Attention Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Wanafuzi(HESLB)

HKiboka

Member
Feb 6, 2007
13
1
Watanzania masikini wasiwe na wasiwasi kwani sisi watoto wao kamwe hatutakubali kunyanyaswa kwa sababu ya umasikini wetu, tumeanza na tutaendelea hadi dakika ya mwisho pale haki itakaposhinda dhulma.
Tunabaguliwa na wanasiasa kwa kuwatumia wasomi vibaraka na wanaotaka kujipendekeza ili wapewe madaraka.
Mkopo ni haki yetu ya kisheria kwani tuna vigezo kwa mujibu wa sheria na sisi kutodai ni sawa na kukubali dhulma itawale! tutadai mpaka kieleweke kamwe hatuwezi kupumbazika na ahadi za kisiasa zisizo na muda maalum wa utekelezaji. Kama tukishindwa kujitetea hata sisi wenyewe ni dhahiri kuwa hatutaweza kuitetea jamii yetu fukara pindi tutakapopata kazi. Kitu cha msingi ni wazazi kutuunga mkono si kutuona wahunu na wakorofi kama watuitavyo wanasiasa na wasomi vibaraka. Wazazi wanalipa kodi ili sote tupate huduma na si kugharamia safari na posho za viongozi ndumilakuwili waliowadanganya watanzania kuwa wataleta maisha bora kwa kila mmoja wao kitu kilchogeuka ndoto.
TUNAPASWA KUJIFUNZA KWA HILO!
 
Bodi ya mikopo elimu ya juu yaja na vigezo vipya

2007-05-26 10:27:41
Na Mwandishi Wetu


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB), imetangaza vigezo vipya vitakavyotumika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambavyo vitazingatia uwezo wa kiuchumi wa waombaji.

Kwa mujibu wa tangazo la HELSB lililotolewa kwenye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, utaratibu huo mpya wa mikopo, utaanza kutumika mwaka wa masomo wa 2007/08.

Chini ya utaratibu huo, waombaji wamegawanywa katika makundi matano yaani A, B, C, D, E na F.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa, wanafunzi katika A watapata asilimia 100 ya mkopo, B asilimia 80 na waombaji wa kundi C, watapewa asilimia 60.

Iliongeza kuwa, waombaji katika kundi D, watalipiwa kwa asilimia 40, E watapewa asilimia 20 na kundi F ambao hawatakopeshwa hata senti.

Wanafunzi watakaokubaliwa mikopo hiyo watalipiwa gharama kadhaa ikiwemo mafunzo, posho ya chakula, malazi, tahadhari, tiba, vitabu na mafunzo ya vitendo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kupewa mkopo kutategemea uchambuzi na mchujo utakaofanywa ili kuona hali ya kiuchumi ya mwombaji, wazazi ama walezi wake na hivyo mikopo itatofautiana kutoka mwanafunzi mmoja hadi mwingine.

Utaoaji wa mikopo utafanywa kwa kuchunguza waombaji kwa utaratibu utakaotolewa na HELSB ambao hata hivyo haukufafanuliwa.

Aidha, Bodi imewaonya waombaji watakaobainika kutoa taarifa za uongo ama kwa maandishi au mazungumzo ambayo yataathiri taratibu za maombi ya mkopo, kuwa watapewa adhabu ya kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya Sh. milioni 1.5.

Kadhalika, ilisema iwapo mwombaji atakuwa amepewa mkopo kutokana na udanganyifu, Bodi itauzuia na kuufuta mara moja na mhusika kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesisitiza kuwa, utaratibu wa wanafunzi wa Kidato cha Sita waliofaulu Daraja la Kwanza kwa wanaume na Daraja la Kwanza na la Pili kwa wanawake, utaendelea kutumika katika utoaji wa mikopo hiyo.

Ilifafanua kuwa, kipaumbele kitatolewa kwa wanafunzi wanaosomea kozi za Tiba, Sayansi, Kilimo, Ualimu, Uhandisi na Teknolojia.

SOURCE: Nipashe
Wadau hii mnaiona je? linatekelezeka? je mambo kama haya kuwepo na vitambulisho vya uraia vyenye details za watu si ingerahisisha? Hofu yangu itakuwa ngumu kwa walengwa kupata mikopo kama ilivyokusudiwa.
 
Bodi ya mikopo hata ije na vigezo vya aina gani itakuwa ni vigumu kubadilika kama mambo ya msingi hayaguswi:

1. Wale waliosoma kwa mikopo kuna haja ya kuwekewa utaratibu warudishe. Ni rahisi bila hata hivyo vitambulisho vya taifa inawezekana. Kwa mfano ikiwekwa sheria/kanuni kwamba kila mwajiri wa Tanzania anaeajiri 'graduate' wa vyuo vikuu lazima afanye makato maalum kwa mfanyakazi huyo yatakayopelekwa TRA/MAMLAKA MPYA YA KUKUSANYA FEDHA HIZI ZA MALIPO YA MKOPO na mlipaji awe ametia saini kabisa kukubali kisheria kwamba analipa mkopo wake. Kiwe ni kiwango kidogo kinachoendana na mshahara wa mhusika.

2. Ikifanyika hivyo manake ni kuwa kutakuwa na hela toka kwa wananchi wenyewe waliowahi kuchukua mkopo, ambao watakuwa wanafadhili wanafunzi wengine. Kutakuwa na mzunguko maalum wa fedha zinazolipwa na kukopesha wanafunzi wengine. Hii ndio ilivyo kwa STUDENT LOANS COMPANY hapa Uingereza.

3. Nijuavyo ni kuwa tuna wanafunzi kidogo sana [tunahitaji vyuo vingi] ambao honestly ukiangalia kwa makini wangeweza kabisa kulipwa wote kwa asilimia mia moja bila kuathiri sekta nyingine. Kama tungekuwa tunazingatia kuwa hizi fedha ni mikopo sio misaada, niliwahi kuandika huko nyuma kuwa ukiangalia ni kama msaada kwa vile hamna utaratibu wa kurudisha. Kama wanafunzi japo elfu kumi waliowahi kupata mkopo wangekuwa wanarudisha kiasi cha shilingi elfu kumi tu kwa mwezi kila mmoja hii ingekuwa ni sawa na milioni mia moja kwa mwezi, bilioni moja nukta mbili kwa mwaka! Sasa hiki ni kiwango cha chini sana kuweka lakini tukiweka takwimu halisia ni kuwa tuna wanafunzi waliowahi kuchukua mkopo zaidi ya elfu kumi na wanaweza kulipa zaidi ya elfu kumi...

4. Kama shirika la mikopo ya wanafunzi lingefanya kazi kama mashirika ya NSSF,PSPF nk ingekuwa ni fursa nzuri kwao, wapewe mtaji kwa njia moja iweze kuwekeza na kuwakopesha wanafunzi kutoka matunda ya uwekezaji huo huku wakiendelea kukusanya malipo kwa upande mwingine.

5. Tukubali kwamba mambo ya mikopo yalipoanza hakukuwa na utaratibu mzuri wa kuchanganua nani alipwe nani asilipwe, nilipokuwa Dar miaka miwili iliyopita baadhi ya jamaa niliosoma nao Tambaza wakiwa wanafanya shahada ya pili walipewa mikopo! Kuna walakini katika mfumo huu.

6. Bado inawezekana kujipanga upya wakaweza kuanza vizuri in time for September. Vinginevyo tunaweza kuwa na vigezo vingiii lakini visisaidie...
 
