Atolewa jela, aapishwa, arudishwa gerezani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Diwani wa Kata ya Bumera kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tengera Marwa jana alitolewa gerezani kwa muda na kwenda kuapishwa wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na baadaye alirudishwa gerezani.

Diwani huyo yuko rumande tangu mwanzoni mwa mwaka huu akituhumiwa kwa mauaji na hata fomu za kugombea udiwani alipelekewa rumande na kufanikiwa kumshinda Katibu Uenezi na Siasa wa CCM wilaya ya Tarime, James Nokwe katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.

Aliletwa katika kikao cha kwanza cha madiwani kwa kibali maalum baada ya kuwapo kwa mvutano baina ya madiwani wa CCM na Chadema, hasa wakielewa kuwa kilichofuata baada ya kuapishwa ni uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri.

Pamoja na `kura’ ya ziada ya Chadema, bado haikuambulia kitu, kwani CCM walikuwa na idadi kubwa ya madiwani na hivyo kushinda kwa urahisi nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na pia Naibu Mwenyekiti.

Aliyeshinda nafasi ya Mwenyekiti ni Amos Sagara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Tarime aliyepata kura 26, kura 25 zikiwa za madiwani wa CCM na nyingine kutoka kwa Charles Mwera mbunge wa zamani wa Tarime kwa tiketi ya Chadema ambaye kwa sasa ni diwani wa Kata ya Itiryo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imenyakuliwa ni Sylvester Marwa Kisyeri pia wa CCM aliyemshinda Riziki Mosama Mwita Mwita.

Mara baada ya uchaguzi huo uliohudhuriwa na madiwani 41, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangweni wa CCM aliwasa madiwani hao kufanya kazi kwa kujituma kama walivyowaahidi wananchi waliowapigia kura na kuonya kuwa, kuanzia sasa milango ya ufisadi imefungwa huku akisema watafuatilia kwa karibu fedha za miradi ya halmashauri hiyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom