Atoweka nyumbani baada ya kupata ‘0’ matokeo ya kidato cha nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atoweka nyumbani baada ya kupata ‘0’ matokeo ya kidato cha nne

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Feb 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,912
  Trophy Points: 280
  Friday, February 12, 2010 10:41 AM
  MSICHANA Joyce Aloyce [18] mkazi wa Shekilango jijini Dar es Salam, ametoweka nyumbani kwao baada ya kupata majibu yake ya kidato cha nne yaliyoonyehsa amefeli mitihani hiyo na kupata divisheni 0.

  Msichana huyo ametoweka nyumbani kwao na hajulikani alipo na mama yake kupata na wasiwasi na kujua mwanae huyo yuko wapi na hajui pa kumpata wapi.

  Mama huyo aliyekutana na Mwandishi wa habari hii katika kutuo cha Urafiki cha jijini akija kuripoti tukio hilo kwa msaada zaidi.

  Mama huyo aliiambia nifahamishe kuwa binti yake huyo hamuoni takribani wiki sasa na kusema toka matokeo hao yatoke na kujigundua kuwa alipata ziro basi hakurudi nyumbani hapo kwa kuhofia kufukuzwa nyumbani kwao hapo kwa kuwa mzazi ake wa kumu alishamwambia awali kabla ya matokeo.

  Alidai walipoona kinywa kinazidi walijaribu kupita kwa ndugu zao wa karibu ambao wangehisi labda angekuwa huko lakini bila mafanikio hawakuweza kumkuta wka ndugu yoyote na kutojua yuko wapi kwa sasa.

  Alidai kutokana na hali hiyo familia hiyo wameanza kuogopa na wamekuja kuripoti kituoni hapo na taratibu zingine zinaendela za kwenda kumsaka na mikoni huenda atakuwa amekwena kujichimbia huko kwa kujhofia aibu na kupigwa na baba yake.

  Mama huyo alidai binti huyo ni mtoto wake wa pili na kuonyesha huzni kubwa kwa kuwa motto wa kike katika familia hiyo hiyo aliuwa jni yeye tu kati ya watoto wannne alio nao.

  “Mimi naweza kumsamehe hata akirudi nyumbani ila mume wangu sijui kama ataweza kumsamehe, wanaume wanakuwa wakali hata watoto wanawaogopa sasa mwanangu ametoweka nyumbani kwa kumuogopa baba yake” huku akionekana kutokwa na machozi kwa mkasa huo uliomkuta

  NIFAHAMISHE ilijaribu kuchukua mawasiliano ya mama huyo na lolote litakaloendelea mtafahamish
  wa
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  sasa toto badala ya kupiga shule linashinda club na kusikiliza miziki kwenye ipod unategemea nini? unakula ugali wa bure kila kitu unapewa huna sababu ya kufeli..namuunga mkono dingi...
   
 3. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 596
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Daa hapa Tunahitaji mapinduzi ya Elimu na si chama cha mapinduzi!!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...