Saidi uliyosema ni kweli acha hata UK bali Kenya wenyewe bodi ya mikopo ya vyuo vikuu inafanya kazi vizuri sana. Hapa waliparamia hii program bila ya maandalizi ya misingi both istitutional and legal aspects ili kuwaridhisha warold bank na IMF kwenye sera zao za cost sharing. Wanatakiwa wakae chini wapange zaidi, huu mfuko unaweza ukafanya kazi vizuri tuu kama mifuko mingine kama watarekebisha kasoro ambazo nadhani bado ni nyingi sana.
 
mkuu Samvulachole hebu anika hayo maswali hapa nadhani hawa jamaa wa loan bord wakipita humu yanaweza kuwasaidia mkuu.
 
kila siku mtasikia vigezo vya mikopo, hivi na hivi na vile. lakini mshawahi kusikia mtu yeyote mmoja tu unayemjua amepata huo mkopo ? mimi sijawahi
 
Hawa jamaa wanarudia makosa yaleyale. Unapotoa mashartia hayo leo karibia na mwezi wa June, uteuzi wa watakaopata mkopo utafanyika kwa muda gani na ni vipi wataweza kupitia na kuhakiki fomu zaidi ya elfu thelathini kama sio zaidi kwa muda huo.

Ushauri wangu masharti waliyoyatangaza sasa yatumike kwa watakaojiunga na vyuo 2008/2009 ambao watakiwe kuanza kufanya maombi ya awali mkopo tangia wakiwa kidato cha sita na baadae kuthibitisha maombi yao mara tu majibu ya kidato cha sita yatakapotoka. Hii itaipa bodi muda wa kutosha kufanya uchanganuzi wao kwa uhakika zaidi na utatoa nafasi kwa wanafunzi na wazazi kujipanga vizuri na majukumu yao.


Tanzanianjema
 
1. Wale waliosoma kwa mikopo kuna haja ya kuwekewa utaratibu warudishe. Ni rahisi bila hata hivyo vitambulisho vya taifa inawezekana. Kwa mfano ikiwekwa sheria/kanuni kwamba kila mwajiri wa Tanzania anaeajiri 'graduate' wa vyuo vikuu lazima afanye makato maalum kwa mfanyakazi huyo yatakayopelekwa TRA/MAMLAKA MPYA YA KUKUSANYA FEDHA HIZI ZA MALIPO YA MKOPO na mlipaji awe ametia saini kabisa kukubali kisheria kwamba analipa mkopo wake. Kiwe ni kiwango kidogo kinachoendana na mshahara wa mhusika.

2. Ikifanyika hivyo manake ni kuwa kutakuwa na hela toka kwa wananchi wenyewe waliowahi kuchukua mkopo, ambao watakuwa wanafadhili wanafunzi wengine. Kutakuwa na mzunguko maalum wa fedha zinazolipwa na kukopesha wanafunzi wengine. Hii ndio ilivyo kwa STUDENT LOANS COMPANY hapa Uingereza.

Kaka Said mbona haya yote yapo katika sheria ya kuanzisha bodi ya mikopo 2004 na kutiwa sahihi na rais mwaka 2005. Ipitie katika website ya serikali ama ile ya bunge. Hata ufuatiliaji wa hilo tayari umeshika kasi.

Tatizo ni kuwa wengi wa hao wanaotakiwa kulipa walilazimishwa kujiunga na mpango huo wa mikopo katika hali fulani ya vitisho. Wengi walilazimishwa kujaza fomu hizo kama sharti la wao kurudi chuoni mara baada ya chuo haswa UDSM kufungwa kutokana na migomo mbalimbali inayohusiana na suala hilohilo la mikopo. Kitu ambacho kinabatilisha uwezo wa kisheria wa mikatba ya mikopo hiyo.

Fomu zilizotumika zina makosa mengi kisheria na hata hiyo sheria inakiuka vifungu muhimu vya katiba. Yaani mikataba hiyo kwa kweli ni dhaifu sana kisheria na wala haihitaji mtikila kuipiga chini kabisa kisheria.


Ni wazi tuna safari ndefu hapa......

Tanzanianjema
 
Bodi ya mikopo yenyewe ina mapungufu mengi mno.

