Atoboe au aendelee kuficha siri?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atoboe au aendelee kuficha siri?!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kisoda2, Jul 8, 2009.

 1. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Lucy kutoka Dodoma,ameolewa na mume mzuri tu na wamepata mtoto mmoja wa kiume umri wa miaka miwili sasa.
  Katika ndoa yao wamehangaika kumtauta mtoto zaid ya miaka minne.
  Ilifikia Lucy akamweleza mai husband wake wakapime kuona tatizo liko wapi ila mumewe aligoma na kujisifia yeye ni kidume cha mbegu,hivyo hana tatizo lolote katika hilo.Mumewe Lucy kutokana na tatizo hilo alianza kujitumbukiza katika ulevi wa kupindukia ili kufuta soo.
  Lucy akajiiba mwenyewe na kwenda kupima nae akajikuta yupo safi kabisa.
  Ndipo alipojaribu kuongea na mdogo wa mumewe ambaye ni pacha juu ya tatizo lilopo baina ya wanandoa hao.Mazungumzo hayo yalipelekea Lucy na pacha wa mumewe waingie katika kuivunja amri ya sita kwa siri,na Lucy akapata ujauzito ambao ndo umewapa huyo mtoto wa kiume(2yrs).
  Mtoto alipopatikana mapenzi yamerudi kama mwanzo na jamaa anampenda mkwe na mtoto kuliko maelezo.

  Tabu inakuja hapa sasa,pacha alietia mimba anamtaka shemeji yake waendelee na kula bata kwa kisingizio la sivyo atatoboa siri na kumdai mtoto wake.
  Lucy amechanganyikiwa ataanzaje kumpa tena jamaa uroda,ama amweleze ukweli mumewe juu ya siri hiyo iliyo sirini.

  Naomba kuwasilisha hoja tafadhali.
   
 2. T

  The Tank New Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lucy aseme kweli tu maana ataficha mpaka lini? Na huyo pacha wa mume wake ataendelea kumsumbua pia makosa yako kwa mwanamume kwa sababu ya ubishi wake wa kutokwenda kupima akasababisha lucy afanye dhambi.
   
 3. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kasheshe ..hii balaa kubwa. sasa huyo pacha anamtishia nini, yeye ana mke? kwani kama ni mimi Lucy ningemwambia mkewe so that its a draw! la sivyo wote waendelee kujienjoy ...cha kufia nini they have done it once wouldnt hurt to continue....infact hebu muulize Lucy kama machezo wa mapacha unafanana...mikwaruzo ya mamba!!!!!ah!
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  huyu binti anayeitwa Lucy ndo kaanza kulikoroga..kwa sababu haijathibitishwa kitabibu kama mumewe halali ana tatizo..sasa kiranga chake tayari keshachomoka, na madhara yake ndo hayo!

  nini miaka minne, watu wanakaa miaka kumi na wanapata watoto? huyo mumewe kasoma ngumbaru au? mambo mengine.....

  by the way ndoa kwani lazima iwe na watoto?
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, mimi nimeshuhudia wanandoa waliokaa miaka 17 bila ya mtoto lakini wakawa wanaishi kwa raha na ufanisi mkubwa wa maisha. Ni mwaka jana tu wamejaliwa watoto mapacha wa kiume na Kike. Ndoa imezidi kunawiri hata kuwafanya warudi kama vijana waliooana miaka miwili iliyopita. Watoto kwenye ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu, mapatano ni ya watu wawili( mke na mme),watoto kuwepo ama kutokuwepo ni mpango wa Mungu.
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kalikoroga mwenyewe na alinywe sasa
   
 7. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwani ye Lucy Hakujua tabu atakayoipata baabdae? aendelee tu kumpa uroda ili apate na watoto wengine,kwani damu ni ile ile tu haina shaka.!
  KIZURI KULA NA NDUGUYO.
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  asingemweleza lengo lake, angetembea nae ajishikie mimba kimya kimya then amuache, sasa maelezo yalikuwa marefuu mpaka yanam cost kwasasa, some people bwana wanajitafutiaga kero za maisha wenyewe....hivi we mtu upo kwenye ndoa unatoka nje ya ndoa yako kwa maelezooo marefuuu juu ya mumeo ili iweje? hata kanma ni ndugu wa mume hakustahili kuyajua hayo.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  nyamayao, wengine hawajui nini cha kusema na nini cha kuacha, in fact kwa nini atoke in the first place? hakuna justifiable reasons
   
 10. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Kwa hiyo kuna kutoka kwa kimya kimya?
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  hahaha...kulinywa ndo naona inakuwa ngumu apo...
   
 12. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na huyo shemeji sasa ameamua kumnyanyasa mwenzake, kama aliamua kumsaidia anataka nini tena, tenda wema uende zako yeye anataka riba.
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  lengo lake lilikuwa kutamfuata mtoto, basi angetafuta kimya kimya, hayo maelezo mengine asingeyapa nafasi.
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  na matokeo yake yatafumaniwa! na itakuwa mbaya zaidi.
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  asaidiwe vipi, katoka na bado kalikoroga, hana msaada! yeye aachane tu na huyo shem wake na kuanzia hapo awe tayari kwa lolote.
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Si ndo hapo sasa dada yangu. Na sie wanawake nao sometimes tunabore hatujui tu. We ushaamua kutoka nje utafute mtoto kuna haja gani ya kuanza kumsimulia maudhui mlengwa? Angejilengesha tu kisha huyoooo lol (utadhani mazuri )

  Pole dada Lucy huna la kujitetea afadhali hata baba angekuwa amethibitika hawezi shughuli ndo ungekwenda huko angekufikiria msamaha
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aachane na huyo shemejo mkware, akitishia kuja kumwaga radhi nae atishie kumwadhiri kwa kumsingizia kumbaka- akaogopa kusema asijeharibu undugu alipoona ameconceive akaamua kukaa kimya kabisa kwa kuwa walikuwa wanahitaji mtoto. lol

  Yaani hapa hana jinsi...
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  ndio hapo sasa wangekaa wapange, yeye kajitokea mwenyewe bila kudhibitisha chochote sasa hivi ngoma imemshinda kuicheza....lol
   
 19. K

  Kilambi Member

  #19
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dada zetu na nyie bana aaah! mara nyingi huwa mnachukua maamuzi ambayo yanakuja kuwagharimu mbele ya safari, hebu badilikeni wajameni. jaribu sana kutafakari kabla ya kutenda. siku za nyuma kulikuwa na habari kidogo kama hii toka kwa mwanadada mwingine nadhani anaitwa mainda, sijui nae aliishia wapi. amkeni dada zanguni
   
 20. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Bibie kwa ushauri wako naamini kabisa jamaa hatothubutu tena kumsumbua mwanamama..
   
Loading...