Attention: Apps zifuatazo ni hatari zaidi kwa uhai smartphone yako

Moo Click

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
3,495
3,237
Apps zifuatazo ni hatari zaidi kwa uhai smartphone yako
Du booster,Clean master na 360 security
Du booster na clean master zinafanya kazi ambazo wengi wetu

tunazisifia kuwa zinapandisha speed ya simu na zinasaidia battery
kutoisha haraka(optimization) kitu ambacho sio kweli
Kwa nini nasema hivyo?

Hizi apps huwa zina clear cache za apps nyengine kitu amabacho kina punguza speed ya simu na sio kuongeza,kwa nini?

Cache kazi yake ni kutunza kumbukumbu za app fulani hivyo inafanya app i load haraka itakapofungukiwa tena mfano camera clean master inapofuta cache za camera ina maana camera itakapo funguka tena inabidi ianze kujikumbusha upya hivyo inapelekea speed ya ufanyaji wake wa kazi kushuka(ni kama mtu akuekee miba kwenye njia uliozoea kupita)
ndio mana kila wakati clean master inakuwa na junk files kwa kuwa huwezi kuzuia apps kutengeneza cache...

ushawahi kujiuliza kwa nini hizi junk files haziish wakati nisha zifuta?

Huwa zina clean RAM kitu ambacho hakina faida kwa sababu kwa android kwa sababu yenyewe huwa ina force app fulani inayokula RAM kujifunga wakati baada ya mda mfupi tu ile app

itajifungua tena yenyew kwa sababu android ina true mult tasking hivyo huwezi kuzuia app fulani isijifungue hii process inafanya hizi apps ziwe zina run mda wote na kumaliza battery yako
Pia hizi apps huwa zinajipa ruhusa amabzo wew kama mtumiaji wa simu hujazipa
hii tabia ni yaki''malware'' inakuwa na uwezo wa kuiba data zako na kufany
mambo mengi ambayo wew hujapenda iyafanye.

Kama unatumia android system kuanzia 5.0 huna haja ya hizi apps kwa kua mfumo wenyewe wa
android umakupa uwezo wa ku optimize battery yako kwenye setting ya battery usage
au tumia power saver

Pia kama storage ya simu yako inakusumbua system yenyewe ina smart manager ambayo inakuruhusu kufuta vitu vyote ambazo sio muhimu kwenye simu yako

NB:Kwa watu amabao wanamatumizi makubwa ya RAM zao mfano wanaocheza sana ma game angalau utumie app

ya Greenify ambayo uzuri wake inafanya kazi kuanzia kwenye hardware level na sio software level
Next time ntakuja na apps zinazonyonya zaidi battery yako na kuia haraka

Nawasilisha
 
Sawa tumekuelewe ila ni bora simu ife ununue nyingine mambo ya kukaa na simu miaka 7 nyie ndio mnarudisha nyuma uchumi wa nchi hii
nyie mnaotumia simu siku moja na kuzitupa ndio mnafanya Guangdong (Guangzhou) itajirike
 
Na izi ambazo samsung wame weka kwenye setting yao kabsa vp
Screenshot_20191016-201108_Device%20care.jpeg
 
Back
Top Bottom