Moja ni ukosefu wa watendanji waaminifu. Wengi wa watendaji wakuu ambao wamekuwa katika kazi hiyo kwa miaka mingi wanahusika na ulaji mkubwa wa mikopo na scholarship hewa kwa miaka mingi.

Wale walioajiriwa karibuni wengi ni wajanjawajanja wa mjini na wengine wameingia humo kwa upendeleo kama kawaida yetu. Tunajuana maana tunatambiana sana mitaani. Sidhani kama wana uwezo wa kutenda majukumu yao kwa nidhamu inayohitajika ili kufanikisha zoezi hilo la uchambuzi wa waombaji wa mikopo hiyo.

Vilevile bila ya watu binafsi kujitokeza na kusaidiwa na serikali kuanzisha mifuko binafsi ya kutoa mikopo kwa wanafunzi ni wazi Bodi ya Mikopo itakuwa inakinzwa na presha kubwa ya maombi kitu ambacho kinaongeza uwezekano wa rushwa na ubadhirifu.

Tanzanianjema
 
nikisikia bodi ya mikopo, mkukuta, mikataba, barabara za juu, mabasi ya kasi, sijui helikopta ya viongozi wa juu ili kupunguza foleni, bustani kubinafsishwa, mara mlimani, mara ukraine na kadhalika naona kama presha inapanda tu !! ndio maana saa nyingine naamua kuchunia ishu hivi hivi au kutozipa uzito unaostahili ( which is not bad )
 
Kweli kaka kadampinzani.

Wahenga walisema Ujuvi ni mateso. Tena zaidi unapokuwa kizazi kipya. Kama ndugu yangu ni wa enzi zile basi ujue kuna tunao umia zaidi yako.

Tanzanianjema
 
Mimi naona serikali yetu inakizunguzungu kama sio kuchanganyikiwa hasa hiyo wizara ya Msola maana matatizo mengi ya elimu ya juu yanaepukika kama hii wizara ingekuwa na viongozi na watendaji makini. Issue kama Ukren na UDSM zisingetokea. Wanaingizia nchi hasara tuu, chuo kilifungwa na usumbufu mkubwa uliwapata vijana wakati kodi zetu ziliendelea kutumika kuendesha chuo bila sababu za msingi.
 
Mtoto wa Mkulima,

Hawasikii hao, na kwa kuwa wapiga kura tumelala, basi wataendelea kutunyanyasa.
 
Hivi kwanini wametangaza suala hili wakati wa suala la wanafunzi wa Ukraine linapamba moto? Inawakumbusha serikali kutangaza mambo ya RCD wakati wa suala la Zitto na Amina... ? Halafu utaratibu huu mpya unawaathiri vipi wale waliokwisha pewa mikopo?
 
Wanafunzi 11 wa kigeni washikiliwa Chuo Kikuu

2007-06-10 10:13:16
Na Richard Makore

Wanafunzi 11 wa kigeni, wanashikiliwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa tuhuma za kujipatia mikopo ya mamilioni ya fedha kwa njia ya utapeli kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Yunus Mgaya, aliiambia Nipashe katika mahojiano maalum juzi kuwa, wanafunzi hao wanatoka nchi jirani.

Profesa Mgaya alizitaja nchi wanazotoka wanafunzi hao kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda na Kenya.

Alisema baada ya uongozi wa Chuo kubaini utapeli huo, ulichukua hatua ya kuwasimamisha masomo mara moja.

Alisema hivi sasa taratibu zinaandaliwa za kuwatimua nchini.
Kwa mujibu wa Profesa Mgaya, wanafunzi hao walikuwa wakisoma kozi katika vitivo vya Uhandisi, Biashara na wengine bado hawajajulikana walikuwa wakichukua kozi gani.

Hata hivyo, Profesa Mgaya aliitupia lawama Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwamba ina udhaifu mkubwa uliosababisha kushindwa kuwabaini matapeli hao.

