewnda mahakamani na T shirt za chadema.
Hilo ni kosa , ni kama mnamuingiza Max kesi yake iwe ya kisiasa zaidi ili hali Max alikuwa hana chama na hajaonyesha msimamo wake wa kisiasa.
Max yeye alikuwa nyundo ni nyundo na msumari ni msumari.
Sasa mkienda na t shirt za chadema mnaharibu.
 
Good,
Ila kuna watu hawatakuelewa. Kuna mmoja nilimquote comment yake na kumwambia asihusishe Melo na chadema (pia chama chochote) yeye akanitapikia nyongo.
 
Good,
Ila kuna watu hawatakuelewa. Kuna mmoja nilimquote comment yake na kumwambia asihusishe Melo na chadema (pia chama chochote) yeye akanitapikia nyongo.
Daah! Pole sana mkuu ila mdogo mdogo wataelewa.
Ila seriously mimi nitasimama kwenye viunga vya mahakamani.
Ukija na t shirt yako ya Chadema nitakurudisha.
Kesi ya Maxence sio ya kichama
 
Back
Top Bottom