Alisema udhaifu wa Bodi hiyo, umesababisha wanafunzi hao wa kigeni, kujipatia mamilioni ya fedha ya mkopo huku wakiwepo mamia ya Watanzania wanaohitaji mikopo hiyo.

Sheria ya nchi inaeleza kuwa, walengwa wa mikopo hiyo ni Watanzania tu.

Profesa Mgaya alisema idadi hiyo ya wanafunzi 11 wa nje, ni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tu na kwamba iwapo utaendeshwa msako maalum kwa vyuo vyote nchini, hapana shaka watanaswa matapeli wengi.

``Hii ni aibu na fedheha kubwa kwa Taifa na mpaka sasa sijajua mchezo huu unafanywa na nani huko Bodi ya Mikopo kwa kuwa haiwezekani mgeni afike nchini na kuchota fedha hivi hivi,`` alisema.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu tangu ilipokabidhiwa jukumu hilo, imekuwa ikilalamikiwa na Watanzania wanaoomba mikopo kwa madai ya kuwa ina urasimu.

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/06/10/92261.html
 
Vipi vijana wetu Ukraine? Bodi ya mikopo wanasemaje? Polisi waitwe wachunguze wanafunzi wote kwenye vyuo vikuu na Serikali iunde tume huru kuchunguza Bodi yote kwa ujumla.

I wonder wabunge wako wapi? Matatizo gani wanatatua?
 
Hatuhitaji ushahidi kutoka kwa Mungu kuthibitisha kwamba Bodi ya mikopo na Serikali ya CCM wameikumbatia Rushwa na hawataki kuiachia kwa sababu inawatia joto na kuwaletea unafuu haramu wa maisha. Pia kwamba serikali ya CCM ni serikali ya Kifisadi.

Kauri za serikali ya CCM na watendaji wake zinapingana na hazichangamani kama maji na moto.
Wanataka tuamini kwamba chemchem yao ina uwezo wa kutoa maji ya moto na baridi kwa wakati mmoja jambo ambalo hata Ibilisi mwenyewe hana uwezo wa kulifanya.

Serikali ya CCM iko hatua moja Mbele ya Ibilisi kwa mazingaombwe ya aina hii.

Watanzania 26 walioko ughaibuni kule Ukireini waliahidiwa mikopo na Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu, kisha wakapigwa chenga na watendaji wa Bodi hiyo. Bila shaka chenga hizi za kiuendawazimu zimeanza baada ya barua na vithibisho vya kuwakopesha mikopo kuvurugwa kwa makusudi na magwiji hawa wa rushwa ili kukidhi hamu yao ya kimumiani ya kukomba mapesa yote kutoka mifuko ya Watanzania wenzao kwa ulafi.

Baada ya kuruka kimanga chetu, huku mafisadi hawa wakisaidiwa na kauri ya Mkuu wa nchi MH Jakaya Mrisho Kikwete kwamba serikali haiwatambui wanafunzi hawa, mafisadi hawa wa Bodi ya mikopo wameendelea kuchekelea kwenye matumbo yao pakacha huku wakijua fika kwamba wanaficha ufisadi mwingine ulio kubuhu na mkuu kuliko wa kwanza wa kuwakopesha Manyang'au kutoka nchi jirani fedha ya wavuja jasho wa Tanzania.

Kisiasa watendaji wa serikali ya CCM pamoja na bodi ya mikopo ni Malaya ni Malaya wakubwa.


Ni vipi Rais mzima wa nchi mwenye mamlaka yote ya kiutendaji akubali jibu la juu juu la watu ambao wako chini yake bila hata kudodosa?

Je Malalamiko ya Watanzania juu ya Bodi ya mikopo amabayo yamekuwa yakitolewa na Watanzania kwa muda mrefu sasa hayamfikii Rais Kikwete?

Je hii ndiyo ahadi ya Rais Kikwete ya Kuwatumikia Watanzania wote kwa uwezo wake wote?

Je Rais Kikwete kuwapa kiburi watendaji wa Bodi ya mikopo haoni kwamba anaendeleza ujenzi wa utamaduni wa kulindana ndani ya serikali ya CCM?

Je Rais kikwete anakubali kwamba jambo hili limeonyesha sehemu ya udhaifu wake katika kushughulikia kero za wananchi?

Je Rais kikwete haoni kwamba Kauri yake ya kuitetea bodi ya mikopo inawalinda wahalifu hawa na kuwapa nguvu wahalifu wengine wote ndani a ya serikali ya CCM ambao nyanja zao hatujazigusa?

Je Rais kikwete yuko tayari kulishughulikia suala hili kwa nguvu zake zote kama mkuu wa nchi ili kutimiza ahadi yake ya kuwatumikia watanzania wote?

Profesa Msolla je anaiendeshaje wizara yake?

Au kwa vile Prof. fani yake ni kuchoma sindano ng'ombe na mbwa kesha tuona siye wote ni wanyama?

Kuna mambo yanaudhi naweza kumtoboa mtu shimo kwenye bichwa lake na hili gobore langu la mfukoni.

Sasa utashangaa pamoja na ushahidi kama huu wa bodi ya mikopo kukopesha fedha wageni Wakereketwa wa CCM bado watasimama kidete kutetea ufisadi.

Hee nyie vipi mmetumwa na vyanma vya upinzani nini?
Huu si mkopo tu watarudisha si wanatoka hapo Kenya tu!!
Na maneno kwamba "ninyi watu mlioko nje ya nchi mna wivu sana na mnajidai na kusoma kwenu kwanza mkimbia nchi sasa mnalalama nini.
Mabox yemewaotesha vipara na shule zimewashinda.

Nawaahidi ninyi mano tetea ufisad kwamba mtaendelea kusota kwenye mbigili huku mkiwa ****** wazi mpaka mwisho wa maisha yenu.
Kama mnataka mabadiriko ya kweli Muda ni huu wa kupinga ufisadi wa serikali ya CCM.

Kuna mijitu itaendelea kutetea ufisadi huu hata kama yenyewe pia ilikosa kupata elimu ya juu kwa sababu serikali ilidai kuwa haina fedha. Kumshabikia mtu anakupa maumivu sijui ni ushujaa au Uhamnazo?

CCM wataendelea kuwafanya nyie Punda Wa dobi na kuitekeleza siasa yao ya Ufisadi juu ya vichwa vyenu na juu ya vichwa vya vilembwe wenu.

Kitendo cha serikali kutoa matamshi kwamba haina fedha za kusomesha watu nje ya nchi na hata ndani ya nchi na wakati huo huo kuwasomesha wageni ndani ya vyuo vyetu kwa fedha yetu wenyewe ni hatari kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na ni dalili kwamba CCM sasa ni ya wachache wengine mnajikomba tu au mnaendeleza uanachma ili mradi muwe na chama.

If you support CCM as a political Party you do that on your own risk. But if you support it as a gang, as in MAFIA, you know the whole deal, keep up.

Ni Watanzania wangapi wanasoma Kenya kwa fedha ya Wakenya?

Hivi sisi ni wapumbavu kiasi gani au tuliumbwa na akili taahira kiasi gani mpaka tunathamini wageni kiasi hiki na kuwapa nafasi kibao za kazi wao kwanza na kuwapeleka wao kusoma badala ya watoto wetu tena kwa fedha zetu chache?????

Si hivyo kuna wageni wengi sana wamepata Scolaship zinazotolewa na nchi tajiri kama Marekani Uingereza ujerumani ambazo walengwa ni WaTanzania.

Mcomoro mmoja aliwahi kuniuliza hivi kwenu hakuna watu wanataka kusoma?

Nikamwambia wako wengi sana.

Akaniambia yeye amesoma na Watusi wengi kutoka Rwanda na Burundi wakiwa na scholarship kutoka Tanzania.

Nikamwambia kwamba tunatatizo la rushwa.
Jibu lake likawa hiyo siyo sababu kwani hata kwao wao wana tatizo la Rushwa pia lakini bado wageni hawapewi kipaumbele cha kuchukua nafasi za wenyeji.
Nilibakia domo wazi kama chewa moyoni nilijua kwamba alikuwa akiniambia kwamba ninyi mna tatizo kubwa zaidi ya Rushwa.

Serikali ya CCM inatatizo kubwa zaidi kuliko Rushwa.Kuna nguvu ya Ibili ambayo inaendesha shughuli za kila siku za serikali ya CCM. Kila mtu ndani ya serikali ni mwoga anaogopa kitu fulani.
Ni kitu gani ndnai ya serikali ya CCM kinatisha?
Maana hii inaonyesha kwamba hata rais kikwete Meno yote aliyo nayo na kubweka kote aliko bweka miezi 12 ya kwanza ya Utawala wake hana uwezo wa kuuma.
Rais naye kuna mahali akifika anaingiwa na hofu kuu kiasi kwamba hata mjumbe wa bodi ya mikopo hawezi kuulizwa sawali.

Ndani ya CCM najua Kingunge Ngambale mwilu ndiye dume lao yeye anahirizi zote za CCM.
Yeye ndiye aliye mtia adabu na stop Mzee Malecela wengine wote Pu#@u zao zilikuwa ndogo kuhimili vishhindo.

Sasa sijui kama rais Mzima anaogopa watendajiwake ni vipi anaweza kuyaamuru majeshi na bunduki zao???

Serikali ya CCM haiwezi kubadirika hata siku moja. Tunao takiwa kubadirika ni sisi wananchi ambao tunaliwa kila uchao wakati wao wanapanga mbinu za kuendelea kuneemeka.Kama ni kuiweka serikali hii madarakani tumeiweka sisi wenyewe pengine kwa kusaidia harakati za kuiba kura, shs 10,000 au ushabiki wa rangi ya kijani.
Siku zote kama kuna matatizo yanayotokana na utendaji wa serikali ni sisi tutakao umia.

Serikali safari hii itakaa kimya au itasema wale wageni wanasomeshwa na serikali ya Tanzania kama ni sehemu ya zoezi la kuimarisha East Afrika kama unavyojua ni majirani zetu?
Sijui! Maana serikali yetu huwa inatoa jibu lolote kwa jinsi inavyjisikia kama lmevi wa gongo.

Kwa mtu mwenye mtizamo finyu suala la wageni kukopeshwa fedha za walipa kodi si hoja hasa kwa vile wanazitumia pale univeristy of DSM. Lakini kama umewahi kukaa nje ya tanzania unajua maana kuwa ughaibhuni. huku ughaibhuni hapendwi mtu. Ule usemi wa mwalimu Nyerere kwamba Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja unaishia kwenye mipaka ya Tanzania kama siyo kwenye vitabu alivyoandika tu.
Sisi tulioko nje tunajua fika kwamba hakuna undugu huku ni unyama unyama tu.
Sasa huu ukarimu wa watendaji wetu unatoka wapi?

Mashirika ya kigeni yanajiri Wakenya na Waganda kwa kisingizio kwamba wao ni Bora kuliko sisi eti ni Presentable. Sasa kama hata vyuo vyetu watasoma wao basi tuanze kutafuta miti na vichaka vya kujihifadhi kule Mikumi kwani tofauti yetu na nyani itakuwa ni kuto kuwa na mkia tu.

Nakuomba Mzee MWanakijiji umwage vitu hivi hadharani pia naomba maswali niliyo uliza hapa usaidie kuniulizia kwa Wasikilizaji wako, Watanzania na MH Rais Kikwete mwenyewe kupitia mtandao wako.
Ninakuombea kwa Mungu akubariki wewe pia aibariki nia yako njema kwa nchi yako Tanzania. Ameni
 
Back
Top Bottom